Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 5,759
- 7,573
Wakuu, sikilizeni habari hii ya ajabu! Ni habari ya mama mmoja ambaye kila alipopata ujauzito, alizaa mtoto wa kike. Mara ya kwanza, mara ya pili, mara ya tatu - wote wa kike. Alifurahi kuwapata hao, na aliwalea kwa upendo. Hata hivyo moyoni alitamani apate na wa kiume.
Kwa imani, nilianza kumuombea. Yesu aliye hai alisikia maombi, mama huyo akapata ujauzito na kujifungua mtoto wa kiume! Sasa amejaa furaha na shangwe kuu.
Je, na wewe una hitaji hilo? Unahitaji mtoto wa kiume au wa kike na hujapata? Yesu hana upendeleo, anaweza kukutendea muujiza huo hata kama madaktari wamekuambia "haiwezekani." Kinachotakiwa tu ni wewe uombe kwa imani, bila mashaka, wala kusikiliza sauti zinazokukatisha tamaa.
Katika Yn 14:13-14 Yesu ameahidi akisema "nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya."
Tena anasema katika Yohana 16:24
"Hata sasa hamjaomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu."
Biblia ni kitabu cha kweli, na ahadi za Mungu zilizoandikwa katika kitabu hiki ni za kuaminika. Haleluya!!