Tanzia

Pole nyingi na mungu awajalie faraja. Inauma sana lakini mwenyezi mungu kamjalia kila mja wake siku za kuishi hapa duniani. Mungu alimpenda zaidi. Poleni sana wafiwa
 
Pole sana. Ni kwa mapenzi ya Mola alikuja duniani na kwa mapenzi yake amemrejesha kwake kama ambavyo sote tutareja kwake, na kwa wakati autakao yeye!
 
Pole sana ndugu yetu katika jina la JF kwa kupotelewa na Mwanao. Mungu awe nanyi katika hiki kipindi kigumu na kuwapa faraja, Amen.
 
asanteni sana wapendwa kwa maneno mazuri ya faraja. mapenzi ya Mungu yameishatimizwa hapa duniani juu ya mtoto yule. jina la Bwana lihimidiwe daima
 
Mungu wetu ni mwema na anatuwazia yaliyo mema!Sifa na utukufu ni mali yake.Pole sana ndugu yangu,Mungu aliekupa ndo aliechukua,na akupe faraja katika kipindi hiki kigumu kwako.
 
Pole sana Mtu Mmoja, sote njia moja tunatofautiana tu siku na saa. Inauma lakini, dah...
 
wapendwa, Mungu wetu ni mwema siku zote na uaminifu wake wadumu vizazi hata vizazi. nawashukuru sana kwa kututia moyo na kutupa nguvu ya kusonga mbele. Mungu awabariki sana.

mama pia amefarijika sana kwa maneno yenu na anawapa salamu za shukrani na heri
 
Mkuu,
Mungu akufariji, na akujalie furaha itakayochukua machungu uliyoyapata.
Tuko pamoja nawe wakati huu mgumu sana!
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom