Tanzia

Maskiniii jamaniiii hata nashindwa cha kusema pole sanaaaa ndugu yangu tuko pamoja kwa sala.....jikaze umpe nguvu mama mtoto ni ngumu sanaaaa lkn Mungu ana mipango yake. Raha ya milele ampe ee bwana na mwanga wa milele amuangazie,apumzike kwa amani, Amina.
 
Ndugu zangu,

january mwaka huu nilikuja hapa na habari za furaha kuu za kupata mtoto wa kiume (angalia link hiyo hapo chini)

https://www.jamiiforums.com/mahusia...a-kiume-mama-na-mtoto-wanaendelea-vizuri.html

leo hii nina huzuni kuu pia, Mwenyezi Mungu muweza wa yote kamuita mtoto huyo kurejea kwake na kutuacha na majonzi makubwa nisiyoweza kuyaeleza vyema. machozi mengi sana yamenitoka, ila sina la kufanya zaidi.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe

RIP mwanangu mpendwa

mpendwa Mtu Mmoja,

hapa duniani tunayo dhiki, tunajishibisha tu kwa "maganda ya nguruwe"!! lakini huko kwa Baba, hata watumishi wake wanakula na kusaza! (rejea kisa cha mwana mpotevu)

mimi najua kwa hakika huko kwetu (kwa Baba) NI PAZURI!!

wimbo: KWETU PAZURI
kwaya: AMBASSADORS OF CHRIST (kutoka Rwanda)

1.
ninayo hamu, kurudi nyumbani,
nyumbani kwetu ambapo hatutatengana
hapo nyumbani kwetu hakuna makaburi,
wala hakuna vyandarua maana hakuna marelia,
kwetu ni pazuuuri, ni pazuri nakuambia,
najua nawe ndugu yangu unayo hamu kufika huko

kiitikio

kwetu pazuri, nimeishapakumbuka
ninayo hamu kuishi na mwokozi wangu,
kwa amani na furaha tena ya ajabu,
sipati picha kwa watakaokufika kwetu mbinguni

2.
hii duniaa imejaa shida,
kama hujui, nenda hospitali kaone,
lakini kwetu hakuna fani ya tabibu,
watakatifu watachuma majani ya mti wa uzima
wawe na afya, hawataugua,
magonjwa tabu tutaziacha zote hapa duniani

kwetu pazuri....

3.
mpendwa njoo, turudi nyumbani,
asubuhi yaja tuyakimbie ya dunia,
atakayekosa kwa kweli ni hasara,
haya matatizo ni mitego ya shetani ili tushindwe
kufika nyumbani, kwetu pazuri,
lakini kwa jina jina la Yesu tumemshinda tunaenda!!

kwetu pazuri...

Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana libarikiwe

pole sana mpendwa na Mungu awazidishie imani katika kipindi hiki kigumu

msiache kuliitia jina la Bwana wa mabwana
 
Mtu Mmoja, pole sana dear.
Mungu mwenyewe awafariji. Kila linalotupata lina kusudi, na pengine Mungu ameepusha lililo gumu zaidi. Kaa karibu na wife, mtapita tu hili bonde la uvuli wa mauti.
 
mpendwa Mtu Mmoja,

hapa duniani tunayo dhiki, tunajishibisha tu kwa "maganda ya nguruwe"!! lakini huko kwa Baba, hata watumishi wake wanakula na kusaza! (rejea kisa cha mwana mpotevu)

mimi najua kwa hakika huko kwetu (kwa Baba) NI PAZURI!!

wimbo: KWETU PAZURI
kwaya: AMBASSADORS OF CHRIST (kutoka Rwanda)

1.
ninayo hamu, kurudi nyumbani,
nyumbani kwetu ambapo hatutatengana
hapo nyumbani kwetu hakuna makaburi,
wala hakuna vyandarua maana hakuna marelia,
kwetu ni pazuuuri, ni pazuri nakuambia,
najua nawe ndugu yangu unayo hamu kufika huko

kiitikio

kwetu pazuri, nimeishapakumbuka
ninayo hamu kuishi na mwokozi wangu,
kwa amani na furaha tena ya ajabu,
sipati picha kwa watakaokufika kwetu mbinguni

2.
hii duniaa imejaa shida,
kama hujui, nenda hospitali kaone,
lakini kwetu hakuna fani ya tabibu,
watakatifu watachuma majani ya mti wa uzima
wawe na afya, hawataugua,
magonjwa tabu tutaziacha zote hapa duniani

kwetu pazuri....

3.
mpendwa njoo, turudi nyumbani,
asubuhi yaja tuyakimbie ya dunia,
atakayekosa kwa kweli ni hasara,
haya matatizo ni mitego ya shetani ili tushindwe
kufika nyumbani, kwetu pazuri,
lakini kwa jina jina la Yesu tumemshinda tunaenda!!

kwetu pazuri...

Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana libarikiwe

pole sana mpendwa na Mungu awazidishie imani katika kipindi hiki kigumu

msiache kuliitia jina la Bwana wa mabwana

asante sana Miss Judith kwa wimbo mzuri. wimbo huo ni moja ya nyimbo zilizomsindikiza mwangu hadi kwenye nyumba yake mpya. ubarikiwe sana dada yangu
 
asanteni sana wakuu, Mungu ameishatuangalia kwa macho yake ya huruma. Jina lake Libarikiwe
 
Pole sana mkuu, upo wajibu wa kumshukuru Mungu, maana walau Mungu alikupa nafasi ya kuwa na mwanao kwa karibu mwaka. Wako watoto wamefia matumboni mwa mama zao kabla ya kuzaliwa. Huoni wapaswa kumshukuru Mungu! Japo kibinadamu ni ngumu.
Jikaze ili uwe msaada kwa mama wa mtoto kumtia moyo, maana kwa hawa wenzetu kwao huwa ngumu zaidi.

Mungu mwenyewe akutie nguvu, lakini unayo kazi. Huyo ni malaika tu mbinguni ametangulia. Unataka kuja kumwona tena? basi ishi maisha matakatifu kama atakavyo Mwenyezi Mungu, UTAMWONA!
 
Pole sana kwa yaliyokupata ,tunakuombea wewe na mwenzi wako MUNGU awajalie wepesi muweze kuvuka kipindi hiki kigumu. R.I.P mwanetu mpendwa.
 
Ndugu zangu,

january mwaka huu nilikuja hapa na habari za furaha kuu za kupata mtoto wa kiume (angalia link hiyo hapo chini)

https://www.jamiiforums.com/mahusia...a-kiume-mama-na-mtoto-wanaendelea-vizuri.html

leo hii nina huzuni kuu pia, Mwenyezi Mungu muweza wa yote kamuita mtoto huyo kurejea kwake na kutuacha na majonzi makubwa nisiyoweza kuyaeleza vyema. machozi mengi sana yamenitoka, ila sina la kufanya zaidi.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe

RIP mwanangu mpendwa

Poleni sana katika huu msiba mkubwa uliowafika. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na awape nguvu na faraja nyinyi Wazazi, ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu kwenu~AMEN
 
Pole sana mkuu, upo wajibu wa kumshukuru Mungu, maana walau Mungu alikupa nafasi ya kuwa na mwanao kwa karibu mwaka. Wako watoto wamefia matumboni mwa mama zao kabla ya kuzaliwa. Huoni wapaswa kumshukuru Mungu! Japo kibinadamu ni ngumu.
Jikaze ili uwe msaada kwa mama wa mtoto kumtia moyo, maana kwa hawa wenzetu kwao huwa ngumu zaidi.

Mungu mwenyewe akutie nguvu, lakini unayo kazi. Huyo ni malaika tu mbinguni ametangulia. Unataka kuja kumwona tena? basi ishi maisha matakatifu kama atakavyo Mwenyezi Mungu, UTAMWONA!

Pole sana mpendwa, amini Mungu bado anakupenda atakupa chema apendacho kidumu nawe

Pole sana kwa yaliyokupata ,tunakuombea wewe na mwenzi wako MUNGU awajalie wepesi muweze kuvuka kipindi hiki kigumu. R.I.P mwanetu mpendwa.

Hii wiki inaisha leo ninesikia misiba mitatu ya watoto. Kwa kweli inauma sana. Poleni kwa msiba.

Poleni sana katika huu msiba mkubwa uliowafika. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na awape nguvu na faraja nyinyi Wazazi, ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu kwenu~AMEN

asanteni sana wakuu, sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake hakika tutarejea siku moja. Mungu awabariki sana kwa faraja mlizotupatia mimi na familia yangu
 
Oh dear,na imagine katoto ka mwaka mmoja,ndo kameanza kutembea,ndo kameanza kuita 'ma' na 'ba' too sad kukapoteza.Be strong ndugu yangu na Mungu akusimamie katika kipindi hiki kigumu,yote ni majaribu,kaza roho utayavuka.Mpe pole sana na mama pia.
RIP mwanetu.
 
Pole sana Mtu Mmoja ...

Personally I've been there - Ni majonzi makumbwa sana ambayo huwa ni vigumu kuelezeka!

Muombe Mwenyezi Mungu akupatie ujasiri na nguvu na UTASHINDA ... Hiki ni kipindi ambacho Mwandamu ujaribiwa IMANI yake kuliko wakati wowote ule ...

Pole pia kwa mwenzi wako ...
 
Back
Top Bottom