Tanzia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzia

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtu Mmoja, Dec 18, 2011.

 1. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu,

  january mwaka huu nilikuja hapa na habari za furaha kuu za kupata mtoto wa kiume (angalia link hiyo hapo chini)

  https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/106574-nimepata-mtoto-wa-kiume-mama-na-mtoto-wanaendelea-vizuri.html

  leo hii nina huzuni kuu pia, Mwenyezi Mungu muweza wa yote kamuita mtoto huyo kurejea kwake na kutuacha na majonzi makubwa nisiyoweza kuyaeleza vyema. machozi mengi sana yamenitoka, ila sina la kufanya zaidi.

  Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe

  RIP mwanangu mpendwa
   
 2. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Daaaaaah!!Nimeishiwa maneno ndugu yangu,ninachosema ni pole japokua nahisi kama haitoshi vile!Mungu awe nawe kipindi hiki kigumu!Daaah!
   
 3. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,217
  Trophy Points: 280
  Pole sana kwa kweli
   
 4. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  asante sana mkuu, jina la Bwana lihimidiwe! Yeyey ndiye Muweza wa yote
   
 5. Heart

  Heart JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,660
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Pole sana Mtu mmoja....Kazi yake Mola haina makosa. Mungu akujaalie wepesi na akujaze imani katika kipindi hiki kugumu.Pole sana.
   
 6. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #6
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  asante sana mpendwa, sisi sote ni wa kwake na hatimaye kwake tutarejea
   
 7. Jomse

  Jomse JF-Expert Member

  #7
  Dec 18, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pole sana jamani.Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu
   
 8. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #8
  Dec 18, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,217
  Trophy Points: 280
  Kifo cha mtoto mdogo kinauma sana,jamani what hap'd.Ni malaria au nini?Again pole sana
   
 9. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #9
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  asanteni sana wapendwa. yaani nimechimbika moyoni kwa kweli
   
 10. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #10
  Dec 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mpendwa! Pole sana tena narudia pole sana! Najua unavyoumia sana kwa namna ujuavyo ila nakuhakikishia ya kwmb MUNGU atakujaza nguvu na utampata mwingine tu,ni vigumu sana kusema niliyonayo lakini kuwa jasiri kwa kipindi hiki chenye majonzi Mpendwa. Pole sana na Mungu amlaze mahala pema peponi! Amen!
   
 11. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #11
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Pole sana mpendwa; hakuna maneno nitakuyooandika yatakayoleta faraja, kwani naujua uchungu wa kuondokewa na mpendwa wako. Mungu akupe nguvu ya kuendelea kuishi na kumshukuru kwa kukupa hiyo miezi michache ya uhai wa mwanao mpenzi.

  Mungu ailaze roho ya malaika wake mahali pema peponi. Kwa sisi tunasema umepata muombezi huko mbinguni.
   
 12. libent

  libent JF-Expert Member

  #12
  Dec 18, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 385
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  pole sana mkuu hii inasikitisha sana umempata mwanzo wa mwaka na umempoteza kwenye mwisho wa mwaka kifo chake kitakuwa na utata, narudia tena pole sana mkuu
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Dec 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mtu MMoja... pole sana, yani nimesoma hii thread na nimepatwa na depression kabisa, this is tough to take and i pray that you maintain your strength and composure ili umsaidie mama mtoto naye

  Kids are little flowers, they always brighten our lives and broaden our smiles... But we always owe it to the higher one

  Shukuru Mungu umewahi kumuona mwanao, kuna watu wanakesha kwa waganga, kwenye ibada na mahospitali wakitafula mtoto japo wa kumuona kwa sekunde moja

  MSHUKURU MUNGU
   
 14. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #14
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  RIP Mtu mmoja jr..
   
 15. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #15
  Dec 18, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Duh! Hadi machozi yamenilenga lenga. Pole mkuu, jikaze maana kila jambo linalotokea hutokea kwa sababu.
   
 16. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #16
  Dec 18, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Pole sana sana mkuu
  Mungu akujalie lililo jema katika kipindi hiki kigumu. Pole sana sana mkuu. Inauma sana na ni kipindi kigumu sana ila muombe Mungu sana akupitishe katika kipindi hiki kigumu. Pole sana mkuu.
   
 17. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #17
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  asanteni sana wapendwa kwa maneno yenu ya faraja. ni kweli tunapaswa kumshukuru Mungu siku zote kwa kila jambo, naam hata pale mioyo yetu inapofumbwa kabisa kwa simanzi

  Jina la Bwana Libarikiwe!
   
 18. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #18
  Dec 18, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Pole sana. Mungu akujalie nguvu katika kipindi hiki cha majonzi.
   
 19. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #19
  Dec 18, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Magumu yatupatayo ni ya kitambo, Mungu yupo na sisi daima! Usibondeke moyo mpendwa, Mungu wetu ajua sababu ya yale yote tuyapitiao na yeye ndie mwenye kutupa faraja na amani!! Pole saaana mpendwa wetu, pole pia kwa mwanamke mwenzangu i.e mama wa mtoto! Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani malaika wake mpendwa......AMEN!!!
   
 20. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #20
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  asanteni sana wapendwa. namjua Mungu wetu Yeye ni mwema kwetu siku zote. nashukuruni sana kwa faraja.

  RIP my little angel
   
Loading...