Tanzia: Nimepatwa na msiba wapendwa

Tanzia: Nimepatwa na msiba wapendwa

Pole mpendwa wetu,Mungu akupe ujasiri katika wakati huu mgumu.
 
Mungu ni mwema Siku zote.Awatie Faraja yake kipindi hiki Kigumu wewe na ndg.wote wa Marehe.Ailaze mahali panapostahili Roho ya Mareh.Pole Sana Ndg.yangu.
 
Basi pole si ndio unachiokitafuta! wewe hauna ndugu na jamaa wa kuwajulisha kwa kuwapigia simu mpaka uje kuanika mambo yako binafsi humu?

Jamani wewe si mwafrica nini? Wa Africa esp wa TZ tunaheshimu sana misiba na msiba si wa ndugu tu hata jirani marafiki wanahusika sana na wewe unakuhusu, ungana na mfiwa katika majonzi na tuungane pamoja kuwafariji.
 
habari
wana jamvi wenzangu

Nina masikitiko na simanzi kubwa ndani yangu kwani nimeondokewa na
kipenzi changu mwanangu wa ukoo.

Kwa taarifa hii ya jana iliyonishtua na kunipa simanzi zisizopimika
nimeondokewa na kipenzi changu ambaye
ni cousin wangu na kwa upande wa mama yangu mzazi ananiita mama wa ukoo
yaani mwanangu, alikuwa anasumbuliwa na tatizo la appendex ambayo
ilipasukia tumboni na vilevile alikuwa mjamzito na presha ilishuka
chini, jana majira ya jioni alipopelekwa chumba cha upasuaji wakati
wanamfanyia matibabu ndipo akakata roho ameacha mume na watoto wawili,
na leo tunafanya taratibu za kuusafirisha mwili kwenda mkoani kuzika.
sina faraja ingine namshukuru Mungu kwani ndiye aliyetoa na ametwaa
jina lake lihimidiwe, mwenzenu niko so sad. Tutasafiri jioni sana na
tutaaga pale Mwimbili kuanzia majira ya saa nane mpaka saa kumi hivi ila
tunasikiliza kamati ya mazishi itakaposema.
karibuni wapendwa.

Pole mamy. Sote kwake tutarejea.
 
Jamani wewe si mwafrica nini? Wa Africa esp wa TZ tunaheshimu sana misiba na msiba si wa ndugu tu hata jirani marafiki wanahusika sana na wewe unakuhusu, ungana na mfiwa katika majonzi na tuungane pamoja kuwafariji.

Si ndio maana nikampa anachokitafuta POLE KUUBWAA!
 
Pole sana, maandiko yanasema tushukuru kwa kila jambo. again pole sana mpendwa.

Mungu anayetupandisha milimani kufurahi ndio Huyohuyo anayetushusha mabondeni kwenye vilio. Yatupasa kumshukuru kwa kila hali, maana si kuwa hakuona, aliona. si kwamba hakujua, alijua. si kwamba hakuweza kuzuia, uwezo anao. si kwamba alisinzia -Hasinzii. ni makusudi basi mama na mtoto wafe- Yeye hutuwazia mema wakatiwote.

SASA NI KWA NINI AMERUHUSU? Binafsi sijui, Ila ni kwa mapenzi yake mwenyewe na kama mbingu na ardhi vilivyo mbali, ndivyo mawazo ya Mungu na wanadamu yalivo.

Tuendelee kumshukuru Mungu mapenzi yeke yatimizwe.
 
Inalilah waina ilayhi rajiuun.. Pole saana. Bt upendo uliyobakia wakumuonyesha ni dua tu kwa wingi
 
Sijui nikugongee "like" kwa hii habari!! Hapana.

Pole sana mwana jamvi
 
Asante sana na nimekwishapoa tupo hapa Mwimbili Hospital tunasubiri taratibu na ibada za kuaga mwili ndipo tuanze hiyo ratiba ya ibada yani we acha ndugu yangu yakikutokea huwezi hata kusimama, namshukuru Mungu japo kwa kiasi fulani amenitia nguvu za kuweza kuandika hapa, ila itafika kipindi sitaonekana hapa kwani ndo hivyo tena
pole sana
 
asante nipo hapa njiani naelekea mwimbili ndiko tunakoaga na kusafirisha mwili wa marehemu jamani so sad
Pole mpendwa wetu,Mungu akupe ujasiri katika wakati huu mgumu.
 
Basi pole si ndio unachiokitafuta! wewe hauna ndugu na jamaa wa kuwajulisha kwa kuwapigia simu mpaka uje kuanika mambo yako binafsi humu?

Watu ambao hamjawahi kufiwa huwa hamjifichagi. Zamu yako ikifika usisahau kututaarifu tuje kuhani.
 
asante acha sasa nitoke kwani nimeshindwa kuvumilia humu ndani na nimeshindwa kuandika nashukuru kwa faraja zenu tuombeeni jioni tunasafiri
Mungu ni mwema Siku zote.Awatie Faraja yake kipindi hiki Kigumu wewe na ndg.wote wa Marehe.Ailaze mahali panapostahili Roho ya Mareh.Pole Sana Ndg.yangu.
 
Watu ambao hamjawahi kufiwa huwa hamjifichagi. Zamu yako ikifika usisahau kututaarifu tuje kuhani.
Siwezi kukutaarifu kwa maana sikujui wala hunijui hivyo msiba wangu haukuhusu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom