Tanzia: Nimepatwa na msiba wapendwa

Tanzia: Nimepatwa na msiba wapendwa

habari wana jamvi wenzangu

Nina masikitiko na simanzi kubwa ndani yangu kwani nimeondokewa na kipenzi changu mwanangu wa ukoo.

Kwa taarifa hii ya jana iliyonishtua na kunipa simanzi zisizopimika nimeondokewa na kipenzi changu ambaye
ni cousin wangu na kwa upande wa mama yangu mzazi ananiita mama wa ukoo yaani mwanangu, alikuwa anasumbuliwa na tatizo la appendex ambayo ilipasukia tumboni na vilevile alikuwa mjamzito na presha ilishuka chini, jana majira ya jioni alipopelekwa chumba cha upasuaji wakati wanamfanyia matibabu ndipo akakata roho ameacha mume na watoto wawili, na leo tunafanya taratibu za kuusafirisha mwili kwenda mkoani kuzika. sina faraja ingine namshukuru Mungu kwani ndiye aliyetoa na ametwaa jina lake lihimidiwe, mwenzenu niko so sad. Tutasafiri jioni sana na tutaaga pale Mwimbili kuanzia majira ya saa nane mpaka saa kumi hivi ila tunasikiliza kamati ya mazishi itakaposema.
karibuni wapendwa.

Pole sana mkongwe wa JF
 
Touching..so sorry Mungu awape Nguvu..mkoani ni wapi ili watu washiriki nawe
 
Asante nimekwishapoa ila nina simanzi kwani amewaacha watoto wakiwa wadogo sana yani kwanza yuko darasa la 3 yaaini so sad nipo najiandaa kwenda mwimbili hospital pale ndipo tunaaga na kusafirisha mwili
pole sana lady.bwana alitoa na bwana alitwaa jina lake lihimidiwe
 
so sad, inasikitisha, inahuzunisha, pole sana wewe, wanae, mumewe na ndugu jamaa na marafiki wote. Mungu kupitia Roho Mtakatifu ndiye mfariji pekee ashindaye faraja na pole za kibinadamu. RIP Marehemu
 
Asante sana namshukuru mungu ndiye aliyetoa naye ametwaa ila ni uzembe wa madaktari pale mwimbilia asingeondoka ndugu yangu tunamwachia mungu ajuaye
pole sana mkuu
 
Asante kwa faraja nzuri hii twamshukuru Mungu wkwa yote nipo najiandaa mpendwa kuelekea Mwimbili Hospital tuombee tunaposafirisha huu mwili tutaondoka jioni sana
so sad, inasikitisha, inahuzunisha, pole sana wewe, wanae, mumewe na ndugu jamaa na marafiki wote. Mungu kupitia Roho Mtakatifu ndiye mfariji pekee ashindaye faraja na pole za kibinadamu. RIP Marehemu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom