TANZIA: Mtambuzi Apata Msiba

TANZIA: Mtambuzi Apata Msiba

Poleni sana Wapendwa. Mama kamaliza safari yake. Mungu awatangulie katika yote!
 
Mkuu Mtambuzi pole sana kwa msiba
Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahali pema apumzike kwa amani
 
Last edited by a moderator:
Yani mm ndo kwanza naona hapa, heee! jamani pole sana Mtambuzi kwa msiba uliokupata Mungu akupe nguvu kwa kipindi hichi kigumu kwako wewe na familia nzima Mungu awape faraja kwa misiba huu wa kuondokewa na mama mkwe mzaa chema
 
Last edited by a moderator:
“…heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa, naam asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao, kwa kuwa matendo yao yafuatana nao”, (Ufunuo 14:13). Amin!
 
pole sana Mtambuzi!
rest in peace mama mzaa chema!
pole sana mama ngina kwa kufiwa na mama!
 
Last edited by a moderator:
Pole sana kaka, Mungu pekee ndiye mwenye faraja ya kweli. Tupo pamoja katika majonzi mazito.
 
Bwana ilitoa na Bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe. pole sana mzee mtambuzi😛ray2:
 
Pole Mtambuzi

RIP Mama!!

Ndugu wanaJF Salam,

Taarifa zilizonifikia hivi punde ni kwamba mwanaJF mwenzetu ndugu Mtambuzi amefiwa na mama mkwe muda mfupi uliopita.

Mama mkwe wa Mtambuzi amefikwa na mauti akiwa amelazwa katika hospitali ya St. Thomas iliyoko jijini Arusha.

Tutaendelea kufahamishana juu ya taratibu za mazishi. Kwa members wa JF mlioko Arusha support yenu katika kipindi hiki ni muhimu sana.

Natoa pole kwa Mzee Mtambuzi pamoja na familia, ndugu jamaa na marafiki wote waliofikwa na msiba huu. Mungu awaongoze na kuwafariji katika kipindi hiki kigumu na cha majonzi.

UPDATES:
Mipango ya mazishi inafanyika Field Force (FFU) Arusha na maziko yanatarajiwa kufanyika upareni, Mamba Miamba siku ya Ijumaa tarehe 03/05/2013.

MORE UPDATES:
Kwa wale ambao wangependa kuuungana na familia ya mzee Mtambuzi katika msiba huu kwa njia ya rambirambi, tafadhali tumieni namba zifuatazo; Tigo-Pesa 0715 729292 na M-Pesa 0752 729292
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom