Emmanuel Nchimbi, Dawa ya kumaliza msiba ni kuzika

Emmanuel Nchimbi, Dawa ya kumaliza msiba ni kuzika

Heci

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Posts
3,820
Reaction score
6,793
Na Mwl. John Pambalu

Si nikaombea maiti afufuke, na hakufufuka. Nililia sana kwa uchungu nikimlilia rafiki yangu niliyesoma naye BAED katika Chuo Kikuu cha SAUT, nikijiuliza kwa nini Mungu amenikatisha tamaa. Kumbe Mungu ni yule yule, tatizo halikuwa kwake, tatizo lilikuwa ni uhaba wangu wa imani.

Nilipofika mwaka wa pili Chuo Kikuu cha SAUT, tulipatwa na msiba wa mwanafunzi mwenzetu na mshiriki wa group discussion letu la UMOJA, mimi nikiwa mwenyekiti wake. Aliitwa Ben. Nilimpenda sana Ben, alikuwa rafiki yangu wa karibu mno. Chuo kikateua wawakilishi wa kushiriki mazishi. Upande wa wanafunzi tuliteuliwa mimi na dada mmoja aitwaye Heriet, tuliokwenda kuzika huko Bahi, mkoani Dodoma.

Upande wa chuo aliteuliwa mwalimu wetu wa saikolojia, Padre Maziku. Upande wa wanafunzi tulichanga fedha na kupata magari mawili aina ya Coaster. Safari ilianza jioni, saa kumi, tukitokea Bugando kuelekea Bahi.

Baada ya kutoka Bugando, safari ilianza nikiwa nimejaa imani nikaanza maombi ya kumfufua Ben. Nilisali kwa bidii kuanzia Mwanza mpaka Bahi, lakini Ben hakuamka. Nikarejea simulizi za Biblia namna Petro alivyomfufua Tabitha, na namna Eliya alivyomfufua mtoto wa mama mjane wa Sarepta lakini bado Ben hakuamka. Oh my God! Bila shaka niliomba, lakini sikuwa na imani ya kutosha. Mungu bado ni yule yule.

Ilipofika saa tatu usiku, tulianza zoezi la kuaga mwili wa Ben nyumbani kwao, Dodoma. Zoezi la kuaga lilikuwa gumu sana, watu wengi walianguka na kuzimia. Wengine walilia kwa uchungu mkubwa. Maombolezo yalitanda kila mahali, vilio, maumivu na ukunga wa uchungu wa kutisha.

Hatimaye tukampumzisha Ben. Baada ya kutoka makaburini nyuma ya nyumba yao, tukaja mbele. Nikagundua jambo la ajabu, waliokuwa wamezimia walizinduka, waliokuwa wameshindwa kula walianza kula, na sisi tuliotoka mbali tulianza kupiga picha za kumbukumbu.

Hapo nikagundua siri kubwa sana siri kubwa ya kifo na uchungu wake. Nikagundua kuwa kumbe dawa ya kumaliza msiba ni kuzika.

Sasa, jana nimemsikia ndugu Emmanuel Nchimbi akisema tusizungumzie mauaji ya kutisha ya Oktoba 29, 2026. Kwa kifupi, ndugu Nchimbi anapendekeza tuanue matanga bila kuzika. Kwa maoni yangu, hilo ni jambo gumu sana na haliwezekani.

Juzi, mtu mmoja alimtumia ujumbe ndugu Twaha Mwaipaya akimshukuru sana, akimueleza kuwa kupitia video za miili alizozipost, hatimaye ameutambua mwili wa ndugu yake aliyekuwa ametoweka tangu Oktoba 29, 2026. Familia ilikuwa haijui alipo wala kilichompata. Sasa, je, ni ndugu wangapi bado hawajui kama wapendwa wao waliuawa au wanashikiliwa kwenye vituo vya polisi au maeneo ya siri ya mateso?

Mtu wa namna hii kumwambia asizungumzie matukio ya Oktoba 29, 2026 hata kama atakusikia ninaamini hatakuelewa.

Mnataka tuzike mjadala wa mauaji ya Oktoba 29, 2026, lakini hamko tayari kuzika athari zake zinazosababishwa na ugumu wa mioyo ya watawala?. Mpaka sasa, mamia ya vijana na watu wazima wanashikiliwa katika magereza mbalimbali nchini kwa tuhuma za uongo za uvamizi wa kutumia silaha, baada ya kuona aibu na kufuta kesi ya uhaini na kuwapa kesi mbadala ya uvamizi wa kutumia silaha.

Mpaka sasa, ndugu Yohana Kaunya, Katibu Mkuu mstaafu wa BAVICHA Taifa, yuko gerezani Bunda. Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Kigoma, mzee Bujoro, yuko gerezani Kigoma. Ndugu Nchimbi na wenzake hawataki kuwaachilia, halafu wanataka mjadala ufe natural death. Hili haliwezekani.

Ndugu Nchimbi, yapo mambo ya kuyazika kabla ya kuzika mjadala wenyewe.

1. Semeni wazi watu waliouawa ni wangapi. Waliotambuliwa watangazwe kwa majina yao ili ndugu waache kutazama video za mauaji kwa matumaini ya kuwatambua wapendwa wao.

2. Watu wapewe miili ya ndugu zao wakazike wapendwa wao kwa heshima. Israel na Palestina wamepigana vita kwa zaidi ya miaka miwili. Katika jitihada za kuzika mjadala wa vita, wamebadilishana miili ili kila upande uzike wapendwa wake. Kama miili ya watu waliokufa zaidi ya miaka miwili inaweza kurejeshwa, sembuse miili ya miezi minne?

3. Serikali itoke hadharani itamke hatua zilizochukuliwa kuwawajibisha wauaji. Najua hili ni gumu sana, hasa ukizingatia hotuba ya ndugu Samia aliyotoa Dar es Salaam aliposema nguvu iliyotumika ilikuwa inafaa. So sad 😔

4. Serikali itoke, ikiri, ilie na kuomba radhi, kisha mjadala wa Katiba Mpya uanze kwa nia ya dhati ya kuzuia unyama kama huu usijirudie tena.

Ninaamini haya yakifanyika hayataumaliza mjadala kabisa, lakini angalau yataupooza na kuupa mwelekeo wa uponyaji wa kitaifa.

Ninapomaliza makala hii, kumbukeni nilivyoomba mfu afufuke na hakufufuka. Nataka kusema nini?. Tanzania haitabaki kuwa ile ile baada ya mauaji ya Oktoba 29, 2025. Tumelitia doa taifa letu, doa ambalo ni lazima tujifunze kuishi nalo kwa kuamua kwa dhati kubadilika, ili dunia ijue kuwa ni kweli yalitokea, lakini pia waone kuwa tulijifunza na kubadilika.

Na mabadiliko huanza kwa kuachana kabisa na ubatili wote uliotufikisha hapa, kuacha utekaji, kuwaachilia wafungwa wa kisiasa na kutokukamata wengine, na kuwahakikishia usalama wale waliokimbia nchi ili warejee kushiriki kulijenga taifa letu moja.

Ninawakumbusha kuwa tarehe 09.02.2026 mwana mpendwa wa Tanzania anayechukiwa na watawala kwa sababu ya misimamo yake ya kupigania HAKI Tundu Lissu ataletwa Mahakamani. Tujitahidi kufika ili kumtia moyo ajue tuko naye.

Share Zaidi makala hii

Wasalamu,
Mwl. John Pambalu
Mwalimu wa Zamu (T.O.D)
 
kina pambalu mbona wao hawajakiri vijana wao wa chadema kuhamasisha hiyo mo29? --- hawaoni kwamba na wao ni wahusika ?
 
Duh! Yaani mkuu uhai wa wengine si kitu kwako kabisa.

Vv
porojo na uzushi ni mambo nonsense na useless kabisa gentleman,

hata hivyo,
kwangu mimi kuishi ni Kristo na kufa ni faida zaidi, kinyume na hapo ni ushirikina mtupu :NoGodNo:
 
kina pambalu mbona wao hawajakiri vijana wao wa chadema kuhamasisha hiyo mo29? --- hawaoni kwamba na wao ni wahusika ?
Wakiri kukataa chaguzi za kihuni ama kuua watu?
 
porojo na uzushi ni mambo nonsense na useless kabisa gentleman,

hata hivyo,
kwangu mimi kuishi ni Kristo na kufa ni faida zaidi, kinyume na hapo ni ushirikina mtupu :NoGodNo:
Kwahyo kristo amekuambia uuwe watu?embu niambie umeteka umebaka na kuua wangapi kwa name of serikali tukufu ya ccm.
 
Wakiri kukataa chaguzi za kihuni ama kuua watu?
kuingiza watu mkenge mkuu, au na wewe ni miongoni walioamini watu wakitoka ccm ingefungasha virago na kukaa pembeni?

yani mtu unajua fika damu zitamwagika alafu unazidi kuhamasisha watu , alafu mwisho wa siku wewe unaingia mitini na kusubiri kuanza kutoa pole na kuona huruma
 
Yaani ukatae chaguzi za maigizo kisha utarajie watu kufa. Kwahiyo ilitakiwa watu watulie ili uchaguzi uendelee kunajisiwa ili usife? Kwahiyo ccm imekuwa ikipora uchaguzi maana ukikataa kuporwa watakuua? Sijaelewa unaongea nini dogo.
 
cdm haikuunga mkono maandamano? siku ya uchaguzi?
 
cdm haikuunga mkono maandamano? siku ya uchaguzi?
Msimamo wa cdm uko wazi NRNE. Cdm walikuwa sahihi sana kugomea uchaguzi wa kihuni, na matokeo ya kura 31m za uongo yamedhibitisha cdm walikuwa sahihi kugomea uchaguzi wa kihuni. Mauaji yalifanywa na serekali.
 
Kwahyo kristo amekuambia uuwe watu?embu niambie umeteka umebaka na kuua wangapi kwa name of serikali tukufu ya ccm.
nonsense,

Gentleman,
kila mwanadamu aliezaliwa na mwananamke siku zake za kuishi si nyingi.
kufa kilofa kwa kubebwa ufala wa kifikra na vibaraka wa mabwenyenye ya magharibi ni dhambi:NoGodNo:
 
kina pambalu mbona wao hawajakiri vijana wao wa chadema kuhamasisha hiyo mo29? --- hawaoni kwamba na wao ni wahusika ?
Hivi maandamano ya October 29 yalikua ya CHADEMA?

Huna habari CHADEMA imefungiwa kufanya shughuli yoyote ya kisiasa hata kusanyiko la watu 10 haliruhusiwi toka June 10 mwaka 2025.

Maandamano yale hakukua na bendera ya CHADEMA, ACT , CUF , TLP wala chama chochote zilikuwepo bendera za Tanzania na hata maiti nyingi zilifunikwa kwa bendera kizalendo.

Ukweli usemwe ufisadi, wizi, kazi za vimemo, chaguzi feki ,ukosefu wa ajira, dharau za watawala ndio ziliwaingiza watu barabarani.

Na msipojifunza watarudi tena barabarani siku za usoni.
downloadfile-430.jpg
downloadfile-75.png
 
Hivi maandamano ya October 29 yalikua ya CHADEMA?

Huna habari CHADEMA imefungiwa kufanya shughuli yoyote ya kisiasa hata kusanyiko la watu 10 haliruhusiwi toka June 10 mwaka 2025.

Maandamano yale hakukua na bendera ya CHADEMA, ACT , CUF , TLP wala chama chochote zilikuwepo bendera za Tanzania na hata maiti nyingi zilifunikwa kwa bendera kizalendo.

Ukweli usemwe ufisadi, wizi, kazi za vimemo, chaguzi feki ,ukosefu wa ajira, dharau za watawala ndio ziliwaingiza watu barabarani.

Na msipojifunza watarudi tena barabarani siku za usoni.View attachment 3539056View attachment 3539057

chadema kupitia vijan wao kina mwaipaya hilda newton na wengineo hawakua na subira iliwabidi washiriki kuhamasisha ili baadae kwenye kuchukua credit chadema isikosekane, tarehe 28 mchana bavicha kupitia akaunti yao ya twitter waliyaunga mkono.

nani anaweza kurudi road nyakati hizi mkuu? wewe road utaingia? uliingia?
 
Back
Top Bottom