Tanzania yaongoza Afrika Mashirika kwa kasi kubwa kuhamia kwenye magari ya umeme

kalacha mateo

Senior Member
Sep 27, 2021
118
237
Kwa mujibu wa ripoti ya E-Mobility Alliance, ambayo ilitolewa mwezi uliopita, inaonyesha kuwa kuna angalau magari 5,000 ya umeme (EVs) nchini Tanzania

Ingawa uagizaji na utumiaji wa magari ya umeme yana changamoto nyingi kwa nchi Tanzania serikali imeanza kuweka nguvu kutanua wigo wa watumiaji magari ya umeme nchini.

Katibu Mkuu wa Nishati Felchesmi Mramba anasema serikali inafanya kila iwezalo kuweka mazingira wezeshi ya biashara ili kukuza uwekezaji katika e-mobility ikiwemo kuwepo kwa umeme wa kutosha unaopatikana kwa EVs.

"Tuko tayari kushirikiana na sekta ya kibinafsi ili kuhakikisha kuna vituo vya kutosha vya kutoza magari yanayotumia umeme," Bw Mramba alisema

Serikali ina azma mpya ya kukuza nishati bora na safi ndio maana imeamua kushirikiana na sekta binafsi kuchochea matumizi ya umeme na gesi kwenye magari.

magari-ya-umeme-kuchaji.jpg
 
Back
Top Bottom