Kamati ya Bunge PAC: Kuna Uwepo wa Magari ya Serikali 547 ambayo Hayatumiki kwa Muda Mrefu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,280
Ukaguzi wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) umebaini jumla ya Magari ya Serikali 547 yalikuwa yameegeshwa kwenye Karakana za Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na katika baadhi ya Taasisi za Serikali

Aidha, baadhi ya magari yaliyotelekezwa hayakuwa kwenye mipango ya matengenezo au ya uondoshwaji. Ukaguzi ulibaini kuwa asilimia (43%) ya magari yalikuwa yameegeshwa kwenye Karakana za TEMESA kwa zaidi ya miaka mitatu (3) kutokana na sababu mbalimbali kama vile ajali, matengenezo, maegesho, na kusubiri vibali vya uondoshaji.

Uwepo wa magari mengi ya serikali yaliyoegeshwa kwa muda mrefu bila kutumika ulitokana na baadhi ya Taasisi kutofanya uhakiki wa hali za mali zake ili kufahamu kama ziondolewe au zitengenezwe. Kuwepo kwa magari mabovu ya Serikali ambayo yameegeshwa na hayatumiki kwa muda mrefu bila kuondoshwa kulikuwa na athari zifuatazo:-

a) Magari kuchakaa na kuharibika zaidi na kwa kasi hali inayopelekea kupungua kwa thamani ya magari haya pale ambapo Serikali itaamua kuyaondoa;

b) Madhumuni ya ununuzi wa magari hayafikiwi ipasavyo kwa sababu magari hayafanyi kazi kulingana na madhumuni yaliyokusudiwa;

c) Kuongezeka kwa gharama za matengenezo kutokana na uchakavu wa magari mabovu ambayo yamehifadhiwa na hayatumiki kwa muda mrefu; na

d) Upotevu wa rasilimali-fedha za umma.
 
Mambo kama haya yanauma sana kama sio kuudhi.


My Take
Chadema hizi ndio hoja za kupigia kelele, hakuna mtu anataka kuona jasho lake linachezewa na maofisa wa Serikali kizembe hivi.

Harafu wanasema lazima wanunue ndege za Viongozi over social services.Hii haikubakiki.

On top of that Kila mwaka wanaagiza magari mapya ya serikali wakati Kuna magari hayo yangeweza kutengenezwa na yanaendelea kitumiwa.

Naunga mkono hoja ya Estee Bulaya na Kamati.
 
Afu kuna miwatu inasema mizungu haitaki tuendelee. Mizungu have nothing to do with this BS. Akili za miviongozi ni kufuja pesa tu, maendeleo ni jambo la mwisho kabisa kwao. Hapo wanasubiri wahisani watoe msaada wa vyoo na madawati ila magari kununua kila mwaka wanaweza.
 
Huu ndio ungese wa hii inayoitwa serikali ya ccm maamae zao hawa mbwa
 
Kwanini wasiziorodheshe hizo Halmashauri kwenye vyombo vya habari na kuwawajibisha wakurugenzi wa maeneo huzika
 
Back
Top Bottom