Benki ya Dunia yaipongeza Tanzania kwa jitihada za kuimarisha upatikanaji wa umeme

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,828
21,457
82299665-33F8-467A-BECF-CE997CAE91CD.jpeg
Benki ya Dunia (WB) imeipongeza Tanzania kwa kuchaguliwa na kuwa miongoni mwa nchi nne barani Afrika zilizoingizwa katika mradi wa Benki ya Dunia wa ‘ASCENT’ ambao unalenga kuimarisha upatikanaji wa umeme kwa wananchi.

Amesema hayo Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Benki ya Dunia, Wendy Hughe wakati wa mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko ambaye amesema suala la upatikanaji wa umeme nchini lina umuhimu kiuchumi, kisiasa na kijamii, hivyo Serikali inapata msukumo mkubwa wa kuhakikisha nchi inakuwa na umeme wa uhakika.

Pamoja na kuishukuru benki hiyo kwa kutoa fedha za kuendeleza miradi mbalimbali ya nishati ukiwemo mradi wa umeme wa Rusumo (MW 80) ambao dola za Marekani milioni 340 [TZS bilioni 851] zimetolewa, na mradi wa kuunganisha umeme kati ya Tanzania na Zambia uliotolewa TZS trilioni 1.13, Dkt. Biteko amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa benki hiyo kutokana na faida zinazotokana na ushirikiano uliopo.

Ameongeza kuwa, fedha zinazotolewa na wadau wa maendeleo ikiwemo Benki ya Dunia zitasimamiwa ipasavyo ili zitumike kwa malengo kusudiwa na hivyo kusukuma mbele sekta ya nishati ili kuwawezesha wananchi wote kuutumia umeme kwa shughuli za kijamii na kiuchumi.
 
Mungu yupo Na Rais samia na serikali yake na Anaendelea kumpatia njia na maarifa ya kuliongoza Taifa letu.Ndio maana kila anapogusa panafanikiwa na kila mipango inafanikiwa na Taifa letu linaendelea kuwa lenye neema na baraka kwa kila jambo.
 
Attachments

  • 0BAE5857-C40C-4017-AE12-FF414B440A03.jpeg
    0BAE5857-C40C-4017-AE12-FF414B440A03.jpeg
    56.6 KB · Views: 4
Mama chapa kazi tu, majungu waachie mabingwa wa majungu.
2025 & 2030 hakuna mwingine ni wewe tu Mungu akipenda. Watanzania wanataka umalize kazi ya miundo mbinu mama ili nchi ipae kiuchumi
 
Mkuu ebu soma ulichoandika ? Kwanini ujinga wote unatokaga ccm ? Ulichosema hapa kinahusiana nini na kinachoongewa ? Ni majungu kwamba umeme hautosh saivi ? Ni majungu kusema ukweli ?
 
Benki ya Dunia (WB) imeipongeza Tanzania kwa kuchaguliwa na kuwa miongoni mwa nchi nne barani Afrika zilizoingizwa katika mradi wa Benki ya Dunia wa ‘ASCENT’ ambao unalenga kuimarisha upatikanaji wa umeme kwa wananchi.

Amesema hayo Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Benki ya Dunia, Wendy Hughe wakati wa mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko ambaye amesema suala la upatikanaji wa umeme nchini lina umuhimu kiuchumi, kisiasa na kijamii, hivyo Serikali inapata msukumo mkubwa wa kuhakikisha nchi inakuwa na umeme wa uhakika.

Pamoja na kuishukuru benki hiyo kwa kutoa fedha za kuendeleza miradi mbalimbali ya nishati ukiwemo mradi wa umeme wa Rusumo (MW 80) ambao dola za Marekani milioni 340 [TZS bilioni 851] zimetolewa, na mradi wa kuunganisha umeme kati ya Tanzania na Zambia uliotolewa TZS trilioni 1.13, Dkt. Biteko amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa benki hiyo kutokana na faida zinazotokana na ushirikiano uliopo.

Ameongeza kuwa, fedha zinazotolewa na wadau wa maendeleo ikiwemo Benki ya Dunia zitasimamiwa ipasavyo ili zitumike kwa malengo kusudiwa na hivyo kusukuma mbele sekta ya nishati ili kuwawezesha wananchi wote kuutumia umeme kwa shughuli za kijamii na kiuchumi.
Umeme juzi usiku ulikatika jana siku nzima haupo..
Ngoja ninyamaze mie 🤐🤐🤐
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom