hako kajizee kamezoea propaganda tuu na sijui bado kanafanya nini naona kanataka kufia ofisini...kaache waliotajwa wajitetee wenyewe kama wanaona kuna cha kujitetea,yaani kamenichafua ile mbaya
Ngoja niwaambie kitu. Baada ya Ofisi ya Waziri Mkuu kukurupuka kujibu hoja ya "kupaa" na baada ya Maelezo kukurupuka na kujibu suala la "kuitwa wasanii" CCM wameamua kutumia njia nyingine kabisa nayo ni kupuuza. Kwa siku za karibuni angalieni na mtaona kuwa hawajibu hoja tena isipokuwa kutoa kauli za "kupuuzia". Hili la kina Dr. Slaa ni mwanzo tu.
Chochote ambacho kitasemwa na wananchi watawala wetu watajibu kwa kejeli na kudharau, hawataenda mahakamani kudai defemation, hawataandika makala kujibu tena, watawatumia kina Kingunge, Makamba na wapambe wao kutoa kauli za kejeli na kupuuzia.. mtasikia kauli kama "hao ni wapinzani hawana jingine la kufanya", "wana haki ya kutoa maoni yao na huo ndio uzuri wa demokrasia" Kitu pekee ambacho hawatafanya ni kujibu hoja kwa hoja.
Now, sisi wakosoaji tunabadili mwelekeo pia, mwelekeo ambao utawalazimisha wajibu hoja.
Jambo moja watakuwa wanasahau ni kuwa ushindi wote unaopatikana kwa CCM siku zote umekuwa hausababishwi na sera au Ilani, ila unasababishwa na kutokuwapo kwa upinzani ambao ni alternative nzuri. Kwa hiyo wakiruhusu upinzani kuwaonyesha wananchi kuwa wanaweza kufanya vizuri zaidi ya CCM kwa kutoa nje makosa ya CCM ambayo yasingefanywa na wapinzani, basi watakuwa wameruhusu upinzani kupiga hatua kubwa sana dhidi ya CCM minus mizengwe ya uchaguzi.
Kumbuka kuwa hili la wizi wa madini linaingia sana akilini mwa wananchi kuliko sera za kujenga sekondari zisizokuwa na waalimu.
Kingunge is a used politician. He was once useful, at least to Mwalimu, as a staunch party ideologue. We discarded the party ideology but forgot to discard this ideologue as well. We are paying the price of that.
Huku "kupuuza" kunakofanywa na CCM kunatokana na "kuhaha". Hawajui wajibuje hasa. Marmo amejaribu kusema ilibidi wapinzani wapeleke taarifa Polisi. Nani kamwambia Polisi hawana taarifa? Kuna kupeleka taarifa Polisi kunakozidi Waziri wa Mapolisi (Lyatonga) kwenda na Mkuu wa Polisi (Mahundi) na kumwonyesha wakosaji wenyewe Uwanja wa Ndege, na Polisi kuwakuta wakosaji wenyewe wameshika kosa mkononi?
Naona CCM inapata kigugumizi kutokana na kufunuliwa hujuma zinazofanywa na viongozi wake wakuu. Wajue hizo ni rasha rasha tu. Mvua zenyewe bado kabisa!
You can cheat some of the people some of the time, but you cannot cheat all the people all the time! Ngojeni magazeti na redio huru, na magazeti na redio za wapinzani zianzishwe na kuimarishwa zaidi halafu mtaona jinsi hujuma zenu zitakavyoanikwa kwa wananchi.
Unajua kuna kitu kimoja ambacho wapinzania wanatakiwa kukua. The battle ground on graft should not only be confined at home, they should go abroad Brussels, London or Washington. By doing so inaweza kuongeza nguvu. Ni kweli watanzania walio wengi wakisikia Kingunge akisema aaaaaahhhhhhhhhh ni uzushi tu, au wakisikia Makamba anasema aahhh wanakichafua chama wanaweza kuamini. Pamoja na kuwa Slaa amesema aliyosema unaweza kushangaa kuwa Slaa anachafuliwa na kuonekana hana maana tena. Nadhani approach ya Seifu ilikuwa nzuri sana, ilifanya crisis ya Zanzibar ijulikane world over na serikali ikalazimika kuanza na talks. Lakini Kama slaa akiishia hapo tu nadhani haitatusaidia sana, lakini it is a good thing that he put things in public, japokuwa kwa watanzania wachache wanaojua it is same old story, may be sasa hatua zitaweza kuchukuliwa.
Lakini kutokana na kuwa sasa hivi serikali imefungwa mikono sidhani kama inaweza kufanya kitu, i do not see JK taking actions against Mramba, Balali, Karamagi, Chenge au Mkono. Sana sana atakachofanya ni kuwaondoa uwaziri lakini hakuna la zaidi atakalofanya. Can he put them behind bars? nadhani aliykuwa anaongea na Condi ni kuwageresha donors tu, and Tanzania has been doing best on that.