Tanzania tunanunulia wapi/nchi gani Internet?

Tanzania tunanunulia wapi/nchi gani Internet?

Mkuu mm naomba ufafanuzi
Kwa mfano,youtube,facebook,yahoo,au mtandao wowote wenye saver ni lazima wawe na fibre cable yao kuzunguka duniani kote?au wao wanaingizaje mitandao yao kwenye hizo cable?

Hapana wao wana link through neno www. So kama utakua na network bas unatumia link hiyo basi
 
apo nimekuelewa hizi speed unaweza kuzipata wirelessly so haina haja ya kuchimba mitaro ... Hiv hizi prvate leased lines walizoweka halotel kwenye packages zao sio fibre.. au ndo zile radio links tunazozionaga banks na tass nyingine???

Yes ndo wanaita point to point antenna ndo njia ya wireless mkuu
 
Kwa raha mimi nilitaka kwaajili ya biashara 50mbps plus kodi wanauza kwa dola ilikua wanataka point to point kwa 1300 dollars

Mkuu kama kuna kampuni inauza 50mbps chini ya hapo naomba details nao nahitaji huduma raha nimejaza form kabs ila nataka kampuni watakao kua cheap zaid iwe dedicated na sio shared networking plus najua share ni cheap ila sio nzuri
mkuu location ni muhimu, zuku kama upo covered installation ni bure unaanza tu kulipia hela yao ya mwezi, 40mbps 130,000 na 100mbps ni 250,000.
 
Na vipi simu zetu hizi za saut nazoo zinatumia muunganiko wa waya baada ya signal kuwaa zimefika kwenye mnara tayari kwenda eneo husika ambalo mpiga simu anataka mawasiliano yake yaende

Kwa mawasiliano ya simu zaman ttcl ndo walikua wanatumia waya kuwasiliana na mtu ila mobile phone mawasiliano yana pita kwa njia ya wireless kwenye minara kuna zile nyungo ni radio wave zina link mnara hadi mnara kupena muunganiko toka makao makuu pia kuna zile ndefu signal antenna kwaajili ya uunganisha na simu zetu zina kuwa nyingi sababu ya band za vifaa vyetu ni tofauti mfani kuna 2.4 band hizi ni frequency signal zake zinaenda umbali mfupi lkn inakua strong na kwenye vifaa vingi vya kizamani ndo inakua hii sana pia 5 ghz band hii signal zinaenda mbali lkn zinakuwa weak pia antenna inaenda kwa degrees kubwa sana nazozijua mimi 120 na ukaa tatu ili kukamilisha 360 digirii nyuzi ili kuzunguka eneo lote au nyingi ni ndogo 90 digirii ufungwa nne na kulingana na eneo ili kupata line of site ndo mana kuna baadhi ya maeneo hasa kimara kwenye milima na mabonde net inakuwa shida sana
 
mkuu location ni muhimu, zuku kama upo covered installation ni bure unaanza tu kulipia hela yao ya mwezi, 40mbps 130,000 na 100mbps ni 250,000.

Ok na hiyo inakuwa dedicated au shared network mkuu
 
Daah kumbee...!! So nkikaa karibu na hiki kidude speed ya net inakuwa kubwa sanaa etii??.
Hamna mzee huo ni waya tu kama waya wa Umeme hauna faida yyte kwenye cm yako huwezi kukaa chini ya nguzo ya Tanesco eti uchaji cm hapana..... Ukitaka mtandao kaa karibu na Mnara wa mtandao wako utaenjoy
 
Yes ndo wanaita point to point antenna ndo njia ya wireless mkuu
point to point naikubali sana nimeona wanafunga huku kwenye dispensaries... ila kwa personal use ni hasara sema show kufungiwa microwave link juu ya house aisee
 
IMG_7154.jpg

IMG_7155.png

IMG_7156.png

Soma
 
mkuu kusema kweli huku mijini wameitandaza sana internet na speed si haba, sasa hivi ukienda Kariakoo maduka mengi yana fiber, hata mitandao yetu kama Halotel na Voda speed zao za 4g ni zaidi ya average speed ya dunia.

tatizo ni kwamba ipo katikati ya majiji tu ukitoka nje kidogo tu hakuna fiber na hata hizo 4g zinaanza kupotea, hivyo wanaofaidika wanakuwa ni wachache.
ni kweli chief Halotel 4g yao wanaenda mpaka mbps 16
 
hakuna eneo maalumu maana kazi yake ni kuzungusha tu hizo data kwenda maeneo mbalimbali, mfano

- unaangalia youtube, umesearch video ya kiba, ile request yako itapelekwa na waya hadi server za youtube marekani, kisha kule marekani itachukuliwa ile video na huo waya na kuletwa hadi Tanzania.

-unachat na rafiki yako china kwa snapchat, inamaana waya utapeleka msg yako kwenye server za snapchat marekani, kisha waya mwengine utachukua na kumpelekea msg yule rafiki yako wa china

hivyo kazi za hizo waya ni kusafirisha tu taarifa baina ya watumiaji na servers mbalimbali duniani, internet inazunguka dunia nzima hakuna aneimiliki ni kama vile barabara, Tanzania tuna miundo mbinu yetu, Kenya wana yao, Usa wana yao, China wana yao etc then kuna makampuni ya kimataifa yanaunganisha miundo mbinu ya nchi mbalimbali pamoja
Dah uko vizuri mkuu.
 
Kuna concept ya Intranet mkuu ambayo inakuwa ni internet inayojitegemea, inakuwa haijaunganishwa na Internet ya dunia. Inatumika sana kwenye makampuni makubwa.

Wanachotaka kutengeneza Russia ni Intranet pia sema wao wataweka Gateway ambayo inaconnect na dunia, incase kuna CyberAttack wanadisconect hio Gateway na kutumia vya kwao tu Ndani.

Pia Si concept ngeni maana Tayari zipo Network kama hizo kama vile
-Kwangmyong ya North Korea
-National Information Network (Nin) ya Iran sema haijakamilika
-hlutaw ya Mynamar
-Snet ya Cuba (hii imetengenezwa tu na wananchi wenyewe, wanacheza games)
Sasa hao warusi kama wanatengeneza itranet kwa ajili ya nchi yao tu kwanini waiunganisha na ya dunia?
 
mkuu kusema kweli huku mijini wameitandaza sana internet na speed si haba, sasa hivi ukienda Kariakoo maduka mengi yana fiber, hata mitandao yetu kama Halotel na Voda speed zao za 4g ni zaidi ya average speed ya dunia.

tatizo ni kwamba ipo katikati ya majiji tu ukitoka nje kidogo tu hakuna fiber na hata hizo 4g zinaanza kupotea, hivyo wanaofaidika wanakuwa ni wachache.
Halotel ukinunua kifurushi kikubwa mfano cha mwezi, vipi hawapunguzi speed?.
 
ni kweli chief Halotel 4g yao wanaenda mpaka mbps 16
16MBps labda, burst speed nimewahi kupata hadi 200mbps (25MBps), na inaweza ku sustani 80mbps mpaka 100mbps (10/12MBps). Hii speed hata Huko Duniani unaipata Nchi chache sana,
 
Sasa hao warusi kama wanatengeneza itranet kwa ajili ya nchi yao tu kwanini waiunganisha na ya dunia?
Sababu Nchi yao Tu haiwezi kujitosheleza, Mfano mrusi akitaka Kuchat na Mtanzania hataweza kwa Intranet ya Ndani ni mpaka atumie Internet ya Dunia.
 
Back
Top Bottom