Tanzania tunanunulia wapi/nchi gani Internet?

Tanzania tunanunulia wapi/nchi gani Internet?

Nimeshapewa jibu la maana la swali nililouliza, hivyo sioni hoja ya kukuletea huo ushahidi maana lengo hapa sio ushahidi ila ni uwezekano wa hicho kilichosemwa.
Kama uko too concerned, nenda Google.
Tupe ushahidi wapi walisema.
 
Ni kama walivyosemaga eti huduma za posta zinaenda kufa nikawaangaliaaa nikasema jambo usilolijua ni kama usiku wa giza. Yaani sasa hivi watu wa posta ndo wanachakarika vibaya mno.
Nawazaga posta kwa nini wasiwe na virtual postal box . Yaani sio lazima uwe na funguo wawe na mfumo unaomwezesha mtu kufungua box na kuweka anuani ya makazi itasaidia mtu kupata mzigo au barua moja kwa moja sio lazima kwenda kufungua box na kuangalia . Pia itaongeza wateja maana itakua rahisi kila anayetaka kutumia huduma zao kufungua account yake na kulipia mwenyewe
 
Mkuu mm naomba ufafanuzi
Kwa mfano,youtube,facebook,yahoo,au mtandao wowote wenye saver ni lazima wawe na fibre cable yao kuzunguka duniani kote?au wao wanaingizaje mitandao yao kwenye hizo cable?
Fiber optic na twisted pair cable ni transition medium tu . Kawa unataka internet isafiri umbali mkubwa na watumiaji ni wengi wanatumia optic fiber kwa sababu ya speed . Pia kama karibu na watumiaji ni wachache na sio karibu karibu unaweza tumia twisted pair cable mara nyingi wanatumia unshilded twisted pair (UTP) . Hao Facebook na wengine kazi yao kuhost hivyo program kwenye server
 
Kwani iyo kampuni bado tu ipo hai ?.mi nilijua ishakufa maana naona kama vile awapo serious na kazi
Kiukweli hao posta wanabebwa tu na serikali ila ni kama imejifia tu.
Maana siku hizi tunatumia email na simu kuwasiliana,kutuma pesa tunatumia Mpesa.
Labda kutuma vifurushi kimataifa na bado kuna DHL ambao ndio wako smart kwa hiyo task.
Kutuma pesa kimataifa kuna Western union inafanya hiyo kazi.
Ishu za kutuma barua siku hizi ni very rare au hakuna
 
Huwa nikienda kupokea mzigo Posta kunakuwa na ka foleni mkuu,

Dhl/Fedex gharama sana unaweza nunua Kitu 5000 ukaambiwa shipping fee laki 1, posta ndio watu wengi wanaponea kwenye shipping za bure.

Sema wanatakiwa waimprove hasa kwenye suala la muda, wanaweza wakaanzisha na wao package zao za muda mfupi za kwa gharama ya kati.
 
Wanaweza tumia njia kama
1. Satelite Internet, sema hii haitumiki sana ni kama backup tu.

2. Cable za Chini ya Bahari ama Nchi kavu, angalia hii picha kwa list ya provider

View attachment 1523682
Ukisikia mkonga wa Taifa ndio hizo cable, zinakuwa na bandwidth za maana, zaidi ya Terabyte kwa sekunde, kuna moja hapo inaenda hadi terabit 100.

Hizo cable ndio Internet Servoce Provider wanatumia kuunganisha na nje ya Bara la Africa.
Kabla ya huo mkongo wa taifa,zamani internet ilikuwa inatufikia kwa njia gani?
Maana huu mkongo ni wa juzi juzi namaanisha miaka ya nyuma ya tisini na kitu huko....huu mkongo si ndio wanatumia fiber cable?
~ ISP wa hapa bongo wananunua internet kwa nani?
 
hakuna eneo maalumu maana kazi yake ni kuzungusha tu hizo data kwenda maeneo mbalimbali, mfano

- unaangalia youtube, umesearch video ya kiba, ile request yako itapelekwa na waya hadi server za youtube marekani, kisha kule marekani itachukuliwa ile video na huo waya na kuletwa hadi Tanzania.

-unachat na rafiki yako china kwa snapchat, inamaana waya utapeleka msg yako kwenye server za snapchat marekani, kisha waya mwengine utachukua na kumpelekea msg yule rafiki yako wa china

hivyo kazi za hizo waya ni kusafirisha tu taarifa baina ya watumiaji na servers mbalimbali duniani, internet inazunguka dunia nzima hakuna aneimiliki ni kama vile barabara, Tanzania tuna miundo mbinu yetu, Kenya wana yao, Usa wana yao, China wana yao etc then kuna makampuni ya kimataifa yanaunganisha miundo mbinu ya nchi mbalimbali pamoja
Hii ni WAN-wide area network inayotumia waya...Mimi nilijua ni wireless?
 
Kabla ya huo mkongo wa taifa,zamani internet ilikuwa inatufikia kwa njia gani?
Maana huu mkongo ni wa juzi juzi namaanisha miaka ya nyuma ya tisini na kitu huko....huu mkongo si ndio wanatumia fiber cable?
~ ISP wa hapa bongo wananunua internet kwa nani?
Mkuu mkonga umekuja Kuongeza Speed na capacity, mfano Kwa TTCL kabla ya Mkonga walikuwa wakitumia Simu ( Adsl) ila siku hizi wana njia za kisasa zaidi sababu Ya mkonga hivyo wameweza kuunganisha Taasisi nyingi.

Na zamani kabisa mkuu hakukuwa na internet kabisa, enzi za mwalimu. Internet imeingia Africa 1995, na huku kwetu internet za mwanzo zilikuwa ni satelite tena tunaziona ziona tu kwenye mashirika kama World vision ukipita nje ya Ofisi zao unakuta Dishi kubwa.

Then zikafuatia Hizo internet za Simu aka Dial up Connection, speed mwendo wa Kobe, zenyewe TTCL wanakuletea simu ya Mezani nyumbani, kupitia hio simu ndio unapata Internet. Zilikuwa zikitumia zile waya zao za shaba za namna hii
images

Halafu baadae zikaja hizo fiber ila hazikuwa zikitosheleza, mpaka leo fiber zinaongezeka moja wapo ikiwa ni huo mkonga.
 
Internet ni Wan mkuu, Japo sio lazima Wan iwe internet, Sijaelewa hapo kwenye Wireless.
Nimeiona hapo wire ndio inaleta internet kutoka ughaibuni mpaka hapa kwetu hii itakuwa Wide area network ambayo huwa ni wireless...sasa hii tutaitaje katika aina za network,maana inaunganisha dunia lakini kwa kutumia wire?
 
Mkuu mkonga umekuja Kuongeza Speed na capacity, mfano Kwa TTCL kabla ya Mkonga walikuwa wakitumia Simu ( Adsl) ila siku hizi wana njia za kisasa zaidi sababu Ya mkonga hivyo wameweza kuunganisha Taasisi nyingi.

Na zamani kabisa mkuu hakukuwa na internet kabisa, enzi za mwalimu. Internet imeingia Africa 1995, na huku kwetu internet za mwanzo zilikuwa ni satelite tena tunaziona ziona tu kwenye mashirika kama World vision ukipita nje ya Ofisi zao unakuta Dishi kubwa.

Then zikafuatia Hizo internet za Simu aka Dial up Connection, speed mwendo wa Kobe, zenyewe TTCL wanakuletea simu ya Mezani nyumbani, kupitia hio simu ndio unapata Internet. Zilikuwa zikitumia zile waya zao za shaba za namna hii
images

Halafu baadae zikaja hizo fiber ila hazikuwa zikitosheleza, mpaka leo fiber zinaongezeka moja wapo ikiwa ni huo mkonga.
Nimekusoma...hizo dial up connection zilikuwepo kwenye simu za mkononi za zamani zile philips na Siemens
 
Nimeiona hapo wire ndio inaleta internet kutoka ughaibuni mpaka hapa kwetu hii itakuwa Wide area network ambayo huwa ni wireless...sasa hii tutaitaje katika aina za network,maana inaunganisha dunia lakini kwa kutumia wire?
wide area network sio lazima iwe wireless mkuu, wire ama wireless ni kipitishio tu cha data.
 
ndio mkuu wireless ni expensive, sababu wireless haina bandwidth kubwa kushinda waya. unaweza ukapitishwa waya mmoja tu mtaani wa 10gbps na mtaa mzima mkawa na internet ya maana.

Hapana wireless ni cheap kwenye kuunganisha point to point services na inauwezo wa kubeba data kubwa tu sema gharama inakuja kwenye operation kwa wired ni gharama ndo mana fiber cable nyingi ziko mjini na bundle kwa town kwa wale wanaopanga kwenye magorofa inatoa huduma ya internet kwa fiber very cheap compared na wireless

Kwa service provider kama simba net ndo anaongoza kuwa na fiber cable town raha ambao sasa wanachukuliwa na telecom wanaongoza kutoa huduma kwa taasisi kubwa na kampuni nyingi zilizo mbali na fiber kwa njia ya wireless lakini mwenye miundombinu mikubwa kwa mikoa yote ni ttcl wana backbone kwa mwenye kutaka kusafirisha umbali mrefu kwenye mikoa na kuitaji fiber services wanakodi kwa ttcl tumewahi jaribu kufanya biashara na raha telecom kwa point to point service ni gharama sana kuliko fiber cable kwa bundle zao za size moja
 
mkuu kusema kweli huku mijini wameitandaza sana internet na speed si haba, sasa hivi ukienda Kariakoo maduka mengi yana fiber, hata mitandao yetu kama Halotel na Voda speed zao za 4g ni zaidi ya average speed ya dunia.

tatizo ni kwamba ipo katikati ya majiji tu ukitoka nje kidogo tu hakuna fiber na hata hizo 4g zinaanza kupotea, hivyo wanaofaidika wanakuwa ni wachache.

Ni kwel unajua huduma za data kwa sasa anakuna tofauti na voice mkuu kampuni zinajiendesha kwa faida alafu antenna za data 4g ni gharama kufunga kwenye minara ya nje ya mji ambao watu wenye vifaa vya kusukuma 4g ni wachache wengi ni wapita njia kwaiyo wanaangalia kwenye idadi kubwa ndo mana mwanzo walifanya promo sana ili watu waamie kwenye 4g hata airtel leo wamenipigia simu nikabadili line yangu kwenda 4g na offer ya 4gb wananipa kwa week nzima ingawa sitaki 4g mana bando litakua linakata mapema alafu faida kwao mana hua natumia yotube sana so unanjey speed lakin bando linaenda na instagram
 
hio speed ni ndogo sana, ni bundle tu ya kawaida inauzwa na isp kibao, zuku na raha ni around laki 1 ama 1 na ishirini kwa 50mbps

Kwa raha mimi nilitaka kwaajili ya biashara 50mbps plus kodi wanauza kwa dola ilikua wanataka point to point kwa 1300 dollars

Mkuu kama kuna kampuni inauza 50mbps chini ya hapo naomba details nao nahitaji huduma raha nimejaza form kabs ila nataka kampuni watakao kua cheap zaid iwe dedicated na sio shared networking plus najua share ni cheap ila sio nzuri
 
Back
Top Bottom