Kikubwa Pumzi
Member
- Jul 25, 2025
- 83
- 182
Jamani, nimelipia router ya Airtel 5G, lakini mpaka sasa sipati internet kabisa.
Nimewasiliana na 100, nikaambiwa kuna tatizo la mtandao lililowakumba watumiaji wote na kwamba internet itarudi, na kwamba siyo tatizo la kifaa wala ufundi.
Sawa, nikasema ngoja nisubiri.
Lakini cha ajabu, mpaka sasa bado sina internet. Na nilipojaribu kuuliza watu wengine wanaotumia Airtel, wanasema wao wana access internet bila shida yoyote.
Sasa hapa ndipo ninapojiuliza, Airtel mnatuonaje sisi wateja?
Hizi TSh 70,000 tunazolipa siyo kwamba tunazitoa mfukoni halafu tunacheka. Wengine tunakopa. Wengine tunazitumia kwa kazi maalum za kutafuta kipato.
Mimi kwa mfano, nimepata kazi ambayo inahitaji internet ya uhakika. Nimeweka pesa ambayo kwa kweli nilihangaika kuipata, lakini sasa nimeshindwa kufanya hiyo kazi kwa sababu internet haipo.
Naomba kuuliza watu wenye uzoefu wa mambo haya:
Mteja anaweza kulalamika wapi?
Je, ukiathirika kwa uzembe au tatizo la huduma ya kampuni ya mawasiliano, una haki ya kudai fidia? Mfano, kama ulikuwa na kazi inayokusubiri na ukashindwa kuifanya kwa sababu huduma uliyolipia haikutolewa, sheria inasemaje?
Je, ni TCRA, Fair Competition Commission (FCC), au kuna chombo kingine cha kulinda haki za mlaji?
Na kama kweli kuna tatizo la mtandao kwa watumiaji wote, kwa nini baadhi ya watu wanaendelea kutumia internet bila shida?
Kwa kweli nimeathirika sana. Sijatumia Airtel kwa muda mrefu, nikarudi kwa sababu nimepata kazi inayohitaji internet yenye uwezo wa kutosha. Nimeamua kulipia router, nimeweka pesa ambayo nimekopa, halafu huduma yenyewe haifanyi kazi.
Hivi Airtel wanaelewa kwamba kwa baadhi yetu internet siyo starehe? Ni chombo cha kazi na kipato.
Mambo kama haya ndiyo yanayofanya watu kupoteza imani na huduma za kampuni za Tanzania.
Kwa sasa mimi binafsi siwezi kumshauri mtu anunue Airtel 5G.
Bongo bado tuna safari ndefu sana kwenye customer service, integrity na kuwajibika kwa mteja. Mteja analipa pesa yake halafu akipata shida anaambiwa tu “subiri, itarudi.”
Swali langu ni moja: NIKIATHIRIKA KIFEDHA KWA SABABU YA HUDUMA NILIYOLIPIA KUTOTOLEWA, NINA HAKI GANI KISHERIA? Na ni wapi napaswa kulalamika?
Wenye uzoefu, tusaidiane hapa.