Tanzania tunanunulia wapi/nchi gani Internet?

Tanzania tunanunulia wapi/nchi gani Internet?

mambo ya digitali ndio hadi simu zetu tunazopiga zinapita kwenye hizo fiber, kwenye analog zilikuwa zinapita kwenye zile nyanya za shaba
twilight-532720_1280-1180x664.jpg
Na zile zama za buzz miaka ya 90 na 2000 mwanzoni minara ya simu ilitumia nn maana nahiss hizi cables hazikuwepo
 
Na zile zama za buzz miaka ya 90 na 2000 mwanzoni minara ya simu ilitumia nn maana nahiss hizi cables hazikuwepo
Zilikuwepo mkuu, buzz na tritel zilikuwa 2g (ilianza 1991 hii 2g) ambayo tayari ni Digital na sauti na sms zinakuwa converted kuwa data(bits). Nyuma ya Hapo ndio walikuwa wanatumia Analog ambayo ilikuwa kama unavyoona Radio call za Police, hizi zilikuwa ndio hazijaunganishwa unapiga tu simu kwenye range ya Mnara.
 
Sababu kubwa ni Nanga mkuu, japo inawezekana pia kugongwa incase sehemu ni deep sana na waya hauwezi kwenda chini.
Oooh hapo nimekupata. Halafu kuna siku ulimtumia mtu link ya kudownlodia Ms office, kama unaukumbuka ule uzi au ile link bado unayo, naiomba na mimi.
 
Zilikuwepo mkuu, buzz na tritel zilikuwa 2g (ilianza 1991 hii 2g) ambayo tayari ni Digital na sauti na sms zinakuwa converted kuwa data(bits). Nyuma ya Hapo ndio walikuwa wanatumia Analog ambayo ilikuwa kama unavyoona Radio call za Police, hizi zilikuwa ndio hazijaunganishwa unapiga tu simu kwenye range ya Mnara.
Anha mkuu naona kwa miaka ya karivuni vodacom calls zao Zimekua na ubora kuliko mitandAo mingine siri iko wapi?
Aswali la pili ile zama ya early 2000 nani alimiliki hizi cables maana mkongo wa taifa haukuwepo au sio
 
Mtanisamehe kwa hili swlai waungwana,inamaana kwa huyo mtengeneza wa kwanza internet ni muunganiko wa nini na nini,nataka kujua chanzo chake ni kama tunavyosikia umeme unatokana na maji je net inakuwaje hapo
 
internet inapitisha data, kitu chochote kinachopitisha data kidigitali kinaweza kutengeneza internet

mfano
1. madishi ya TV yale yanapitisha data kidigitali toka kwenye satelite huko mpaka nyumbani, unaweza kutengeneza internet kwa kutumia satelite mbalimbali na madishi mbalimbali kwenye majumba ya watu ama server

2. wapo jamaa wa cable tv mitaani wenyewe wanapitisha cable kwenye nyumba then unaona chanell, internet pia ni same concept cable zinaweza kupitishwa baina ya nyumba na server na computer mbalimbali kupitia hizo nyaya.

hivyo mkuu kukishakuwa na medium kama waya, modem za wireless etc ambazo zinapitisha data baina ya computer na computer lakini kwa eneo kubwa tunaita internet.
 
Kulinganisha Na vipato ni kweli Internet ni gharama kuliko vipato vyetu, ila ukilinganisha Na nchi nyengine bei zetu ni Rahisi sana.
Ukienda nchinza wenzetu, wireless ipo almost kila sehemu, almost kila nyumba ina wifi network. Mighahawa, bar, ofisi lobbies.

Ila sisi kwetu ni kuhesabu.
 
Wanaweza tumia njia kama
1. Satelite Internet, sema hii haitumiki sana ni kama backup tu.

2. Cable za Chini ya Bahari ama Nchi kavu, angalia hii picha kwa list ya provider

View attachment 1523682
Ukisikia mkonga wa Taifa ndio hizo cable, zinakuwa na bandwidth za maana, zaidi ya Terabyte kwa sekunde, kuna moja hapo inaenda hadi terabit 100.

Hizo cable ndio Internet Servoce Provider wanatumia kuunganisha na nje ya Bara la Africa.
Mkuu, asante kwa kunitoa ushamba, kiukweli kwenye mkonga wa taifa nilikua najua itajengwa kama tower hvi ndeeeeefuu, kumbe ni waya ziko chini?
 
Waya unaspeed sana tena sana sana sana compare na wireless,

Kuna kipindi fulani miaka kama 8 ama 9 iliopita meli iligonga hizo waya network ya internet ikakata nchi nzima, na baadhi ya mitandao kama voda wakaswitch kwenda satelite, ilikuwa slow balaa.
Upo deep sana mkuu
 
Mkuu,

Kuna wakati Trump alikuwa anasema hii Internet tunayotumia Africa inatoka kwao na tukiwachezea wataizima ili tukose.

Hili limekaaje chief, ni kweli wazungu wanaweza zima huko tukabaki bila kitu?
hakuna eneo maalumu maana kazi yake ni kuzungusha tu hizo data kwenda maeneo mbalimbali, mfano

- unaangalia youtube, umesearch video ya kiba, ile request yako itapelekwa na waya hadi server za youtube marekani, kisha kule marekani itachukuliwa ile video na huo waya na kuletwa hadi Tanzania.

-unachat na rafiki yako china kwa snapchat, inamaana waya utapeleka msg yako kwenye server za snapchat marekani, kisha waya mwengine utachukua na kumpelekea msg yule rafiki yako wa china

hivyo kazi za hizo waya ni kusafirisha tu taarifa baina ya watumiaji na servers mbalimbali duniani, internet inazunguka dunia nzima hakuna aneimiliki ni kama vile barabara, Tanzania tuna miundo mbinu yetu, Kenya wana yao, Usa wana yao, China wana yao etc then kuna makampuni ya kimataifa yanaunganisha miundo mbinu ya nchi mbalimbali pamoja
 
Kama nimelielewa swali lako vizuri nikujibu tu kwamba ISP kwa ni Tanzania ni:-

1. Mkonga wa Taifa By TTCL.

2. Seacom By Simbanet

3. Eassy by WIOCC

Unapozungumzia internet ni connection na hizo taarifa unapata kwenye server ,server zinaweza kuwepo sehemu yoyote hata hapa hapa tanzania kwahiyo connection tunapata kwa ISP hao niliowataja juu.

Unaweza kupata taarifa locally kwa intranet au externally kwa internet.....Unapoweka www.google.com kwenye toolbar na kusachi DNS server inatranslate kwenda IP ya google 172.XX.XX.XX server na kukupatia taarifa unayotafuta.
 
Mkuu,

Kuna wakati Trump alikuwa anasema hii Internet tunayotumia Africa inatoka kwao na tukiwachezea wataizima ili tukose.

Hili limekaaje chief, ni kweli wazungu wanaweza zima huko tukabaki bila kitu?
hawawezi labda anamaanisha zile waya zinazotoka kwao kwenda west Africa, ila still hata wakizizima unaweza ukatumia route ndefu kupitia ulaya, ping itakuwa kubwa ila utapata mawasiliano, na hata akiamrisha watufungie website zao still kuna vitu kama vpn. kifupi mkuu haiwezekani ni mikwara tu.
 
Ukienda nchinza wenzetu, wireless ipo almost kila sehemu, almost kila nyumba ina wifi network. Mighahawa, bar, ofisi lobbies.

Ila sisi kwetu ni kuhesabu.
ni kweli mkuu ila kwetu kwa buku unapata 1gb ama zaidi mitandao mingi tu, tena kwa speed nzuri kushinda majority ya hizo Wifi. wao hawana vitu kama hivi, mobile data ni ghali sana huko.
 
Umeeleweka mkuu, asante sana
hawawezi labda anamaanisha zile waya zinazotoka kwao kwenda west Africa, ila still hata wakizizima unaweza ukatumia route ndefu kupitia ulaya, ping itakuwa kubwa ila utapata mawasiliano, na hata akiamrisha watufungie website zao still kuna vitu kama vpn. kifupi mkuu haiwezekani ni mikwara tu.
 
Mbona zimechimbiwa kitambo mkuu huonagi vitofali vya njano pembeni ya barabara kuu zote ukitoka dar ndo mkonga/FIBRE zmetembea humo .kama nguzo za umeme vile ikifika kwenye mji wanasambaza kwenye minara michache ya karibu na town alafu wanaboost signal kwenda mingine ya pembeni. Huo waya ukizingua mnajikuta mtandao flan unasumbua kwa wote siku hiyo. Na ukiwa kwa juu utaona minara imefatana kama nguzo tu kuingia interior kutokea main road.
Tuwekee ka picha please tujifunze kitu kiongozi
 
Mkuu,

Kuna wakati Trump alikuwa anasema hii Internet tunayotumia Africa inatoka kwao na tukiwachezea wataizima ili tukose.

Hili limekaaje chief, ni kweli wazungu wanaweza zima huko tukabaki bila kitu?
Tupe ushahidi wapi walisema.
 
Back
Top Bottom