Tanzania ni nchi ya pili Afrika kuamini uchawi na ushirikina. Elimu duni, kuamini dini sababu kuu za kuamini uchawi sana

MELEKAHE

JF-Expert Member
Nov 19, 2023
434
1,966
Nchi zinazoongoza kwa kuamini ushirikina (uchawi) barani Afrika.
1. Cameroon
2. Tanzania.

DINI NI SABABU YA WATANZANIA KUAMINI SANA UCHAWI NA USHIRIKINA

Ukiamini dini za ukristo na uislamu ni lazima pia uamini na ushirikina maana imani hizo zinategemana.

Quran imeongelea ushirikina na ina sura kabisa ya majini.. ukiwa muislamu maana yake lazima uamini majini yapo na ni lazima uamini ushirikina na uchawi upo. ukigoma kuamini maana yake unabishana na Quran yenye Topic kabisa ya majini.

Mkristo na yeye biblia ina mistari mingi inayosema uchawi upo. hivyo ukigoma kuamini kwamba uchawi upo maana yake unabishana na biblia takatifu hivyo wewe sio Mkristo.

310459610_2748495355290491_9176532087696591968_n(1).jpg

ushirikina.jpg

1711576429561.png

Ukweli mchungu Hakuna kirusi kitakachokuja kutengenezwa Duniani kiwe na madhara makubwa kwa nchi zetu za Africa kama dini za ukristo na uislamu
 
1. Tuna dini sana, ushirikina sana.

2. Tuna umaskini sana.

Kipi kimemsababisha mwenzake hapo? Chemsha ubongo.

ukiamini dini za ukristo na uislamu ni lazima pia uamini na ushirikina maana imani hizo zinategemana.

quran imeongelea ushirikina na ina sura kabisa ya majini.. ukiwa muislamu maana yake lazima uamini majini yapo na ni lazima uamini ushirikina na uchawi upo. ukigoma kuamini maana yake unabishana na Quran yenye Topic kabisa ya majini

mkristo na yeye biblia ina mistari mingi inayosema uchawi upo. hivyo ukigoma kuamini kwamba uchawi upo maana yake unabishana na biblia takatifu hivyo wewe sio mkristo

DINI NA UCHAWI VINATEGEMEANA
 
1. Tuna dini sana, ushirikina sana.

2. Tuna umaskini sana.

Kipi kimemsababisha mwenzake hapo? Chemsha ubongo.
Undumilakuwili. Asubuhi ni waislamu na wakristo, Usiku ni watu wa jadi. Mwisho wa siku maombi yanaishia hewani hayamfiki Mungu yoyote hapo. Ni bora wangekuwa wanajikata kwenye shughuli za maendeleo kuliko kwenda sehemu za ibada tujue moja.
 
Undumilakuwili. Asubuhi ni waislamu na wakristo, Usiku ni watu wa jadi. Mwisho wa siku maombi yanaishia hewani hayamfiki Mungu yoyote hapo. Ni bora wangekuwa wanajikata kwenye shughuli za maendeleo kuliko kwenda sehemu za ibada tujue moja.
Duh!
Vigagula wanapaa na ungo na kuzidaka dua za upako na albadiri kwenye stratosphere na kuzipiga pini :D
 
Atheists wengi ni wapumbavu kama mtoa mada ,Africa yote inaamini uchawi haswa mizimu hata wale wazee wa December ukienda ukerewe ndio usiseme.

Uislamu unasema dhambi zote zinasamehewa isipokuwa ushirikina ,ni kwamba watu wameonya kuhusu ushirikina kabisa..wengi wanadai dini zimekuja kuharibu mila za waafrica eti kisa inakataza uchawi

Wewe unaongea ujinga ,halafu hata hayo mafanikio hauna umebaki na idea za kijinga ,unaongelea vip ushirikina ambao haitaki kuamini😅😅.

Uwe unasoma usiwe mpumbavu matatizo yako yanatokana na wazazi wako maskini ,acha kujumuisha watu kweny ujinga wa ukoo wako

Atheists wote ni wapumbavu badala wapambane na maisha yao ,wanalalamikia dini ambazo hawaamini.
 
Kwanza takwimu zenu mnajichanganya mara Tanzania ni ya pili kwenye maelezo mara ni ya kwanza kwenye namba!

Pili, inaonekana mna nia fulani mliyojaribu kuificha lakini imeshindikana. Mlitaka kutukana dini tu

Tatu, Hicho unachosingizia tena umejichanganya. Kwa sababu kama ingekuwa ni hivyo ilitakiwa tuone vinara hapo wakiwa ni mabeberu wa Afrika kusini, Kenya nk au waarabu wa Tunisia, Morocco, nk maana kwa matusi yenu ni kwamba ukristo na uislamu ndo unasababisha imani za kishirikina. Inakuwaje tuwe vinara sisi tulioletewa dini hizi (kama mnavyodai) halafu wenyewe waliozitunga (kama mnavyodai) wawe nyuma?

Nne, huwa mnapinga uwepo wa Mola, uchawi, majini, malaika na mfano wa hayo sasa mbona mnapenda kuyajadili sana mambo hayo wakati kwenye uhalisia wa maisha yenu hayapo? Mnateseka na kipi? Kitu hakipo sasa haunt ya nini tena?

Tano, najua mtaruka hoja namba tatu kwamba tumepigwa changa sisi huku wenyewe wakijilia maisha. Well, tufungue sasa minakasha (midahalo) hapa mtuoneshe hiyo sehemu dini ya ukristo na uislamu zinapofundisha watu wake imani za kishirikina?

Twende kwa hoja ya uislamu hapo, umesema quran tukufu imekuja na sura nzima ya majini! Kwanza ujue kabisa Quran imewataja viumbe hao siyo kwenye sura hiyo tu! Tena jambo hili naomba lieleweke vizuri sana. Wengi wanadhani sura ikiitwa jina fulani basi ndo sura nzima imehusika na kitu hicho, hapana! Sura chache sana zitazungumza kitu husika kama ilivyo jina la sura mfano surat yusuf, hii imeeleza kisa cha yusuf mwanzo mwisho. Lakini sura nyingine unakuta jina la sura ukakuta maudhui yake kwenye baadhi ya aya tu au kipande cha aya mfano Surat Dukhaaan, Baqara, Naml Ankabut nk. Hii ni kumrahisishia msomaji wa haki na kumkomesha msomaji wa kukariri na kukejeli

Tuache hapo sasa tuendelee, tuambie quran na surat jin imesababishaje waislamu wa Tanzania wawe na imani za kishirikina (yaani uhusiano ni upi?). Maana nijuavyo kwenye quran imesemwa ushirikina ndiyo dhambi (dhulma) kuu na akifa nayo mtu kabla ya kutubu basi ni motoni moja kwa moja! Kwa upande wa majini kwanza kuna huyo mshenzi ibilisi ambaye ni chanzo cha maovu yote huyu anajulikana ni wa motoni halafu kuna majini wengine ambao wamegawika makundi kuna wema na waovu kama ilivyo kwa binadamu kuna wema na waovu
 
Nje ya dini,uchawi upo hata bila dini,jamii zote duniani zinaamini uchawi upo.
Wayahahudi ndio wachawi kuliko wote.
 
Uchawi wa mwafrika ni WA level ya chini hauna nguvu thus ulishindwa kumzuia mkoloni
 
Back
Top Bottom