sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,033
uchawi upo na hutuwezi kuuepuka kwa kuamini kwamba haupo, Kama wewe ni Mkristo au Muislam lazima uamini uwepo wa uchawi lakini hupaswi kuuamini kwa matumizi.
Hapa nazungumzia uchawi sio matambiko maana matambiko mengi yana lengo positive kuondoa tatizo japo kuna baadhi ya matambiko yapo kichawi, uchawi lengo lake huwa ni moja tu, KUHARIBU MAENDELEO YA WATU (waweza tajirika lakini masharti yakakunyima uhuru).
Ni sayansi ya nguvu za giza zenye lengo la kudhuru iwe ni kutupia mtu busha, kumtupia majini, kumsumbua usiku, kumuua, n.k. ilimradi mtu akwame kwenye maendeleo.
Mambo ya uchawi yamekuwa yana nafasi kubwa sana hata kwa viongozi wa juu hapa Afrika, hapa kwetu huwa tunajionea mambo haya live kipindi cha chaguzi za wabunge ambao huja kuwa mawaziri na baadae hata maraisi, Ukienda Afrika Kusini nako viongozi wanatembea na Muthi (Hirizi) kwa lengo la kujibusti, Nigeria nako nchi inayongoza kwa maendeleo bara la Afrika kwa nchi za sub saharan nao hawapo nyuma.
Kutumia Akili uliyopewa kuna nguvu kuzidi uchawi, hilo linadhihirishwa vita ya maji maji mtaalam wa kuitwa Kinjikitile Ngwale aliwatengenezea kinga babau zetu dhidi ya risasi na kilichotokea kimebaki kuwa historia ya aibu, watu wanaamini bado kupaa na nyungo wakati ndege zilishatengenezwa kitambo, wachezaji wazuri hasa wa kigeni wanasajiliwa na timu zetu lakini wanarogwa na wenzao wanaolazimisha kupewa namba uwanjani hata kama viwango vimeshuka, n.k.
Si Africa tu, hata nchi za huko Amerika ya kusini kama Haiti imejaa Waafrika ndio inaongozea kwa umasikini ila ndio kinara wa mambo ya uchawi ukanda huo.