Tanzania ni nchi pekee duniani inayopuuza tamaduni zake

Mr Why

JF-Expert Member
Nov 27, 2019
1,118
1,915
Husika na kichwa cha habari cha mada hii. Ni kweli kuwa Tanzania ni nchi pekee duniani inayopuuza utamaduni wake na kuiga tamaduni za nchi nyingine za Afrika na ulimwenguni kwa ujumla.

Katika swala la utamaduni kwa upande wa Tanzania basi haishikilii chake inatupa na kushikilia ya wageni. Tuanze na Muziki wa Tanzania,

Muziki wa Tanzania ni Bongo Flava, RnB, Hip Hop, Taarabu, Kibaokata, Singeli, Kaswida, Msondongoma nk,

Katika chambuzi za genre hizi tukianza na Bongo Flava, hii ni ile genre ya muziki wa Pop wa Marekani ilikopwa na Tanzania ambayo huimbwa kwa lugha ya Kiswahili kwahiyo sio asili ya Tanzania.

RnB ni hii ya Marekani inaimbwa hapa Tanzania kwa lugha ya Kiswahili lakini sio asili yetu.

Hip Hop ni asili ya Marekani pia nayo imekopwa na Tanzania ikiimbwa kwa lugha ya Kiswahili kwahiyo sio asili yetu.

Kaswida hii ni aina ya Muziki kutoka kwa Waarabu Tanzania imekopa na kuimba kwa lugha ya Kiswahili lakini sio asili ya muziki wa Tanzania.

Asili ya Muziki wa Tanzania ni hizi zifuatazo,
Taarabu hii ni asili ya Muziki wa Tanzania na hakuna Taifa jingine hapa duniani lenye ujuzi wa muziki huu zaidi ya Tanzania.

Kibaokata ni asili ya Muziki wa Tanzania wenye utaalamu wa kuimba na kucheza ni Watanzania peke yao.

Singeli hii ni asili ya Muziki wa Tanzania inayofanywa na kizazi kipya ambao ndio wajuzi wa aina hii ya Muziki.

Msondongoma ni muziki asili wa Tanzania unaochezwa na kuimbwa na Watanzania peke yao.

Kwa maelezo haya mafupi tunaweza kugundua kuwa Tanzania tumepoteza asili yetu ndio maana mataifa yote duniani yanatupuuza na kutuona wafu kwasababu ya sisi kuiga tamaduni zao na kuacha zetu.

Tabia ya tamaduni ni kuwa kila nchi inatakiwa kushikilia tamaduni zake ili iwe na Identity ya kuonesha kwa wengine.

Madhara ya kuiga tamaduni za mataifa mengine ni kuwa, aliyeigwa anamuona muigaji kama mpuuzi, lakini anajiuliza kwanini muigaji asioneshe asili yake ili asiyeijua akaburudishwa nayo?

Mwanamuziki anapoiga asili ya muziki wa nchi nyingine ni kuwa shabiki humuona kama feki na kuacha kufuatilia muziki wake na kufuatilia Origin ya huo muziki kwasababu ndio utakaomburudisha kuliko huo feki.

Njia za kutibu huu ugonjwa ni Producers na Wasanii wa Singeli, Taarabu, Kibaokata, Msondongoma watengeneze nyimbo nyingi ziteteme Tanzania nzima kwa kasi ili dunia itutambue kwasababu mpaka sasa hatuna Identity yetu tumekuwa kama wafu.

Ndugu zangu ni aibu kubwa pale tunapowatazama watu wa Nigeria, Afrika Kusini, Ghana, bara lote la Asia wanavyokuza na kuheshimu tamaduni zao angali sisi tukiduwaa na kukosa Identity ya kupeleka duniani.

Lawama zote ziwaendee Baraza la sanaa la Tanzania amkeni manake mmelala ninyi ndio mnaochangia utamaduni wa Watanzania kupotea kwa kuwaruhusu wasanii kuiga tamaduni za mataifa mengine na kutupa zetu.

Nchi isiyo na utamaduni wake peke yake ni sawa na nchi mfu.
 
Tanzania ina makabila zaidi ya 130 yenye mila na tamaduni tofauti, ni ngumu sna kuwa na kitu kimoja tuite asili yetu kwa pamoja.
 
Tanzania ina makabila zaidi ya 130 yenye mila na tamaduni tofauti, ni ngumu sna kuwa na kitu kimoja tuite asili yetu kwa pamoja.
Inawezekana kutengeneza chetu kwa kutumia Baraza la Utamaduni
 
Inawezekana kutengeneza chetu kwa kutumia Baraza la Utamaduni
Sure , vazi la taifa ni vazi lipi na asili yake ni kabila gan ,kwa sababu hizo nyimbo zote ulizosema ni za tanzania ni kwel ni za apa ila zina asili ya mwambao wa makabila ya pwani, sio kote zinakubalika .
 
Tanzania ina makabila zaidi ya 130 yenye mila na tamaduni tofauti, ni ngumu sna kuwa na kitu kimoja tuite asili yetu kwa pamoja.
Pamoja na utofauti mkubwa wa makabila na Mila, Tamaduni na Desturi zilizopo kati yetu kutokana na utofauti wa makabila yetu, lakini kuna vitu/Tabia/kasumba/mazoea/tamaduni tunazochangia (share) Kama watu tunaotokea sehemu moja ya ardhi.

Kuna tamaduni za watu kutoka eneo fulani na tamaduni za watu wa kabila fulani, za kwanza haziangalii dini, kabila wala maumbile. Huku hizo za pili zikiwa na mipaka yenye sheria tofauti kati ya kabila na kabila.
 
Husika na kichwa cha habari cha mada hii. Ni kweli kuwa Tanzania ni nchi pekee duniani inayopuuza utamaduni wake na kuiga tamaduni za nchi nyingine za Afrika na ulimwenguni kwa ujumla...
Tz ina nini inachofanya kwa umakini? Labda wizi na rushwa.
 
Sure , vazi la taifa ni vazi lipi na asili yake ni kabila gan ,kwa sababu hizo nyimbo zote ulizosema ni za tanzania ni kwel ni za apa ila zina asili ya mwambao wa makabila ya pwani, sio kote zinakubalika .
Tangu nazaliwa sijui vazi asili la kijana wa kiume wa Kitanzania lakini la Nigeria bila shaka tunalifahamu ni kanzu ya Kitenge kama sijakosea.

Tazama jinsi Nigeria wanavyothamini chao. Nina hamu kubwa sana ya kwenda kuwadai Baraza la Utamaduni hii haki yetu hatujaipata
 
Pamoja na utofauti mkubwa wa makabila na Mila, Tamaduni na Desturi zilizopo kati yetu kutokana na utofauti wa makabila yetu, lakini kuna vitu/Tabia/kasumba/mazoea/tamaduni tunazochangia (share) Kama watu tunaotokea sehemu moja ya ardhi.

Kuna tamaduni za watu kutoka eneo fulani na tamaduni za watu wa kabila fulani, za kwanza haziangalii dini, kabila wala maumbile. Huku hizo za pili zikiwa na mipaka yenye sheria tofauti kati ya kabila na kabila.
Nmefikir sana ila naona tuna share zaid umbea , wivu , kusengenyana ,uchawa na uwoga ,ujuaji na kuibua vijineno flani na matukio flani kama la wasudani ,tunavumisha kwa wote then linapita kama halikuwepo.
 
Niliwahi kumwambia mtu siku mmasai atakaposlim na kuwa muislam basi hakutakua tena na mmasai
Kwa sababu wamasai wanaume hawatasuka nywele zao tena, na wala hawatavaa mavazi yao ya asili (rubega) maana wataonekana wanatembea uchi, wanawake hawatatembea vichwa wazi na kuonesha urembo wao. Zile bangili na shanga hawatavaa tena

Kwao mavazi yatakua ni baibui na kanzu tu, viatu vyao vya asili hawatavaa tena.

Je hapo kutakua na mmasai? Jibu ni hapana.

Ili kuweza kudumisha tamaduni zetu ni lazima tukatae tamaduni za kigeni
 
Niliwahi kumwambia mtu siku mmasai atakaposlim na kuwa muislam basi hakutakua tena na mmasai
Kwa sababu wamasai wanaume hawatasuka nywele zao tena, na wala hawatavaa mavazi yao ya asili (rubega) maana wataonekana wanatembea uchi...
Tena tukatae kwa nguvu zote
 
Inawezekana kutengeneza chetu kwa kutumia Baraza la Utamaduni
Inawezekana lakini kukubalika kwa watu wote si rahisi.

Hivi mguu unajua like vazi la asili la wanawake wa kiganda linaitwa guma kumbe alilibuni mzungu kama uniform ya wanafunzi wa shule aliyokuwa akiiongoza enzi za ukoloni
 
Naona hata ukristu ni mambo tu ya kuiga, ni utamaduni wa wazungu. Unaacha jina lako la asili unachukuwa la kizungu.
Sio ukristo tu bali ni dini zote tulizoletewa, kama ambavyo wakristo wanajiita majina ya kizungu na waislam nao wapo bize kuwapa watoto wao majina ya kiarabu.

Tumeacha tamaduni zetu na kuiga tamaduni za wageni Kwa kisingizio cha dini
 
Inawezekana lakini kukubalika kwa watu wote si rahisi.
Hivi mguu unajua like vazi la asili la wanawake wa kiganda linaitwa guma kumbe alilibuni mzungu kama uniform ya wanafunzi wa shule aliyokuwa akiiongoza enzi za ukoloni
Bado hatujaweka juhudi yeyote ndio maana kwenye sanaa tunaona mambo yasiyo asili yetu yakifanywa na wasanii wetu ambao kwa uso wa dunia wanaonekana feki
 
Back
Top Bottom