Mr Why
JF-Expert Member
- Nov 27, 2019
- 1,125
- 1,922
Husika na kichwa cha habari cha mada hii. Ni kweli kuwa Tanzania ni nchi pekee duniani inayopuuza utamaduni wake na kuiga tamaduni za nchi nyingine za Afrika na ulimwenguni kwa ujumla.
Katika swala la utamaduni kwa upande wa Tanzania basi haishikilii chake inatupa na kushikilia ya wageni. Tuanze na Muziki wa Tanzania,
Muziki wa Tanzania ni Bongo Flava, RnB, Hip Hop, Taarabu, Kibaokata, Singeli, Kaswida, Msondongoma nk,
Katika chambuzi za genre hizi tukianza na Bongo Flava, hii ni ile genre ya muziki wa Pop wa Marekani ilikopwa na Tanzania ambayo huimbwa kwa lugha ya Kiswahili kwahiyo sio asili ya Tanzania.
RnB ni hii ya Marekani inaimbwa hapa Tanzania kwa lugha ya Kiswahili lakini sio asili yetu.
Hip Hop ni asili ya Marekani pia nayo imekopwa na Tanzania ikiimbwa kwa lugha ya Kiswahili kwahiyo sio asili yetu.
Kaswida hii ni aina ya Muziki kutoka kwa Waarabu Tanzania imekopa na kuimba kwa lugha ya Kiswahili lakini sio asili ya muziki wa Tanzania.
Asili ya Muziki wa Tanzania ni hizi zifuatazo,
Taarabu hii ni asili ya Muziki wa Tanzania na hakuna Taifa jingine hapa duniani lenye ujuzi wa muziki huu zaidi ya Tanzania.
Kibaokata ni asili ya Muziki wa Tanzania wenye utaalamu wa kuimba na kucheza ni Watanzania peke yao.
Singeli hii ni asili ya Muziki wa Tanzania inayofanywa na kizazi kipya ambao ndio wajuzi wa aina hii ya Muziki.
Msondongoma ni muziki asili wa Tanzania unaochezwa na kuimbwa na Watanzania peke yao.
Kwa maelezo haya mafupi tunaweza kugundua kuwa Tanzania tumepoteza asili yetu ndio maana mataifa yote duniani yanatupuuza na kutuona wafu kwasababu ya sisi kuiga tamaduni zao na kuacha zetu.
Tabia ya tamaduni ni kuwa kila nchi inatakiwa kushikilia tamaduni zake ili iwe na Identity ya kuonesha kwa wengine.
Madhara ya kuiga tamaduni za mataifa mengine ni kuwa, aliyeigwa anamuona muigaji kama mpuuzi, lakini anajiuliza kwanini muigaji asioneshe asili yake ili asiyeijua akaburudishwa nayo?
Mwanamuziki anapoiga asili ya muziki wa nchi nyingine ni kuwa shabiki humuona kama feki na kuacha kufuatilia muziki wake na kufuatilia Origin ya huo muziki kwasababu ndio utakaomburudisha kuliko huo feki.
Njia za kutibu huu ugonjwa ni Producers na Wasanii wa Singeli, Taarabu, Kibaokata, Msondongoma watengeneze nyimbo nyingi ziteteme Tanzania nzima kwa kasi ili dunia itutambue kwasababu mpaka sasa hatuna Identity yetu tumekuwa kama wafu.
Ndugu zangu ni aibu kubwa pale tunapowatazama watu wa Nigeria, Afrika Kusini, Ghana, bara lote la Asia wanavyokuza na kuheshimu tamaduni zao angali sisi tukiduwaa na kukosa Identity ya kupeleka duniani.
Lawama zote ziwaendee Baraza la sanaa la Tanzania amkeni manake mmelala ninyi ndio mnaochangia utamaduni wa Watanzania kupotea kwa kuwaruhusu wasanii kuiga tamaduni za mataifa mengine na kutupa zetu.
Nchi isiyo na utamaduni wake peke yake ni sawa na nchi mfu.