Kila mtu ni mtumwa wa utamaduni wake

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
6,088
8,474
Kama umezaliwa kijijini kwenu, ukakulia kijijini kwenu, ukasomea kijijini kwenu, na shughuli zako zote ukazifanyia kijijini kwenu, ni rahisi kuamini kuwa mila na desturi zenu ndizo bora kuliko zingine zote. Lakini wakati huo huo, kwa watu wa tamaduni zingine, wanaweza wakawa wanawashangaa jinsi mlivyo na utamaduni wa ajabu.

Na, kwa muktadha wa Uzi huu, utamaduni wako si lazima uwe na asili ya kabila lako, bali utamaduni wo wote ule ulioukubali na kuwa sehemu ya maisha yako.

Kuna mila zingine, kwa mfano, ambazo wakati wahusika wakijitahidi kuzikumbatia, watu wa nje na huo utamaduni wanawaonea huruma kwa kuwaona kuwa wanateseka. Mfano, ukeketaji kwa wanawake, kutahiri vijana wa kiume bila ganzi, n.k.

Ikitokea mtu amesoma, na kubaini kuwa baadhi ya mila zao ni "mbaya" na hivyo kuamua kuachana nazo, wenzake wa Jamii yake humhesabu kuwa kapotoka huku yeye akiwa na kuwa ni wajinga.

Tamaduni huwafanya watu waliozikubali kuwa watu wa wake.

Na, kila mtu ni mtumwa wa utamaduni aliouridhia.
 
Wanaume wangapi wangeikubali hiyo changamoto?

Lakini dogo kwa kuwa anataka atambuliwe na watu wa utamaduni wake kuwa yeye naye yumo, kaikabili "kiroho safi"
 

Attachments

 • mtoto_wa_miaka_sita_kutahiriwa_Kwa_kisu_mbele_ya_umati_mchana____Luhyia_culture(144p).mp4
  7.7 MB
Unawaonaje hawa?
 

Attachments

 • Omo_valley_Mursi__Tribe__Feb_2020(144p).mp4
  619.4 KB
 • Woman_from_Surma_tribe_inserts_lip_plate___Omo_Valley_Ethiopia_#shorts(240p).mp4
  461.4 KB
 • Omo_Valley_Mursi_tribe_village_life_in_the_morning(240p).mp4
  5.9 MB
Unafikiri siku hiyo mkuu wa wilaya alitafsiriwaje na hao wanaume?
 

Attachments

 • KUTAHIRIWA_UKUBWANI_SI_MCHEZO___MCHECK_MKAKA_HUYU_KILICHOMKUTA(144p).mp4
  5.3 MB
Wamependeza hawajapendeza?
 

Attachments

 • Why_Do_the_Mangbetu_People_have_Elongated_Heads_(144p).mp4
  6 MB
Ukifikiri wanaotekeleza "mila" ni watu wasio na "exposure" peke yao! Hata "waheshimiwa" nao wanazoheahimu.
 

Attachments

 • Nyumban_kwa_MBUNGE_GIBSON_MESEYEK_muda_mfupi_kabla_ya_kutahiri_vijana_wake_kimila(144p).mp4
  8.8 MB
 • Waitara_azikingia_kifua_Mila_za_Kikurya,_anena_mazito__Ametahiliwa_mara_mbili_(360p).mp4
  8.8 MB
Kilichokufanya usiwe kama wao ni kwa sababu hukuzaliwa miongoni mwao.
 

Attachments

 • The_Most_Unique_Humans_on_Earth!!!__Omo_Valley_(240p).mp4
  6.4 MB
 • MAAJABU_YA_MAKABILA_HAYA_YANAYO_TOBOA_WANAWAKE_MIDOMO_NAKUWAWEKEA_VISAANI_NCHINI_ETHIOPIA(360p).mp4
  16.4 MB
Fisi siyo usafiri wa wachawi
 

Attachments

 • Mji_wa_Ethiopia_ambao_wakazi_huishi_na_fisi(360p).mp4
  7.4 MB
Kuwa "mwanaume" si lelemama
 

Attachments

 • MAAJABU_YA_TOHARA_ZA_WAKURYA_SERENGETI_MARA_TANZANIA.(144p).mp4
  1.9 MB
 • Tazama_mila_za_kimasai_kutahiri(144p).mp4
  3.6 MB
Huu utumwa tuchukulie ni kama jela. Kuna jela mbalimbali hapa duniani, ila jela kuu ni Muda na Nafasi. Jela ndogo ndogo ndogo tunaweza vigawanya ambazo mawikli jela zinazonekana na zile zilizo katika fikra.

Jela zinazoenekana
1. Mito
2. Mlima
3. Msitu wenye wanyama wakali
4. Bahari
5. Jangwa
6. Barafu
7. Nchi
8. Jumuiya
9. Bara
10. Dunia
11. Jua
12. Galaxy
13. Multiverse
14. Gereza

Jela za fikra

1. Dini
2. Utamaduni
3. Elimu
4. Exposure
5. Genetic
6. Psychological
7. Malezi
9. Personality
10. Sexuality
11. Gender.
 
Kila binadamu afuate anachokifuata yupo sahihi ,mtu anakosoa halafu hana msaada wowote.
Ni sahihi mkuu, ila anachokiamini kisiwaletee wengine madhara. Mila na desturi za kipuuzi hazifai.

Ona;
1. Kuna wajinga wanaoamini kuwa albino ni "bidhaa"

2. Kule Nigeria, kuna jamii inayowatupa watoto wadogo kwa visingizoo kuwa ni wachawi

3. Madagascar nako si salama. Watoto wanaozaliwa mapacha hukabiliwa na "adhabu" ya kifo. Hutakiwa kuuwawa ili kufurahisha "mizimu" yao.

Vile vile, watu wa hiyo Jamii hawaruhusiwi kujenga vyoo.
 

Attachments

 • I_Chose_Die_With_My_Albino_Children___EXTRAORDINARY_STORY(144p).mp4
  13.6 MB
 • Aid_Worker_Saves_Nigerian_Boy_Accused_Of_Being_A_Witch(360p).mp4
  3.4 MB
 • The_Cursed_Twins___Unreported_World_Shorts___Channel_4(144p).mp4
  3.1 MB
 • Abandoned_at_birth__the_cursed_twins_of_Madagascar___Unreported_World(144p).mp4
  34.9 MB
Back
Top Bottom