The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 5,462
- 17,277
Mimi kama mkazi wa Ukonga, naetumia barabarani ya Tabata naomba kutoa ombi kwa IGP ama mkuu wa usalama wa barabarani mkoa wa Dar es Salaam.
Inajulikana kwamba asubuhi ni muda wa rush hours, watu wanawahi kwenda kwenye shughuli zao za kiuchumi na pia inajulikana setup ya barabara zetu asubuhi gari nyingi zinaelekea upande wa mjini na jioni zinatoka mjini kurudi nyumbani.
Hivyo ni common sense tu kwamba askari wa usalama barabarani kwa asubuhi wasaidie gari zinazoelekea mjini kufika mapema na jioni zinapotoka mjini kufika majumbani mapema.
Cha ajabu askari wa usalama barabarani wa Tabata kila siku sa 12 wako barabarani sio kwa kusaidie gari zipite kwa haraka bali kutengeneza foleni kwa faida yao wenyewe hivyo unakuta barabara ya kutoka mjini kuja Segerea iko tupu, nyeupe lakini barabara ya kwenda mjini imejaa foleni bola sababu za msingi huku askari wakiwa wamejazana barabarani kuanzia magereza hadi barakuda.
Hii foleni hua wanaotengeneza kwa faida yao ili ikitokea umechepuka hata kama mistari ya barabarani inakuruhusu, wanakukamata na kukuandikia faini ya makosa 2 ya matumizi mabaya ya barabara ama uwape kitu kidogo usamehewe.
IGP ama mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Ilala, tupunguzie hawa, wamekua ni kero hasa nyakati za asubuhi.