JF Toons
Digital Art by JF
- Feb 19, 2024
- 32
- 66
Kweli, matumizi ya taa za gari ni muhimu sana kwa usalama barabarani. Kutumia mwanga mkali (full light) katika mazingira ya foleni au msongamano wa magari kunaweza kuwa hatari kwa sababu ya athari ya kumulika moja kwa moja kwa madereva wengine.
Hii inaweza kusababisha kutopata mwelekeo mzuri wa kina, kuchanganyikiwa, au hata kusababisha usumbufu au ajali.
Kwa bahati mbaya, baadhi ya madereva hutumia taa za gari kwa njia isiyo sahihi au bila kuzingatia mazingira yanayowazunguka.
Elimu juu ya matumizi sahihi ya taa za gari na uelewa wa jinsi mwanga unavyoathiri madereva wengine ni muhimu kuboresha usalama barabarani.
---
Matumizi ya taa barabarani yanaongozwa na kifungu cha 39C cha sheria ya Usalama Barabarani, yaani The Road Traffic Act, Cap.168
Nini Maana ya Neno Usiku?
Kwa mujibu wa kifungu cha 39C (1), neno “Usiku” linamaanisha kipindi kati ya jua kuzama na jua kuchomoza, na pia inahusisha wakati wote ambapo kunakuwa na uoni hafifu kwa sababu ukungu, mvua, kupita kwenye handaki au kwa sababu nyingine yoyote ile.
Wakati wa Kutumia taa na aina ya taa zinazoruhusiwa
Sheria hii inalazimisha kila dereva anayeendesha gari barabarani usiku kuwasha taa na atatumia taa zilizotengenezwa maalumu kwaajili ya gari hilo.
Na wakati wowote dereva atatumia taa kubwa mbili zenye kutoa mwanga mweupe zilizopo upande wa mbele wa gari lake na taa nyekundu mbili zilizopo nyuma ya gari lake. [Kif.39C (2)]
Pikipiki au chombo kingine chenye magurudumu mawili kitatuma angalau taa moja nyeupe mbele na taa moja nyekundu nyuma. [Kif.39C(3)]
Matumizi Sahihi ya Taa
Gari linapoendshwa barabarani, dereva wa gari hilo atatumia taa za mwanga mkali (full beam) au taa za mwanga wa kawaida (dipped headlights) kulingana na mazingira ya uoni ya wakati huo. [Kif.39C(4)]
Matumizi ya taa zenye Mwanga kidogo [Dippled headlights]
Taa zenye mwanga kidogo zitatumika
(a) Maeneo yote ya makazi yenye taa za kuangaza barabarani(street lights);
(b) Dereva anapopishana na gari jingine
(c) Dereva anapotaka kuovateki na kulipita gari jingine ili kumfanya dereva mwenzie aendelee kuona vizuri.
Je, ushawahi kushuhudia madereva huadhibiwa kwa matumizi mabaya ya taa?