Tanzania haijaolewa EAC - Samwel Sitta

Tanzania haijaolewa EAC - Samwel Sitta

Jana nilimsikia Museveni akiongea kwa tahadhari kubwa kuwa Tanzania haijatengwa bali kwa sasa wanashughulikia Northern Corridor yaani Mombasa - Kampala - Kigali! Baadaye watashughulikia Southern Corridor yaani Dar - Tabora-Kigoma - Mwanza!


Ni kweli MUSEVENI alikuwa makini mno.Hata alipoulizwa na mwandishi wa habari kuwa Kuna kiongozi wa Tanzania alisema kile kikao chao kilikuwa illegal kulingana na makubaliano ya EAC alijibu kuwa hafanyi kazi kupitia waandishi wa habari hadi atakapopata barua rasmi kutoka kwa huyo kiongozi ndio atajibu kwani waandishi wa habari mara nyingi waongo.

Kwa ujumla MUSEVENI alikuwa makini mno kuepuka maswali mtego yaliyoilenga Tanzania.

Nafikiri anakumbuka wema nchi iliomfanyia.Mzee Kawawa alimkabidhi dola 50,000 zimsaidie kuanza vita Uganda ashike nchi.Pale alionekana ndiye kinara wa kujibu maswali na alikuwa katulia mno.Yale maswali yangeenda kwa Kagame au Kenyatta sijui wangejibuje?
 
hizi kauli zingine mbona ni balaa .. sasa muoa na muolewa... na mshenga ni yupi sasa
 
Hii nchi ya mipasho tu, viongozi wetu wanayaweza maneno ya kwenye kanga tu.!!!
 
Ha ha ha ha ha ha nimeipenda hii Tanzania kwasababu ina eneo 52% huku nchi nyingine zikibakiwa na 48%.Hapa Tanzania ni muoaji kwakigezo cha eneo ngoja wala urojo wakusikie.

Ngongo hawa wala UR0J0 hawana N0MA kwakuwa ni WATANZANIA na0 tuk0 na0 katika KU0A! Wasih0fu kabisa🙂
 
Mimi nitaendelea kuwa na msimamo kuwa, surely we don't need EAC in the prevailing situation (having Kagame and Museveni with their ideology of creating Bahima Empire). These two are violent tyrants, war mongers, ready to shed innocent blood to have their goals attained. Muungano ni kitu kizuri sana, lakini sio kuungana na watu wenye nia mbaya kama hao wawili!.. Ni watu ambao hawana nia njema na Tanzania, na hata huo muungano wa EAC hawana nia njema nao kwani wana agenda zao za siri!... Tuwe makini sana na hawa watu watutsi (nisieleweke kuwa ni mbaguzi au nina chuki na watutsi, la hasha, ila tabia zao ovu ndio ninazozichukia)...
Kwa mawazo yako hao Musaveni na Kagame watakuwa presidents for life au vipi, tujitahidi kuangalia mbele zaidi na sio kujikumbatia na misifa,..mara nyingi ukiwa na tatizo suluhisho la kudumu ni kulifanyia kazi na sio kulikimbia,..
 
Dodoma. Wabunge wa bunge la tanzania wamedai kuwa tanzania imepewa talaka ndani ya jumuiya ya EAC, kutokana na kitendo cha kenya, rwanda na uganda kuamua kujiunga wenyewe na kutengeneza shirikisho lao bila kushirikisha tz & burundi.. Kitendo cha nchi izo kuanzisha system ya kusafiri bila pasport na kuamua kutumia bandari ya mombasa tu, ndivyo vilivyokasirisha wabunge wa tanzania.

sasa na wao wameamua nini au wanaishia kulalama tu??
 
Bungeni leo kwenye kipindi cha maswali na majibu akijubu swali la Mbunge John Komba kuhusu EAC Waziri wa wizara ya Afrika mashariki Mh. Samweli Sitta amesema hakubaliani na kauli ya kusema Tanzania inasubiri talaka kutoka Nchi za Afrika mashariki zinazoonekana kuizunguka EAC. Waziri Samwel Sitta amesema Tanzania inaeneo la 52% katika eac na nchi zinazobaki zina 48% hivyo akasema katika EAC Tanzania ni muoaji kama litatokea jambo baya Tanzania ndio itatoa Talaka.

Naona jibu la Samwel Sitta kwa kiasi fulani limedhalilisha wanawake/wake...kwamba mwenye nguvu, mali (52% ya ardhi) ndiye mwanaume na muoaji, na ndiye mwenye kuamua kutoa talaka! Hivyo wanawake ni kundi 'dhaifu' tu, waolewaji, na hawawezi kutoa talaka...pathetic kuongea huo ujinga Bungeni, and am sure kuna waBunge wanawake walipiga meza kushangilia kudhalilishwa!
 
None-sense!!!wanaacha kujadili mambo ya msingi wana komaa na mambo ambayo yapo waz kila mtu anaelewa ili iweje?
 
Siamini kama Tanzania haitaendelea bila Rwanda, Kenya na Uganda wanafiki hao. Wanataka Tanzania itumie akili zake kupaa kiuchumi maana wanazo hoja za kificho viongozi wao, bado na wao wataparaganyika tu sio mbali. Hilo ni shirikisho la viongozi wao na sio wananchi wa nchi hizo.
 
Naona jibu la Samwel Sitta kwa kiasi fulani limedhalilisha wanawake/wake...kwamba mwenye nguvu, mali (52% ya ardhi) ndiye mwanaume na muoaji, na ndiye mwenye kuamua kutoa talaka! Hivyo wanawake ni kundi 'dhaifu' tu, waolewaji, na hawawezi kutoa talaka...pathetic kuongea huo ujinga Bungeni, and am sure kuna waBunge wanawake walipiga meza kushangilia kudhalilishwa!

Hakuna mahali ambapo Sitta amewataja wanawake wala wanaume.
 
Hakuna mahali ambapo Sitta amewataja wanawake wala wanaume.

Sitta amekanusha 'kusubiri talaka'...akidai Tanzania kwa 'utajiri wake wa ardhi' ndio waoaji na watoa talaka...sasa hapa Tanzania tuna waoaji wa kike?
 
Mimi naona hapa ishu ni kiswahili tu.Uwe muoaji au muolewaji talaka inaweza kutolewa kwa yeyote.Hivyo Membe hakukosea.
Sasa bibie, talaka na itolewe kwa ustaarabu madhali kuna siku utaweza kuniota nimekupakata au umenipakata maadam koo zetu pande zote zinajua tunapendana. Isije ikawa tunalatikiana lakini tunaendelea kuzaa pamoja kwa kificho. Noma yaani mwe!
 
alaa kwa hio ss zanzibar ni wake kwa watnganyika?

nnaona safari hii mke huyu ama atapewa talaka au mme atakua mke yy mara hii
 
"CCM ni kokolo...humu ccm kuna mataahira, makopo, wahuni, etc" capt. John Komba (Mb-Mbinga magharibi) sasa tukiwa na eneo kubwa kiasi hicho what are we earning from it? ukilinganisha na hao wadogo 48%

GDP ya Tanzania ni sawa na combined GDP ya Uganda, Rwanda na Burundi. Population ya Tanzania (Market) ni sawa na combined population ya Uganda, Rwanda na Burundi. Tunaweza kuiwekea vikwazo vya kiuchumi nchi yoyote ndani ya EAC ikapata shida lakini hakuna nchi yoyote ndani ya EAC inayoweza kutuwekea vikwazo tukapata shida. (Ukitaka kupinga huu ukweli uwe na hoja za kutosha)
 
Mimi nawashauri mawaziri wetu waanzishe kundi/bendi ya muziki wa taarabu kabisa.

Ukimsikiliza Membe, Sitta,Wassira, Chikawe, Lukuvi na Mamalao Sofia Simba basi unatambua kuwa raisi Kikwete anajua kubaini ''vipaji spesheli'' hadi akaviteua kuingia katika baraza lake la Mawaziri.

#CabinetModernTaarab
 
Back
Top Bottom