Tanzania haijaolewa EAC - Samwel Sitta

Tanzania haijaolewa EAC - Samwel Sitta

Jana nilimsikia Museveni akiongea kwa tahadhari kubwa kuwa Tanzania haijatengwa bali kwa sasa wanashughulikia Northern Corridor yaani Mombasa - Kampala - Kigali! Baadaye watashughulikia Southern Corridor yaani Dar - Tabora-Kigoma - Mwanza!

Kwa kifupi Museveni, Kenyatta na Kagame wanaelewa umuhimu wa Tanzania katika EAC lakini wanachofanya ni kutoa msukumo kwa Tanzania ili iharakishe kutafakari hoja zao!

Bila Tanzania hakuna EAC!

museveni ni muongo, kwanini hawakumuita JK kwenye mkutano wa kudiscuss hiyo north coridor??
 
Ha ha ha ha ha ha nimeipenda hii Tanzania kwasababu ina eneo 52% huku nchi nyingine zikibakiwa na 48%.Hapa Tanzania ni muoaji kwakigezo cha eneo ngoja wala urojo wakusikie.

Wala urojo wapo na time fahamu kuwa tumeolewa
 
Sitta ajibu ajibuvyo, ukweli ni kuwa Tanzania inafanya mambo yake kwa kujikokota sana kiasi kwamba nchi zingine zenye malengo ya maendeleo haziwezi kuisubiri. Mwalimu Nyerere alituambia mapema kama wenzetu wanatembea sisi tunapaswa kukimbia kwani tuko nyuma sana kimaendeleo. Bado Viongozi wa Tanzania hawana mpango wa maendeleo na wala hawajafahamu kuwa wamechelewa. Wewe miaka yote hii uhuru nchi bado maskini kabisa. Ni watanzaniwania wachache tu wanomudu milo mitatu kwa siku. Ukitoka Dar kwenda Rwanda kuna vizuizi vingi barabarani na hivyo vyote vinarudisha nyuma kasi ya maendeleo ya wenzetu. Siyo hivyo tu bali pia ni mwanya wa rushwa kwa hao walio kwenye vizuizi hivyo. Kama tuna dhamira kweli ya kupata maendeleo na kuwa usafirishaji ni njia nzuri ya kupata pato sioni sababu ya sisi kutokuwa na Reli inayounganisha Tanzania na Rwanda, Burundi na Uganda. Ila kwa kuwa sisi ni wavivu na mambo yetu ya mwendo wa konokono wenzetu hawawezi kutungoja. Ukubwa wa eneo letu siyo hoja ya kuhitajiwa na nchi nyingine. Hoja ni kuwa sisi tuna mchango gani kwa maendeleo ya wenzetu. Sitta aeleze watanzania ni tunasuasua katika mambo muhimu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Tunahitajiana kwa Maendeleo ya Afrika Mashariki. Kama Sitta kazi hiyo ameshindwa ajiuzulu aache usanii atupe majibu yenye substance.
 
Mkuu ime-exclude Kenya hapo? je kwenye GDP ya TZ wote tunazalisha au kwa mawazo yako kwa kuwa tuna population kubwa basi ni soko zuri? how much are we selling to those market achana na wao wanatuuzia nini?Mind you Sitta ameongelea habari za ukubwa wa eneo na wala si faida au hasara tutakayopata kwa ukubwa wa eneo letu, na wewe pia naona unaelekea huko
GDP ya Tanzania ni sawa na combined GDP ya Uganda, Rwanda na Burundi. Population ya Tanzania (Market) ni sawa na combined population ya Uganda, Rwanda na Burundi. Tunaweza kuiwekea vikwazo vya kiuchumi nchi yoyote ndani ya EAC ikapata shida lakini hakuna nchi yoyote ndani ya EAC inayoweza kutuwekea vikwazo tukapata shida. (Ukitaka kupinga huu ukweli uwe na hoja za kutosha)
 
Tanganyika bwana kwa kupenda KUOA, OAO. Mmewao Zanzibar sasa mnataka pia kuwaoa Wakenya, Waganda na Wanyarwanda. Hivi wabunge wale wa CUF haWAkusikia hiyo kejeli Sitta kwamba mwenye eneo kubwa ndiye anaoa, hivyo Zanzibar ni MKE MPENZI WA TANGANYIKA!!

On the seroius note Kama issue ni ukubwa wa ENEO mbona DRC yenye eneo kubwa INAOLEWA na Ka-Rwanda? Hadi tunapeleka wapiganaji wetu kusaidia jahazi DRC?!
 
Hii kauli imenifanya nicheke hadi jamaa alokaa karibu yangu akacheka kwa kunishangaa!!!!!
 
Kwa mawazo yako hao Musaveni na Kagame watakuwa presidents for life au vipi, tujitahidi kuangalia mbele zaidi na sio kujikumbatia na misifa,..mara nyingi ukiwa na tatizo suluhisho la kudumu ni kulifanyia kazi na sio kulikimbia,..
Kwa maoni yako solution ya tatizo uliloliona ni nini?
 
Jana nilimsikia Museveni akiongea kwa tahadhari kubwa kuwa Tanzania haijatengwa bali kwa sasa wanashughulikia Northern Corridor yaani Mombasa - Kampala - Kigali! Baadaye watashughulikia Southern Corridor yaani Dar - Tabora-Kigoma - Mwanza!

Kwa kifupi Museveni, Kenyatta na Kagame wanaelewa umuhimu wa Tanzania katika EAC lakini wanachofanya ni kutoa msukumo kwa Tanzania ili iharakishe kutafakari hoja zao!

Bila Tanzania hakuna EAC!

Hilo ni shinikizo la kichinichini ili Tanzania ijisikie vibaya na kuamua ku-conform na mambo yao mengi ya kihuni.

Tusisahau kwamba watu hawa watatu ni extract ya BAHIMA; an expansionist clan; genociders, dictators and Muderers.
 
Bungeni leo kwenye kipindi cha maswali na majibu akijubu swali la Mbunge John Komba kuhusu EAC Waziri wa wizara ya Afrika mashariki Mh. Samweli Sitta amesema hakubaliani na kauli ya kusema Tanzania inasubiri talaka kutoka Nchi za Afrika mashariki zinazoonekana kuizunguka EAC. Waziri Samwel Sitta amesema Tanzania inaeneo la 52% katika eac na nchi zinazobaki zina 48% hivyo akasema katika EAC Tanzania ni muoaji kama litatokea jambo baya Tanzania ndio itatoa Talaka.

Majibu ya mzaha mzaha, na mipasho kwenye suala linalohitaji kufikiri na kuwajulisha wananchi kilichotokea, kinachotokea na madhara yake kwa mustakabali wa taifa letu na majirani wetu tulionao na uhusiano mkubwa wa kijamii, kibiashara n.k. Ni lini viongozi wetu wajifunza kutumia bongo zao?
 
Hilo ni shinikizo la kichinichini ili Tanzania ijisikie vibaya na kuamua ku-conform na mambo yao mengi ya kihuni.

Tusisahau kwamba watu hawa watatu ni extract ya BAHIMA; an expansionist clan; genociders, dictators and Muderers.
You are very right MTK, tunahitaji sana kuwa macho na hata watu waliopo Serikalini na huko Bungeni ambao wanajiita waha, wahangaza, washubi nk lakini asili yao ni watutsi (hata kama wamezaliwa hapa nchini na kuishi hapa miaka yote hadi leo). Hawa watu lengo na nia yao ni moja; huwa hawatupani na huwa wanafanya vikao vyao vya siri kutekeleza mipango yao. Mliopo makazini, kama unafanya kazi na watu wa aina hii ni kuwa nao makini sana. Ni watu wanaocheka na wewe ukazani ni rafiki kumbe ana lake jambo! Tafuteni waraka wa Mtikila,,,,
 
Hivi mna matatizo gani. Waziri mzima unasema bungeni ati Tanzania ndiyo imezioa Kenya, Rwanda na Burundi, Waziri tena wa huo ushirikiano wa A.Mashariki. Nchi imepatwa na janga gani? Badala ya kutoa hoja mnatukana nchi nyingine, nini hii jamani. Sasa mlivyo, mnataka kuficha uzembe wenu kwenye kutukana ili muwachochee watanzania wawaunge mkono. Viongozi wa ajabu kabisa!!!
 
kwanza kwenye jumuiya tumeingia tu,lakin hakukua na kura ya maoni kuhoj wananchi,,,,watz wengi hatuon umuhim wa EAC,

Mkoroshokigoli, unajuaje wananchi hawaoni umuhimu wa EAC kama hawajapiga kura? WaTz, tangu enzi za Nyerere, wanataka kushirikiana na majirani, na kama sio hujuma za mabeberu ya Kaskazini tungekuwa na Muungano wa nchi zinazotuzunguka: Kemya, Uganda, Rwanda, Burundi, D.R.Congo, Zambia, Malawi (Nyasaland), Msumbiji na Comoro.
 
Mimi nitaendelea kuwa na msimamo kuwa, surely we don't need EAC in the prevailing situation (having Kagame and Museveni with their ideology of creating Bahima Empire). These two are violent tyrants, war mongers, ready to shed innocent blood to have their goals attained. Muungano ni kitu kizuri sana, lakini sio kuungana na watu wenye nia mbaya kama hao wawili!.. Ni watu ambao hawana nia njema na Tanzania, na hata huo muungano wa EAC hawana nia njema nao kwani wana agenda zao za siri!... Tuwe makini sana na hawa watu watutsi (nisieleweke kuwa ni mbaguzi au nina chuki na watutsi, la hasha, ila tabia zao ovu ndio ninazozichukia)...

we jamaa sijui watutsi walishakukosea nini?? katika michango yako yote hapa jf ya kuhusu EAC kazi yako kubwa ni kuwaponda watutsi tu na kuonesha chuki yako dhidi yao, acha ubaguzi usiokua na maana watu wote ni sawa in africa! kwani hujui mtutsi nyerere ndo alitupatia uhuru wa tanganyika!?
 
Ingekuwa ukubwa wa eneo ni hoja, Uingereza isingetwala Marekani na India miaka hiyo
 
2015 kitaeleweka tu, pale CDM ikichukua hatamu ya awamu ya tano, na tena hatutaitaji ilo shirikisho! tutasimama kwa miguu yetu wenyewe...soon enough and i cant wait..
 
Bungeni leo kwenye kipindi cha maswali na majibu akijubu swali la Mbunge John Komba kuhusu EAC Waziri wa wizara ya Afrika mashariki Mh. Samweli Sitta amesema hakubaliani na kauli ya kusema Tanzania inasubiri talaka kutoka Nchi za Afrika mashariki zinazoonekana kuizunguka EAC. Waziri Samwel Sitta amesema Tanzania inaeneo la 52% katika eac na nchi zinazobaki zina 48% hivyo akasema katika EAC Tanzania ni muoaji kama litatokea jambo baya Tanzania ndio itatoa Talaka.

[h=3]Deputy President William Ruto wants EAC members allocated land at Mombasa
Port
[/h]Wacha tuendelee kurushiana maneno
 
Jana nilimsikia Museveni akiongea kwa tahadhari kubwa kuwa Tanzania haijatengwa bali kwa sasa wanashughulikia Northern Corridor yaani Mombasa - Kampala - Kigali! Baadaye watashughulikia Southern Corridor yaani Dar - Tabora-Kigoma - Mwanza!

Kwa kifupi Museveni, Kenyatta na Kagame wanaelewa umuhimu wa Tanzania katika EAC lakini wanachofanya ni kutoa msukumo kwa Tanzania ili iharakishe kutafakari hoja zao!

Bila Tanzania hakuna EAC!

Mkuu kwa uelewa wangu Museven katika jibu lake alijibu tu Kidiplomasia kwani hakuna ukweli wowote katika hicho alicho kisema na iwapo hiyo ndo ingekuwa position basi vikao vingefanyika kwa mujbu wa utaratibu na tunapozungumzia networking na intergration majibu yake yameonesha wao wana Disintergrate na siyo ku intergrate Africa Mashariki.Hata hivyo nadhani fursa ya Tanzani ni ndogo kutokana na Ubize wa viongozi wetu kwenye mambo mengine wanayo yajua wao.Huwezi kudharau soko kubwa kama hili hasa kwa mazao ya Kilimo na kosa kubwa sisi tuna miundo mbinu ya Reli inayohitaji Kuboreshwa tu lakini badala ya kutambua na kuainisha fursa zilizopo we have became too defensive in almost everything kila ukiuliza jibu ni TALAKA...TALAKA...TALAKA...ardhi... ardhi... ardhi...
 
Jana nilimsikia Museveni akiongea kwa tahadhari kubwa kuwa Tanzania haijatengwa bali kwa sasa wanashughulikia Northern Corridor yaani Mombasa - Kampala - Kigali! Baadaye watashughulikia Southern Corridor yaani Dar - Tabora-Kigoma - Mwanza!

Kwa kifupi Museveni, Kenyatta na Kagame wanaelewa umuhimu wa Tanzania katika EAC lakini wanachofanya ni kutoa msukumo kwa Tanzania ili iharakishe kutafakari hoja zao!
Bila Tanzania hakuna EAC!
rejea tena alivyosema Mseveni si Kama ulivyomnukuu. Kuna Uzi humu ambao una press ya marais na unaweza kusikiliza alivyosema kikamilifu. Sikusikia kuwa 'wanashughulikia' northern corridor, bali alifafanua northern na central corridor katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Na hapa alikuwa akikanusha au kufafanua swali au hasa maelezo ya mwandishi kuhusu 'coalition of the willing'.

Pamoja na haya, approach ya hawa marais ni nje kabisa ya utaratibu wa Jumuiya. Maana Kama wanashughulikia miundo mbinu ya ukanda wa kaskazini, Tanzania tulipaswa kuhusishwa na kubwa zaidi ingefuata au kusimamiwa na Sekretariat ya Jumuiya. Mbona tulipokuwa tunajenga barabara ya Arusha Namanga Athi River, nchi zote walikuwa wanahusika, pamoja na kwamba ilihusisha nchi mbili tu za Kenya na Tanzania? Huu si mwenendo mzuri kwa Jumuiya, na nachelea kusema kuwa inaelekea kusiko. Nafikiri sasa kumekosekana viongozi wenye hekima na hasa katika baraza la mawaziri kuwashauri vyema hao Marais. Marehemu Katagaya nafikiri atakuwa anakumbukwa sana Uganda, lakini pia hawa wa kwetu hapa wanashangaza na kauli zao za kuolewa, kuoa na talaka!
 
Back
Top Bottom