Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,197
- 4,120
Tangu wanaume wawaimbie sifa za kuwa na makalio makubwa wanawake ndio wenye soko mjini na vijijini mabinti wamelewa sifa hizo na akili wameweka kando wamebakiza makalio, yawezekana ndio ujana wa sasa ulivyo ila je wamewahi fikiri haya wanayoyafanya sasa huko mitandaoni kama wataweza kutamani kuyaona yakiwarudia miaka 10 mbele?
Kwenye mitandao ya kijamii mabinti wanashindana kuyatikisa makalio yao na kuona ndio ujana na mtindo wa maisha, sawa lakini hivi wanajua kuwa internet haisahau na haya wanayofanya yatawarudia hata wakiwa wazee? Je, watatamani wakutane na vidio zao wakiwa wanatikisa makalio yao hapo baadae? Au ndio wataanza kulaumu watu kufukua makaburi kwa wakati huo?
Tena wengine ni watoto wadogo kabisa miaka 16, 17, 18, 19, 20 hata bado hawajui muelekeo wa maisha yao, hawajui kesho ya wala hawajui wapi wataelelekea, sitaki kuzungumzia kuhusu kuolewa kwa kuwa kuolewa ni maamuzi binafsi na pengine muoaji anapenda hayo maisha. Nazungumzia kwa habari ya kupata ajira kwa watakaotaka kuajiriwa, je, unadhani kuna taasisi itamuhitaji mtu anayetikisa makalio aende kuchafua sura ya taasisi? Au mtu anayejiheshimu anaweza kukupa mchongo mtu wa namna kama yako? fursa zinaweza kukukimbia kwa mtindo wako unaoonesha maadili yako kuwa ya ovyo.
Kucheza ni burudani na ni afya lakini kwa nini ucheze mpaka uutoe au uuvue utu wako? Kwa nini ucheze kama mtu asiye kuwa na maadili? Najua mnaiga wanenguaji hao tayari wameyachanua maisha yao huko, hiyo ni kazi yao ndio inawapa kula kwao na si ajabu akitoka jukwaani hafanyi hayo sasa wewe mdogo wangu unayeanza kurekodi challange ukamtumia msanii akupost unajua unachokifanya kina impact gani kwenye maisha yako ya baadae?
Wanaume mnahusika sana katika hili, mnawapoteza sana mabinti kwa kuwadanganya kuwa kuonesha makalio yao ndio kuwa kwenye soko hali ya kuwa ukweli ni kwamba hamuhitaji mwanamke wa aina hiyo kuwa naye kwenye mahusiano ya kudumu ila mnawafanya viburudisho vya muda tu, hebu waambie kuwa wakiwa na maadili ndio huvutia zaidi ili hicho kichaa kilichowakumba mabinti kitoke.
Kumbuka chochote ufanyacho au uwekacho mtandaoni iwe picha, video au maandishi hakisahauliki kitarudi kwa wakati usiotegemea pengine kitakuokoa au kukuangamiza kabisa.