Kuna mtu nilimuomba 300k akajichunisha baada ya siku 3 akarudi anajichekesha kama hakuona ile text, nimefukuzia mbali, unakuwaje karibu na mtu asiye na msaada.
Hilo limekuwa ni gonjwa. Kuna comment hapo juu inasema kumuomba pesa mwanaume mwanzomwanzo kabisa kabla ya kukoleza mahusiano, ni njia mojawapo ya kumkataa mwanaume. Hilo nimeona ndiyo wazo sahihi.
Hii tabia ya kujaribu akili za wanaume kwa njia ya kuombaomba pesa ovyo, imeacha rundo la wanawake mitaani wakizeekea majumbani kwa wazazi wao.
Kuna kanuni rasmi za kutafuta wenza wa kuoa na zingine si rasmi.
Njia isiyo rasmi ya kutafuta mchumba ama mwenza, ni hii ya kumtamani mwanamke manjiani na kuanza kumtongoza.
Mkikubaliana, ndiyo mwanaume huanza kazi nyingine ya kusaka "particullars" za mwanamke huyo na kukazia dhamira yake.
Wakati haujaanza kupata hata abc's za mwanamke, tayari umeanza kuripuliwa mabomu. Inaingia akilini kweli?
Kunakuwa na tofauti gani kati yako na anayejinadi barabarani?
Hilo la kwanza, jambo la pili kauli za kuwajibikiana kabla hamjawekana ndani na kuanza maisha. Kwamfano unapoanza mahusiano na mwanamke, utasikia anakuuliza 'unajua ninakula nini na kuvaa nini?'
Hivi mapenzi ya urafiki kabla ya kufunga ndoa kuna kuwajibikiana kwa malazi na chakula?
Mambo madogomadogo ya mfano huo yamerudisha nyuma dhamira za wanaume wengi wenye malengo ya kweli ya kuoa wanawake wenye vitabia vya hovyohovyo.
Mwanaume anamuwajibikia kumtunza mkewe bila hata ya kukumbushwa.
Zamani nilikuwa nawadharau sana majamaa wanaokwenda mitaa ya dada poa na kuchagua wanawake kwa kupangiwa penzi kwa njia ya gulio hadi kufikia maridhiano.
Maana yake ni kwamba hao ni bora kuliko wanawake waliojificha kinafiki wakijifanya ni wanawake wema wenye maadili yao, kumbe ni malaya wanaojiuza kisirisiri kwa gharama kubwa kwa kisingizio cha kuomba msaada. Hovyo kabisa.