#COVID19 TANGA: Wanafunzi wakimbia shule kisa hofu ya kuchanjwa

Leo Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Samia Suluhu Hassan Ameongoza Viongozi Wa Juu Wa Serikali
Kuchanjwa Chanjo Ya COVID 19 Aina Ya Johnson And Johnson


Sasa Huko Tanga Wanafunzi Wamekimbia Shule Hasa Hasa Wakihofia Kuchanjwa,Huku Wazazi Wakiwaambia Wasijekuchanjwa Maana
Wataambukiza Wengine Kwa Haraka Sana!!
Mwalim Alipoulizwa Anasema Hali Tete Sana

Wanafunzi Na Watanzania Wapate Elimu

CHANZO: TBC
Kwahiyo ni Tanga sehemu gani?
 
"Kuchanjwa Ni hiari" Wanashawishi watu wachachanjwe serikali kimyaaa akitokea wa kupinga Sasa!!!!
 
Kama viongozi wa dini zenye wafuasi wengi wamechanjwa, waumini wao watawabishia nini kama si kuchanjwa na wao? Ni hiari lakini itakua lazima kuchanja kadiri ya hali ya maambukizi itakavyokwenda
Hii Ni Lazima Maana Top Leaders Kama Ulivyoona
Ila Ni Hatari Kuchanja Viongozi Wakubwa Kwa Pamoja
Wakati Mwingine Tumezungwa Tu
Yaani Wakiumwa Wote Ndiyo Zabayanga Aingie 😂😁😀😉😃😃😃
 
Chanjo ni lazima, wamechanja viongozi wakuu wa serikali na dini, nani atabaki katika watu waliochanjwa? Serikali haitakubali raia wake wapate maambukizi kizembe, hakuna kukimbia
 
Wasiotaka chanjo wapo duniani kote sio Tanzania tu, sasa tusimtwishe tu mzigo Magufuli kana kwamba bila ya yeye Tanzania wasingekuwepo wasiotaka kuchanjwa. Muhimu hapo ni kutoa elimu tu maana hao wanataka kuchanjwa sio wote wana elimu sahihi wengine mkumbo tu na ndio maana hata huko Marekani kuna watu wanachoma dozi moja ya chanjo halafu hawaendi tena kwa dozi ya pili wanaona inatosha ile dozi moja wengine zile side effects walizopata kwa dozi ya kwanza huwafanya wasirudi tena kwa dozi ya pili.
Huo mzigo lazima aubebe, mataifa mengine wapo wasiotaka chanjo lakini hawakuwa na support ya kiongozi wao mkuu, leo hii asilimia kubwa kama sio asilimia 100 ya wale wanaoikataa chanjo nchini wanamnukuu yeye, alikuwa anauwezo wa kipekee kuongea na mwananchi wa kawaida na akamsikiliza... conspiracy theories zipo kila sehemu ila kama watu maarufu ama wenye nguvu wakiziongelea basi raia wengi zaidi wanaweza kuziamini. Utoaji elimu utakuwa ni mgumu sana na hatuwezi kukwepa kwamba uongozi wa awamu ya tano umeaminisha wengi misingi iliyo kinyume na zoezi serikali hii ya awamu ya sita inajaribu kufanya.
 
Kama viongozi wa dini zenye wafuasi wengi wamechanjwa, waumini wao watawabishia nini kama si kuchanjwa na wao? Ni hiari lakini itakua lazima kuchanja kadiri ya hali ya maambukizi itakavyokwenda
Sasa hali ya maambukizi unaijuaje na hatupimi ?
 
Tamko la kijinga kabisa limekwepa maswali ya msingi
1. Afrika ni nchi ipi iliyofanikiwa baada ya kuchanja?

2. Ni kwa nini tupewe chanjo na wazungu waliokufa sana na corona wakati sisi hatujaarithiriwa kihivyo
1. Ili chanjo ifanikiwe lazima zaidi ya asilimia 70 wawe aidha wamechanjwa au wametengeneza kinga asilia mwilini. Ni nchi ngapi Afrika zimefikia hili?

2. Nchi nyingi za Afrika hazijapima asilimia kubwa ya watu wake, au kuweka wazi takwimu halisi za maambukizi na vifo. Kuna uwezekano maambukizi yalikuwa au ni mengi kuliko tunavyodhania. Halafu, hili gonjwa halina mipaka. Tusipolitokomeza duniani litaendelea kuathiri dunia nzima. Kadri maambukizi yanavyoendelea ndivyo virusi hupata mwanya wa kujibadilisha. Itafika mahali hata hizi chanjo zisiweze kudhibiti virusi vilivyojibadilisha. Hii itakuwa hasara kubwa sana kwao. Ndio maana wanasisitiza chanjo kwa dunia nzima. Ingekuwa chanjo ina madhara yanayosemwa wasingeanza na nchi zao.
 
Hili limetokea hata Arusha jana,,kuna shule rafiki yangu mmoja anafanya kazi ananiambia zilikuja gari mbili za Afisa Elimu na Wakaguzi wanafunzi kuziona walikimbia wote tena kupitia madirishani baadhi hakubaki mtu zaidi ya watoto wa walimu wanaulizwa wanadai wenzak wamesema hao watu wamekuja kuwachanja na wazazi wao wamewaambia wasikubali maana kenya wamechanjwa wakafa wengi na watakaobaki hai hawataweza kuzaa tena

Serikali basa wizara ya afya ina kazi ya ziada kuwaelimisha wananchi wake,,hakuna haja ya watu kufanya kama baadhi ya viongozi walio mjiaa Juu GWAJIMA watumie lugha za kueleweka na kuwakumbusha hii sio lazima ni hiyari
 
Akili za hao wazazi zinalingana na akili za hao watoto.Hiyo ndiyo legacy ya mwendakuzimu aliyoacha.
 
Hayati ameacha legacy ya kuogopa chanjo
Ufahamu wako umewekeza kwenye masikio. Wekeza kichwani. Akili za kuambiwa ongeza na za kwako.

1627541667435.png


1627541758410.png


 
Huo mzigo lazima aubebe, mataifa mengine wapo wasiotaka chanjo lakini hawakuwa na support ya kiongozi wao mkuu, leo hii asilimia kubwa kama sio asilimia 100 ya wale wanaoikataa chanjo nchini wanamnukuu yeye, alikuwa anauwezo wa kipekee kuongea na mwananchi wa kawaida na akamsikiliza... conspiracy theories zipo kila sehemu ila kama watu maarufu ama wenye nguvu wakiziongelea basi raia wengi zaidi wanaweza kuziamini. Utoaji elimu utakuwa ni mgumu sana na hatuwezi kukwepa kwamba uongozi wa awamu ya tano umeaminisha wengi misingi iliyo kinyume na zoezi serikali hii ya awamu ya sita inajaribu kufanya.
Watu kumnukuu mtu haina maana ya kwamba hiyo misimamo yao imetokana kwa kumsikiliza huyo mtu tu, mitazamo ya watu wengi kuhusu chanjo inaanzia kwenye mitazamo yao kuhusu hiyo corona yenyewe. Tatizo ni utoaji wa elimu ukiangalia hata sasa ni kiasi gani cha elimu kilichotolewa hadi tuseme maneno ya Magufuli ndio inakwamisha hilo suala la chanjo? Hata waziri Gwajima jana amekiri kiwango cha elimu kinachotolewa ni kidogo.
 
Back
Top Bottom