#COVID19 TANGA: Wanafunzi wakimbia shule kisa hofu ya kuchanjwa

Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
49,008
54,277
Leo Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameongoza Viongozi wa Juu wa Serikali
Kuchanjwa Chanjo ya COVID 19 Aina ya Johnson And Johnson

Sasa huko Tanga wanafunzi wamekimbia Shule Hasa Hasa Wakihofia Kuchanjwa, huku wazazi wakiwaambia wasije kuchanjwa maana
wataambukiza wengine kwa haraka sana!

Mwalim alipoulizwa anasema hali tete sana

Wanafunzi Na Watanzania Wapate Elimu

CHANZO: TBC
 
Hayati ameacha legacy ya kuogopa chanjo
Huu ndio ule msemo alieturoga kafa, alitema sumu halafu kabla ya kuweka mafaili sawa akaondoka...kuna ndugu yangu kajifungua mwezi uliopita, nilimsikia anaogopa kumpeleka mtoto kufuata taratibu za chanjo zilizobakia alivyosikia chanjo ya COVID-19 imefika, anasema wasije wakamdanganya na kumchanja mtoto bil yeye kujua
 
Leo Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Samia Suluhu Hassan Ameongoza Viongozi Wa Juu Wa Serikali
Kuchanjwa Chanjo Ya COVID 19 Aina Ya Johnson And Johnson

Sasa Huko Tanga Wanafunzi Wamekimbia Shule Hasa Hasa Wakihofia Kuchanjwa,Huku Wazazi Wakiwaambia Wasijekuchanjwa Maana
Wataambukiza Wengine Kwa Haraka Sana!!
Mwalim Alipoulizwa Anasema Hali Tete Sana

Wanafunzi Na Watanzania Wapate Elimu

CHANZO: TBC
Tanga ni kubwa,nafikiri ina wilaya karibia 11,kwa hiyo ni wilaya IPI,na ni shule gani hiyo?
 
Taarifa Hiyo Haikutaja Shule Gani Hata Mwalim Hakutajwa Jina
Isije ikawa mnataka tu kutuchafua watu wa Tanga ili tuonekane ndiyo Washaamba!!

Ingawa inawezekana hiyo taarifa ikawa ya kweli maana hata miaka ya 80's tulikuwa tunawaogopa sana watu wenye ngozi nyeupe au magari yenye msalaba mwekundu kwa kuaminishwa eti ni ya wanyonya damu a.k.a Mumian
 
Huu ndio ule msemo alieturoga kafa, alitema sumu halafu kabla ya kuweka mafaili sawa akaondoka...kuna ndugu yangu kajifungua mwezi uliopita, nilimsikia anaogopa kumpeleka mtoto kufuata taratibu za chanjo zilizobakia alivyosikia chanjo ya COVID-19 imefika, anasema wasije wakamdanganya na kumchanja mtoto bil yeye kujua
Wasiotaka chanjo wapo duniani kote sio Tanzania tu, sasa tusimtwishe tu mzigo Magufuli kana kwamba bila ya yeye Tanzania wasingekuwepo wasiotaka kuchanjwa. Muhimu hapo ni kutoa elimu tu maana hao wanataka kuchanjwa sio wote wana elimu sahihi wengine mkumbo tu na ndio maana hata huko Marekani kuna watu wanachoma dozi moja ya chanjo halafu hawaendi tena kwa dozi ya pili wanaona inatosha ile dozi moja wengine zile side effects walizopata kwa dozi ya kwanza huwafanya wasirudi tena kwa dozi ya pili.
 
Kama viongozi wa dini zenye wafuasi wengi wamechanjwa, waumini wao watawabishia nini kama si kuchanjwa na wao? Ni hiari lakini itakua lazima kuchanja kadiri ya hali ya maambukizi itakavyokwenda
 
Leo Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Samia Suluhu Hassan Ameongoza Viongozi Wa Juu Wa Serikali
Kuchanjwa Chanjo Ya COVID 19 Aina Ya Johnson And Johnson

Sasa Huko Tanga Wanafunzi Wamekimbia Shule Hasa Hasa Wakihofia Kuchanjwa,Huku Wazazi Wakiwaambia Wasijekuchanjwa Maana
Wataambukiza Wengine Kwa Haraka Sana!!
Mwalim Alipoulizwa Anasema Hali Tete Sana

Wanafunzi Na Watanzania Wapate Elimu

CHANZO: TBC

Safi sana.
 
Back
Top Bottom