Tanga: Mwanafunzi wa Darasa la 5 adaiwa kujinyonga. Ndugu wadai kuna kitu nyuma ya pazia kinafichwa na Shule na Polisi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Ujumbe huu nimeukuta huko Duniani

Naomba utupazie sauti, kuhusu mtoto wetu Heri Severin Yagaza (11) ambaye anadaiwa kujinyonga shuleni. Heri alikua darasa la 5, shule ya msingi Triple A iliyopo mjini Tanga. Inadaiwa amejinyonga bwenini kwa kutumia shuka, siku ya jumatano saa 10 jioni.

Heri ni Timekeeper (wagonga kengele za vipindi mashuleni) na uongozi wa shule unadai alikua mzima wa afya na alihudhuria vipindi vyote darasani. Alikua mchangamfu kama kawaida yake na ilipofika saa 10 aligonga kengele, kisha eti akaenda bwenini kujinyonga.

Maelezo haya hayakuturidhisha, hasa ukizingatia kuwa tangu saa 10 walipodai amejinyonga, wametupa taarifa familia saa 3 usiku, mwili ukiwa umeshapelekwa Hospitali ya Bombo. Inawezekanaje mtoto ajinyonge shuleni, familia ipewe taarifa masaa matano baadae, tena baada ya kupeleka maiti mochwari?

Tulipofika Bombo, tulikuta Askari polisi na Mmiliki wa shule. Wakatufokea kwanini tumeenda wengi? Wakati wa kuingia kutambua maiti wakasema aingie mmoja tu. Akaingia mjomba wake. Alipoangalia maiti hakuona alama ya kujinyonga. Akahoji mbona mtoto haonekani kujinyonga?

Mmiliki wa Shule na Polisi wakamfokea na kudai yeye si daktari. Hata tulipoomba haki ya kuingia bwenini kuona mazingira anayodaiwa kujinyongea, uongozi wa shule ulikataa na kudai wanaoruhusiwa kuingia ni polisi peke yao.
photo_2023-08-06_12-23-21.jpg

Jana tumekaa vikao na uongozi wa shule wakasema amueni kama mnataka kuzika, au kufungua file afanyiwe postmoterm. Tukaomba haki ya kuosha mwili. Baada ya kuosha tukaambiwa tukazike kwa sababu postmoterm haiwezekani tena. Polisi wakatusukuma tukazike haraka haraka.

Baada ya kuambiwa Postmotetm haiwezekani tena kisa tumeosha mwili, tukaamua kuja kuzika nyumbani hapa Korogwe mjini kwenye makaburi ya familia. Lakini tunaamini hatujatendewa haki.

Uongozi wa shule umetoa jeneza na usafiri, lakini hawajaja msibani. Si mmiliki wa shule, mkuu wa shule, walimu wala wanafunzi wenzie waliofika msibani. Inaumiza sana na tunahisi kuna jambo limejificha. Familia tunaomba tusaidiwe kupaza sauti ili mtoto wetu apate haki yake. Tupo tayari kuahirisha mazishi ili uchunguzi wa kina ufanyike. Tafadhali share kwa wingi ili Serikali ichukue hatua.
 
Hizi Shule hizi!,

jirani yangu bintiye amepata upofu, alipigwa bakora na Mwalimu,akawa anazizuia kwa mkono,kipande kikaruka kwa nguvu na kugusa jicho, wamekaa na mtoto wiki nzima jicho linatoa maji, mpka Matroni alipomjulisha kwa siri mamake! Kwenda ndiyo wakampeleka KCMC!, baada ya mwezi mmoja kulazwa KCMC, wakatoa taarifa mtoto apelekwe India!,ndiyo amerudi ana wiki moja,jicho bado halioni...
 
Jambo linatugusa Sana, lakini pia wanafamilia wamekosea. Kwanini waliomba kuosha mwili wakati walipewa chaguo la kuzika au kufungua file??tayar hapo wamewapa fursa ya kujitenga na jambo hilo.
Huyo dogo kuna asilomia kubwa ameuwawa na uongozi wa chuo wanajua kilichotokea wakaamua kukificha ndio maana wamekuwa wakali wangekaza mwili haukutakiwa kutoka mochuari mpaka uchunguzi ufanyike mbona ukweli ungejulikana
 
Ujumbe huu nimeukuta huko Duniani

Naomba utupazie sauti, kuhusu mtoto wetu Heri Severin Yagaza (11) ambaye anadaiwa kujinyonga shuleni. Heri alikua darasa la 5, shule ya msingi Triple A iliyopo mjini Tanga. Inadaiwa amejinyonga bwenini kwa kutumia shuka, siku ya jumatano saa 10 jioni.

Heri ni Timekeeper (wagonga kengele za vipindi mashuleni) na uongozi wa shule unadai alikua mzima wa afya na alihudhuria vipindi vyote darasani. Alikua mchangamfu kama kawaida yake na ilipofika saa 10 aligonga kengele, kisha eti akaenda bwenini kujinyonga.

Maelezo haya hayakuturidhisha, hasa ukizingatia kuwa tangu saa 10 walipodai amejinyonga, wametupa taarifa familia saa 3 usiku, mwili ukiwa umeshapelekwa Hospitali ya Bombo. Inawezekanaje mtoto ajinyonge shuleni, familia ipewe taarifa masaa matano baadae, tena baada ya kupeleka maiti mochwari?

Tulipofika Bombo, tulikuta Askari polisi na Mmiliki wa shule. Wakatufokea kwanini tumeenda wengi? Wakati wa kuingia kutambua maiti wakasema aingie mmoja tu. Akaingia mjomba wake. Alipoangalia maiti hakuona alama ya kujinyonga. Akahoji mbona mtoto haonekani kujinyonga?

Mmiliki wa Shule na Polisi wakamfokea na kudai yeye si daktari. Hata tulipoomba haki ya kuingia bwenini kuona mazingira anayodaiwa kujinyongea, uongozi wa shule ulikataa na kudai wanaoruhusiwa kuingia ni polisi peke yao.
Jana tumekaa vikao na uongozi wa shule wakasema amueni kama mnataka kuzika, au kufungua file afanyiwe postmoterm. Tukaomba haki ya kuosha mwili. Baada ya kuosha tukaambiwa tukazike kwa sababu postmoterm haiwezekani tena. Polisi wakatusukuma tukazike haraka haraka.

Baada ya kuambiwa Postmotetm haiwezekani tena kisa tumeosha mwili, tukaamua kuja kuzika nyumbani hapa Korogwe mjini kwenye makaburi ya familia. Lakini tunaamini hatujatendewa haki.

Uongozi wa shule umetoa jeneza na usafiri, lakini hawajaja msibani. Si mmiliki wa shule, mkuu wa shule, walimu wala wanafunzi wenzie waliofika msibani. Inaumiza sana na tunahisi kuna jambo limejificha. Familia tunaomba tusaidiwe kupaza sauti ili mtoto wetu apate haki yake. Tupo tayari kuahirisha mazishi ili uchunguzi wa kina ufanyike. Tafadhali share kwa wingi ili Serikali ichukue hatua.
Huyu haelekei ana akili za kujinyonga.
 
Hizi Shule hizi!,

jirani yangu bintiye amepata upofu, alipigwa bakora na Mwalimu,akawa anazizuia kwa mkono,kipande kikaruka kwa nguvu na kugusa jicho, wamekaa na mtoto wiki nzima jicho linatoa maji, mpka Matroni alipomjulisha kwa siri mamake! Kwenda ndiyo wakampeleka KCMC!, baada ya mwezi mmoja kulazwa KCMC, wakatoa taarifa mtoto apelekwe India!,ndiyo amerudi ana wiki moja,jicho bado halioni...
Waalimu hawa,ni wakatili sana.
 
Hivi mtoto wa miaka 11 anaweza kweli kuchukua hayo maamuzi.

Na kwani hao viongozi wa shule wanawalete ukali.

Kuna namna hapo,na vile mbongo wetu hawaaminiki.
 
Huyo dogo kuna asilomia kubwa ameuwawa na uongozi wa chuo wanajua kilichotokea wakaamua kukificha ndio maana wamekuwa wakali wangekaza mwili haukutakiwa kutoka mochuari mpaka uchunguzi ufanyike mbona ukweli ungejulikana
Bado tu changamoto ni je ambaye angeufanyia uchunguzi huo mwili angetoa majibu sahh? Maana hapo inaonekana Kuna kitu huyo mwenye shule anajaribu kukificha ili kulinda reputation ya shule yake
 
Back
Top Bottom