Shule nzima Pangani wameshindwa kuuzia mzungu maandazi kisa lugha ya kiingereza

Covax

JF-Expert Member
Feb 15, 2021
6,276
21,448
Wananchi wa Kijiji cha Mkwaja Wilayani Pangani Mkoani Tanga wamemuomba Mkuu wa Wilaya hiyo Zainab Abdallah kuangalia uwezano wa kuwaongezea Walimu wa lugha ya Kiingereza kwenye Shule zao za Msingi na Sekondari ili kuwafanya Wanafunzi wengi kufahamu lugha hiyo kwakuwa wanashindwa kufanya biashara na Watalii na jana wameshindwa kumuuzia maandazi Raia wa kigeni kisa lugha na hata walipowakusanya Wanafunzi kuongea nae nao walishindwa.

Akiongea kwa niaba ya Wananchi hao, Juma Majidi amesema lugha ya Kiingereza imekuwa tatizo kwa baadhi ya Wananchi kwenye Kijiji hicho na washindwe kufanya biashara na Watalii.

wanaotembelea kwenye maeneo yao “Mhe.Mkuu wa Wilaya, Mama nae yule mzungu mpaka sasa yupo Gesti namuogopa”

Kwa upande wake DC Zainab ambaye anaendelea na ziara ya kusikiliza na kutatua changamoto za Wanakijiji wa Vijiji mbalimbali vya Pangani aliyoipa jina la “Twende na Mama Samia Kijiji kwa Kijiji’ amewataka Walimu wa somo la Kiingereza kutumia lugha hiyo ili kuwawezesha Wanafunzi kupata maarifa ya Kiingereza na pia ameahidi Serikali itaongeza Walimu wa lugha hiyo.

#MillardAyoUPDATES
 
Kwani hao waalimu wenyewe wanajua kiingereza? Labda cha kuandika ila cha kuongea utacheka mpaka basi, nilisha wahi kusikia mualimu moja watuition anaitwa wanafunzi " three both of you come here" aibu tupu.
Kwani hapo haijaeleweka lengo lake nini?Au ukimwambia mzungu hivyo hatokuelewa?Au chukulia mzungu anayeongea kiswahili je sentensi zote arazitamka sawasawa kama wew mwenye lugha yako uliyezaliwa nayo?
 
Wananchi wa Kijiji cha Mkwaja Wilayani Pangani Mkoani Tanga wamemuomba Mkuu wa Wilaya hiyo Zainab Abdallah kuangalia uwezano wa kuwaongezea Walimu wa lugha ya Kiingereza kwenye Shule zao za Msingi na Sekondari ili kuwafanya Wanafunzi wengi kufahamu lugha hiyo kwakuwa wanashindwa kufanya biashara na Watalii na jana wameshindwa kumuuzia maandazi Raia wa kigeni kisa lugha na hata walipowakusanya Wanafunzi kuongea nae nao walishindwa.

Akiongea kwa niaba ya Wananchi hao, Juma Majidi amesema lugha ya Kiingereza imekuwa tatizo kwa baadhi ya Wananchi kwenye Kijiji hicho na washindwe kufanya biashara na Watalii.

wanaotembelea kwenye maeneo yao “Mhe.Mkuu wa Wilaya, Mama nae yule mzungu mpaka sasa yupo Gesti namuogopa”

Kwa upande wake DC Zainab ambaye anaendelea na ziara ya kusikiliza na kutatua changamoto za Wanakijiji wa Vijiji mbalimbali vya Pangani aliyoipa jina la “Twende na Mama Samia Kijiji kwa Kijiji’ amewataka Walimu wa somo la Kiingereza kutumia lugha hiyo ili kuwawezesha Wanafunzi kupata maarifa ya Kiingereza na pia ameahidi Serikali itaongeza Walimu wa lugha hiyo.

#MillardAyoUPDATES
Huyu mzungu aache ujinga anajua anaenda vijijini ambapo lugha inayotumika sio English kwann asiende na mkalimani wake wenyeji wana language zao..
Aache ushamba huyo mzungu.
 
Back
Top Bottom