Tanga: Afisa Upelelezi ashikiliwa na Polisi kwa kudaiwa kuwaachia huru Watuhumiwa wa uhujumu uchumi

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba amesema Afisa Upelelezi Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga anashikiliwa na Polisi kwa kudaiwa kuwaachia huru Watuhumiwa wa uhujumu uchumi waliokamatwa na mali za magendo zenye thamani ya zaidi ya Tsh. Bilioni 1.2.

RC Mgumba amesema September 09,2022 akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama walikamata Jahazi lililobeba baro 170 za vitenge vinavyokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya Tsh. Mil 570 na Watu wanne wakihusishwa na usafirishaji huo ambapo wote walifikishwa Kituo cha Polisi cha Duga Wilaya ya Mkinga kwa hatua zaidi za kisheria.

Pia amesema September 11,2022 Kamati hiyo iliwakamata Watu 20 na Malori mawili aina ya fuso yakiwa na baro 90 za vitenge kila moja “Nimeshangazwa kuona Watuhumiwa wote wanne waliokamatwa na Jahazi wameachiwa huru bila ya taarifa na hawajafunguliwa kesi kama vile hakuna walichofanya, pia Watuhumiwa 15 kati ya 20 ambao walikamatwa na baro 180 za vitenge nao wameachiwa huru ingawa wamefunguliwa kesi za uhujumu uchumi”

RC Mgumba amesema alipofanya kikao na Kamati hiyo ndipo akabaini Afisa Upelelezi Wilaya ya Mkinga ndiye aliyehusika na kuachiliwa kwa Watuhumiwa hao huku akidai amepewa maelekezo na Afisa Upelelezi Mkoa ambae hakuwepo katika kikao hicho.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amesema Afisa huyo wa upelelezi tayari yupo ndani na sheria itafuata mkondo wake “Huyu ni mmoja tu na wale wote walioshiriki kuhujumu zoezi hilo hatua kali zitachukuliwa kwa kila atakayebainika”
 
Ni huko Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga.

Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Mkinga amewatorosha watuhumiwa wa uhujumi uchumi na hawajulikani walipo.

Kwa mjibu wa mkuu wa Mkoa wa Tanga Afisa huyo wa Polisi alidai alipewa maelekezo ya kuwaachia huru watuhumiwa wale na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Tanga.

Afisa huyo amewekwa mahabusu kwa hatua zaidi.

 
Ni huko Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga.

Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Mkinga amewatorosha watuhumiwa wa uhujumi uchumi na hawajulikani walipo.

Kwa mjibu wa mkuu wa Mkoa wa Tanga Afisa huyo wa Polisi alidai alipewa maelekezo ya kuwaachia huru watuhumiwa wale na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Tanga.

Afisa huyo amewekwa mahabusu kwa hatua zaidi.

View attachment 2361782

Mbona mkuu anaonekana amepaniki sana kuhusu suala hili la TShs bilioni 1.2.


FULL VIDEO
MKUU WA MKOA TANGA AMSWEKA MBARONI AFISA UPELELEZI MKINGA TANGA, magendo Tshs bilioni 1.2.


19 September 2022
AFISA upelelezi Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kudaiwa kuwaachia huru watuhumiwa wa uhujumu uchumi waliokamatwa na Mali za magendo zenye thamani ya zaidi ya Shs bilioni 1.2.


Mkuu wa Mkoa RC Omari Mgumba ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa alisema ameshangazwa na watuhumiwa wote wanne waliokamatwa na jahazi kuachiwa huru bila ya taarifa yoyote sambamba na kutokufunguliwa jalada la kesi kama vile hakuna kitu kilichofanyika kwa watuhumiwa hao.

 
Hao watu watajwe majina in public tuwajue, Je wako hai?, akili yangu inakataa mahala.

Hapo Mkinga sio ndio kwenye zile maiti zilizookotwa baharini kwenye viroba? majibu ya tume na upepelezi yako kapuni eeh.

hahahahaha
 
PGO INAENDELEA KUWA MWIBA KWA POLISI

Mkuu wa mkoa hajui kuwa katika jeshi la Polisi ule waraka wa PGO hauzingatiwi, ndiyo maana Mkuu RC umeshindwa kupewa taarifa kamilifu hivyo ni ngumu kupata mtiririko wa jinsi tuhuma za kesi hii inavyochunguzwa.


 
Back
Top Bottom