Katavi: Watuhumiwa 121 wanaswa na Jeshi la Polisi kwa makosa mbalimbali

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limewatia mbaroni watuhumiwa 121 kwa makosa mbalimbali ikiwemo wizi, uzururaji, mauaji na uvunjifu wakiwa na vielelezo vya tuhuma hizo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi, ACP Kaster Ngonyani amesema katika misako mbalimbali inayoendelea katika mkoa huo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 121 wakiwa na vielelezo mbalimbali vya tuhuma hizo.

Aidha, jeshi hilo limewakamanda Watuhumiwa 14 kwa makosa ya mauaji ambayo yametokea kwa nyakati tofauti katika mkoa huo ambapo amesema watuhumiwa wote wanaendelea na mahojiano mara baada ya kubainika na makosa jeshi hilo litawapeleka mahakamani ili kujibu mashitaka ya tuhuma zao.

Katika hatua hiyo Kamanda Ngonyani amewataka wananchi wote wa mkoa huo kuendelea na shughuli zao za uzalishaji mali kwa amani na utulivu hasa katika kuelekea msimu wa sikukuu ya krismas na mwaka mpya.
 
Back
Top Bottom