Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 5,897
- 10,358
Akizungumza leo September 18 katika kipindi cha #Supa Breakfast cha East Africa Radio, Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO ndugu Maharage Chande amedai kuwa Tanzania hakuna kabisa mgao wa umeme bali kuna upungufu
Wateja na wananchi watuvumilie katika kipindi hiki najua ni kigumu kuvumilika na kuelekeweka lakini wafanyakazi wanajitahidi, wizara inajitahidi na serikali inajitahidi kuhakikisha tunatatua changamoto, vile vile uchumi unakua sana kwahiyo ni vizuri na mahitaji ya umeme yanaongezeka, tuko katika kushindana kuzalisha na matumizi ambayo ni mashindano mazuri kwa ustawi wa nchi yetu
Katika mitandao ya umeme hitilafu huwa zinatokea mara kwa mara maeneo mbalimbali huwezi kusema utakuwa na mtandao wa umeme isitokee hitilafu na pale zinapotokea wateja wetu huwa wanafahamishwa lakini pale ambapo tunapata upungufu"
Siyo kwamba nchi nzima hakuna umeme, kuna baadhi ya meeneo yanakosa na pia tunatoa taarifa kwenye hayo maeneo, ni vizuri mwananchi apate taarifa na tumekuwa tukitoa taarifa na tutaendelea kufanya hivyo.