Mbagala mnakata sana umeme
Kuna jamaa yangu anaishi Mbagala Mgeni Nani, Day in Day out analia umeme unakatwa, kinachomkera kuna eneo jirani yao haukatiki!
Mbali na maelezo kuwa kuna matengenezo yanafanyika kwa eneo hili sidhani kama sababu ni hiyo.
 
Mbona hunijibu kuhusu hili

Nawashukru kwa huduma hii, Mi niko Mwanza nina tatizo kama la ndugu hapo juu nimelipia TANESCO-NYAKATO nguzo mbili tangu Tarehe 6 Septemba 2016 hadi leo sijaletewa nguzo, kila siku madai ni hakuna nguzo sasa mi kama mteja hamuoni kama mnanionea?

Ikumbukwe hadi kulipa hiyo pesa kuna huduma niliamua kutozifanya ili nipate huduma ya umeme, badala yake nimekosa huduma zote mpaka leo huku nyie pesa yangu mkiifanyia biashara.

Naomba nipewe ufafanuzi kuhusu jambo hili.

Natanguliza shukrani zangu.


ngoja tusubiri *majibu*
 
Hongereni kwa kutuletea ID hapa ili tuweze kuwapa malalamiko yetu na ushauri pia. Karibuni sana The Home of Great Thinkers JF.
 
Matumizi yangu ni chini ya unit 70 kwa mwezi nilikuwa naomba utaratibu wa kujisajiri ZERO TARIF maana nimejaribu bila mafanikio
 
Matumizi yangu ni chini ya unit 70 kwa mwezi nilikuwa naomba utaratibu wa kujisajiri ZERO TARIF maana nimejaribu bila mafanikio
me nakumbuka walisema nikiona manunuz yangu ni chini ya unit 75 kwa mwezi kwa miezi miwili nilienda ofisin kwao wakanipa karatasi nikaandika barua kama ushahidi nikaacha baada ya muda walinipigia simu kuwa tayari baada ya kukidhi mahitaji..waliniambia nisinunue umeme zaidi ya shilingi 9150 kwa mwezi..

sasa hivi napata raha ya umeme wa TANESCO
 
Hapa kuna watu wanatafutwa- si bure, unaweza kutoa taarifa za mtaa hadi nyumba kabla tanesco hawajafika tayari ushabebwa na wababe
nimeona wamesema kuwa akaunti ipo salama yale yalikuwa maelezo ya mteja walikopi. nilishituka nikajua labda waneibiwa PW lakni wapo vizuri
 
Mi wameshakuja kufanya survey tangia tarehe 17 mach mpaka sasa walisema watatuma msg ya kwenda kulipia but naona kimya mpaka leo.

So naomba mnijuze huwa inachukua Muda gani Baada ya survey?
 
Niliomba kuhamishwa tariff tangu mwaka jana feb kwa sababu natumia chini ya unit 75 kwa mwezi lakini wapiii, pili umeme ukiwa mdogo tu mita yangu ni ya juu inazima mara kwa mara.
 
Niliomba kuhamishwa tariff tangu mwaka jana feb kwa sababu natumia chini ya unit 75 kwa mwezi lakini wapiii, pili umeme ukiwa mdogo tu mita yangu ni ya juu inazima mara kwa mara.


weka na namba ya mita watakusaidia moja kwa moja
 
Back
Top Bottom