Hiki ni nini serikali imefanya?
Yaani majukumu ya TRA wameyaingiza TANESCO ili iweje!
Kodi ya jengo, kodi ya ardhi ni miongoni mwa kodi za kizamani sana zilizopitwa na wakati kama ile kodi ya kichwa!
Ni utwana uliopitiliza kuendelea kukusanya kodi hii kibabe!
Sheria ziko wazi kabisa kwamba chombo kinachosimamia masuala ya kodi ni TRA!
Sasa inakuwaje mambo ya TRA yaingizwe TANESCO kama chombo cha kukusanya mapato?
Usahihi wa takwimu za makusanyo umezingatia vigezo gan kuchukua kodi kupitia LUKU?
Nachojua shirika la umeme Tanzania ni la kiserikali lakini pamoja na yote hayo! Bado haiondoi ukweli kwamba TANESCO ni taasisi ya kibiashara inauza na kusimamia umeme kwa wateja wake!
Sasa kama ni taasisi ya kibiashara kwanini ishirikishwe kwenye uzembe wa TRA?
Yaani kama tutaruhusu huu ujinga wa kila taasisi kutumia LUKU wananchi watakuwa na hali gani?
Haya Leo TRA wanakusanya kupitia LUKU, kesho manispaa naowaombe, keshokutwa NHC nao waombe, dawasco nao waombe!
Huyu mwananchi atakuwa na hali gani?
Kwanza kitendo cha TANESCO Kutumika kukusanya kodi TRA ni kutokuzingatia masharti waliyoyaweka kwa wateja wa umeme kupitia mkataba wa maombi;
Ukisoma masharti ya TANESCO kwenye fomu ya maombi ya umeme TANESCO! Hakuna kipengele hata kimoja palipoandikwa kwamba mteja Usipolipa kodi ya Jengo umeme hautanunulika!
Sasa kwanini Leo mteja anyimwe umeme TANESCO kisa anadaiwa kodi ya jengo?
Huku ni kwenda kinyume na mkataba wa biashara! Nashauri Kwa hili TANESCO tuwapeleke mahakama ya kibiashara kwa kutunyima wateja haki ya kupata umeme kinyume na utaratibu!
Napinga sana huu utaratibu wa TRA kukusanya kodi kupitia LUKU!
Kila mtu afanye kazi yake anayolipiwa nayo mshahara!
Kwamba hebu fikilia unyonyaji huu!
1.ukiwa na wapangaji kwenye jengo moja na kiwanja kimoja wote wanafyekwa kodi ya jengo!
2. Inamaana huu utaratibu kwa wanaotumia solar na majenereta hawalipi kodi
3. Wale ambao hawana umeme hawalipi kodi
4. Ukijenga Leo nyumba na kuweka umeme mwezi huu wa tano wanakutoza kodi kama mtu aliyejenga nyumba zamani!
5. Hakuna elimu yoyote iliyotolewa wananchi tunakutana na kodi kama surpplize pasipo kujipanga! (Usipolipa kodi ya TRA huna haki ya kupewa umeme na TANESCO! (Ebu fikilia mtu unadaiwa 180000 au 240000 usiku! Na usipolipa hupati umeme ajabu sana hili)
Haya yanatokea huko EWURA kuna taasisi inayosimamia walaji wa huduma za umeme imesinzia usingizi wa pono kusubilia mshahara wakati walipaswa hili zoezi watusemee wananchi!
Ebu someni hapa chini masharti ya TANESCO kuunganishiwa umeme kama kuna sehemu pameandikwa kwamba mtu asipokuwa na hela ya kodi ya jengo hataki kupata umeme!
Ardhi kaumba mungu bure, majengo yetu tunajenga kwa gharama ambazo kila vifaa tulivyojengea mlikata kodi!
Lakini Bado mnatufuatilia hadi kwenye LUKU ili iweje?
Nchi hii tatizo siyo walipa kodi, Bali tatizo kubwa ni wasimamizi wa kodi, kwasababu pesa zinapotea kwenye mambo yasiyo na tija
Mfano;
Kuna haja gani kuwa na mkuu wa wilaya/ mkoa awe mwenyekiti wa ulinzi na usalama wakati kuna ma OCD na RPC?
Wakuu wa wilaya na mikoa kila mwaka wananunuliwa mashangingi mapya, mishara na huduma ni nyingi kiasi gani?
Kwanini serikali wasingejikita kupitisha katiba ya kufuta hivyo vyeo ili kutuondolea KODI ZA KIPUUZI ambazo hazina tija kama hizi kodi za ardhi na majengo?