sajo
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 3,022
- 5,254
Jana usiku umeme uliisha kwenye mita yangu. Nikanunua wa shilingi elfu 9 kwa tigopesa, nashangaa muamala unasitishwa kila naponunua. (Ninatumia tarrif ya chini ile) umeme wa elfu 9 unanitosha kwa mwezi mzima.
Ikabidi nipige simu tigo, wakaniambia kuwa mita inadaiwa shilingi laki 1 deni ya kodi ya majengo kwa mwaka 2022/23, kwa hiyo ninunue umeme wa kuanzia Tshs. 100,000/= ndio itakubali.
Kwa kweli nikashangaa na kusikitika sana. Nyumba ni andagraundi, imehesabika kuwa ni ghorofa, na muda wote nilikuwa nalipa elfu 1 kila naponunua umeme. Kama ni limbikizo, sio mimi niliyelizalisha bali ni TRA wenyewe kwa kutonichaji kwa wakati. Ile elfu 1 wanasema waliikata kimakosa, ilipaswa nilipe elfu 5 kwa mwezi kwa kila sakafu
Sasa hii ya kufungia mita ili ninunue umeme wa laki kwa kweli ni uonevu, hapa ndio nimeelewa kwa nini wafanyabiashara wa Kariakoo waliandamana. Yaani usiku umeme umeisha halafu unaambiwa ili upate umeme, nunua wa kuanzia Tshs. 100,000/=, itoke wapi??
Halafu mwaka wa fedha 2022/23 unaisha mwezi huu, Juni 30, maana yake ikifika mwezi wa 7 watanifungia tena ili nilipe wanaloliita deni la mwaka 2023/24 la kodi ya majengo..vyumba viwili vya andagraundi nachajiwa laki na ishirini.. TRA Tanzania hapa mnazingua, mnachofanya ni wizi. Mnashirikiana na TANESCO kutufanyia wizi huo.
Kodi ya majengo kwanza ni kodi kandamizi ya kizamani, badala ya kupeleka majeshi DRC huko walete madini hapa tuuze nyie mnawaza kutukamua sisi wananchi. Yaani mnapowaza mapato chanzo pekee kwenu ni wananchi wenu, hamuwazi kuwapa huduma bora bali mnawaza kuwakamua kodi.
Cha ajabu bunge nalo linakuwa zembe, linatunga sheria halafu linaacha waziri wa fedha ndio awe na jukumu la kupanga kiwango cha Tozo, hili ni jambo la aibu.
Fedha yoyote ya kodi, inapaswa kupitishwa na bunge na sio na waziri. Viwango vipitishwe bungeni, sio kwenye kanuni za waziri. Waziri mwenyewe hajali chochote, yeye ashasema tuhamie Burundi, mtu wa hivi mnapaje mamlaka ya kutamka viwango yeye peke yake??
Hapa nilipo nawaza laki ya ghafla naipata wapi ili ninunue umeme. Japo najua kwa kununua umeme huo nitakuwa nabariki wizi wenu, ila inabidi ninunue ili nisiingie hasara ya vyakula kuharibika na kazi kushindwa kufanyika. Floor za ghorofa si mngezichaji tu kama nyumba mbili, hela iwe ni ya nyumba mbili, kila moja elfu 1.