TANESCO & TRA (Kodi ya Majengo) Wanaposhirikiana kuwaibia Watanzania kilazima!

Chawa wa Zamani

Senior Member
Mar 12, 2023
113
154
Awali ya yote niwaombee utulivu. Timu ya Utopolo waendelee 'kuota' ile ndoto yao sio ya kupata ushindi tu, bali na kuchukua kombe.

Nirudi kwenye mada. Hivi karibuni nilinunua umeme kwa njia ya simu kiasi cha elfu 30k. (Kwa kawaida nina matumizi ya wastani tu ya umeme.) Nikaambiwa nina deni la 100,000 hivyo sitoweza kununua umeme.

Nikaongea na mtoa huduma wa TANESCO (anichekie mita namba yangu). Akaniambia ninadaiwa kodi ya majengo 120k ya mwaka mzima ndani ya mwaka huu wa fedha 2022-2023.

Hivyo, ili niendelee na huduma, inabidi nilipe hiyo "pesa ya majengo" kwani kila nyumba imekadiriwa mfano wa chini 5000 kwa mwezi, na kwa ghorofa kuanzia moja inaongezeka 5000 kadri unavyokwenda juu.

Kwa kuwa pale nina kachumba kimoja juu, basi ikahesabika kama ghorofa moja (kwa mujibu wa sensa na makazi). Hivyo, nikakadiriwa 10,000 kwa mwezi, hivyo basi kwa miezi kumi na mbili ni 120,000. Nikafanya hivyo kwa sababu katika mfumo zao, unalipa kwenye umeme, yaani ukinunua umeme ndio unakatwa huko juu (kodi ya pango).

WIZI WAO WA KULAZIMISHA

Kipindi naongea na TANESCO (customer care), niliwauliza katika mwaka huo huo wa pesa (2022-2023), tayari tumeshakatwa elfu 1,000. Je, hizo pesa zipo wapi? Kwa hesabu inaweza kukaribia 10,000-11,000 (ukiutoa mwezi June unaokuja). Je, hicho kiasi tulichokatwa kabla hio sheria kuanza kazi kipo wapi? Nani atafidia? Customer care wale wakasema hata wao hawana majibu.

Rai yangu! Serikali iache kila kitu wanachofanya muda huu ije hapa mara moja! Itoe majibu sisi mabosi wao "wananchi", pesa yetu ipo wapi? Nani kaila hiyo pesa? Kwanini imekuwa ghafla?... Otherwise, Serikali ijiandae kupandishwa 'kizimbani' ili tuwafunge kabisa gerezani (korokoroni wakazibue kinyesi), kama hawatatoa majibu ya kutosheleza (kuridhisha) juu ya huo wizi, uporaji, unyonyaji (wa kilazima) juu ya mabosi zao "wananchi tuliotukuka kwa uzalendo".

Njooni mjinibu tuhuma mara moja, mimi sio wale wa sijui nakupa siku saba, mie na wale tunaochukua hatua ghafla bin vuu! (hasa nikiwa na ushahidi)
 
Property tax ni sawa.

Ni swala la muda kabla watu hawajaanza thaminishiwa nyumba ilivyo
Mkuu' suala hapa sio kma tunakataa tunachouliza zile Buku Buku zetu tulizokatwa ndan ya huu mwka wa fedha (2022_2023) Zipo wap ili Hali hio Hela ya pango ya mwaka tushalipia?

Wakati n ukuta lakn mie sitosubr n kuisekwa SERIKALI mahakaman kama hawatotoa Majawabu makin!
 
Vjjn huko umeme n bei rais buku 5 unit za kutosha...sasa s wana chaji sm na maybe tv tuu wanakaa hata miez 4 bila units kwisha...umeme ukiisha unashangaa inabd uwanunulie kuazia elfu kazaaa ..hii itapelekea kina bibi hukoo vjjn kuwa na umeme wasio umudu kabsa sku za uson maana hautakubali kununulika..
 
Aliileta magufuli hyo raisi wenu
Kipind hicho tulikatwa Buku 2 ikaja baadae tukakatwa 1000..Sasa hoja n ya mwaka huu wa fedha tu (2022_2023) tangu sheria ianze kufanya Kaz ..hizo Hela makadirio 10000_11000 zpo wap nani kazila ? na kwanin azile Hela zetu Tena kilazima?
 
Mie nilivuta umeme . Vuymba vitatu , kila chumba kina mita yake.
Sasa nashangaa kila mwezi nakatwa kila chumba.
Utartibu upoje ili nijitoe kwenye haya makato
Nenda kawaeleze siku hii Kodi ya pango ikija utatoa 15k Kwa mwez mana majamaa yameamua kutuibia kilazima..
 
Vjjn huko umeme n bei rais buku 5 unit za kutosha...sasa s wana chaji sm na maybe tv tuu wanakaa hata miez 4 bila units kwisha...umeme ukiisha unashangaa inabd uwanunulie kuazia elfu kazaaa ..hii itapelekea kina bibi hukoo vjjn kuwa na umeme wasio umudu kabsa sku za uson maana hautakubali kununulika..
inafkrsha sana..
 
Back
Top Bottom