Tanesco Mbeya kuna tatizo kubwa; mgawo wa ratiba haifuatwi, makali ya mgawo yanaongezeka kila siku

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
2,858
7,847
Shirika la umeme TANESCO mkoa wa Mbeya kuna tatizo kubwa, tunaomba viongozi wa makao makuu pamoja na wizara ya Nishati mliangalie hili. Hali ni mbaya sana. Kuna matatizo yafuatayo:

1. Ratiba ya kile kinachoitwa, "upungufu wa umeme" haifuatwi. Pamoja na TANESCO mkoa wa Mbeya kutoa ratiba hiyo kila wiki inayoonyesha muda ambao line husika zitakosa umeme, ratiba hii imekua ni kama kiini macho tu, kwani haifuatwi kwa asilimia 80. Shida ni nini? Tunashindwa kuelewa, ratiba wanaiandaa wenyewe na wanaikiuka wenyewe.

2. Hali ya upungufu wa umeme inazidi kuwa mbaya kadri siku zinavyokwenda mkoani Mbeya, wakati tulikua tunategemea hali izidi kuimarika. Kwa mfano, pamoja na mvua kubwa kuwa zinanyesha kuanzia December 2023 kwa ukanda huu, pamoja na maeneo ya Ruaha ambayo ndio chanzo kikubwa cha maji kwa bwawa la Mtera, hali ya umeme imezidi kuwa mbaya sana kulinganisha hata na kipindi cha ukame. Pia, tuliambiwa kuwa kuanzia Januari hii majaribio ya bwawa jipya la Nyerere yataanza, hivyo hali ya umeme itaboreka zaidi, lakini hakuna maboresho yoyote sana sana hali inazidi kuwa mbaya tu kwa mkoa wa Mbeya.

3. Nimeambatanisha ratiba ya upungufu wa umeme kwa wiki hii kama mfano. Hii ratiba hadi sasa haijafuatwa kwa asilimia 80. Mfano eneo nililopo, siku ya Jumatatu tarehe 15, kwanza tulilala bila umeme usiku wa kuamkia jumatatu (ulikatika jumapili saa 5 usiku na kurudi saa 11 asubuhi), halafu saa 12 ukakatika tena, ukarudi saa tatu za usiku, wakati ratiba ilikuwa inaonyesha ungerudi saa 12 jioni. Pia, siku ya leo, Jumanne tarehe 16 ratiba yetu ilikua inaonyesha utakatika saa 12 jioni hadi saa 5 usiku, lakini tayari umekatika tangu saa tatu asubuhi.

TANESCO MKOA WA MBEYA INA SHIDA GANI?
Aione kwenye jalada beny jr
 

Attachments

  • RATIBA YA UPUNGUFU WA UMEME - MBEYA JAN 15 - 21 2024.pdf
    542.6 KB · Views: 2
Kuna clip moja twitter nilimwona mzee Dewji akisema matumizi ya umeme yameongezeka kutokana na kuongezeka kwa vifaa vinavyotumia umeme vilivyoingizwa nchini katika miaka mitatu ya mama wa taifa, TV laki sita, friji laki saba, pasi laki tano, majiko ya umeme laki 8, pump za kujazia mafuta elf 60 na blah blah nyingine kibao huku akidai hizi takwimu kazipata TRA.

Kwa hiyo anatafsiri upungufu wa umeme kama maendeleo na kwamba hata bwawa la Nyerere likianza uzalishaji umeme hautatosha maana chini ya mama maendeleo yanaenda kwa kasi watu wengi wananunua vifaa vya umeme.

Sasa nilichojiuliza huo uchambuzi kautoa kama mtaalamu, kalumanzila au kaamua tu kujivika uchawa.​
 
Kuna clip moja twitter nilimwona mzee Dewji akisema matumizi ya umeme yameongezeka kutokana na kuongezeka kwa vifaa vinavyotumia umeme vilivyoingizwa nchini katika miaka mitatu ya mama wa taifa...​
Kaamua kujivika uchawa labda ili apate uwepesi fulani kwenye masuala ya TRA. Bongo ukiwa mfanyabiashara mkubwa lazima ujue "kula" na sirikali. Huyu unaweza kuta kodi anayolipa kwa mwaka kwenye biashara zake ni ndogo kuliko PAYE unayokatwa wewe kwa mwaka mzima.
 
Back
Top Bottom