KERO TANESCO acheni ulaghai, kulikuwa na haja gani ya kusema mgawo umeisha huku watu wa Makongo Juu tukilala gizani siku 3 mfululizo?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Heparin

Senior Member
Sep 24, 2021
127
420
Nashindwa kuelewa kama TANESCO ni shirika linalosimamia maslahi ya umma, nini maana ya kutoa ahadi feki kila siku?

Kwa masikitiko makubwa sana, shirika hili limegeuza kile kinachoitwa 'Mgawo wa umeme' kuwa 'Hitilafu za kiufundi'

Ni siku 3 sasa watu wa Makongo Juu tunapata usumbufu mkubwa kutokana na kukatika kwa umeme usiotangazwa wala kutolewa ufafanuzi. Mathalani, Jana umeme ulikatika mchana, na umerudi saa 1:58 usiku, ukadumu kwa saa 1 kisha ukakatwa tena hadi saa 9 usiku.

Jambo la kushangaza zaidi hata nyakati ambazo umeme unakuwepo, unakuwa na nguvu ndogo sana isiyoweza kuwasha hata feni na friji. TANESCO , hii maana yake nini?

Jana baadhi ya wakazi wa Makongo Juu, usiku wa manane baada ya kuchoshwa na kadhia hii, walijaribu kupigia customer care, wakaunganishwa na mafundi wa eneo hili. Mojawapo ya sababu zilizotolewa ni kuwa transformer 2 za eneo hili zimeungua, hazifanyi kazi hivyo nyaya zimeungwa ungwa tu ili tupate umeme, na zinapozidiwa baadhi ya vifaa vyake huungua, ndiyo sababu kila siku umeme unakuwa unakatika.

Najaribu kuwaza, kama hii ndiyo sababu, kwanini tatizo halirekebishwi? Kuna joto kali, watu wamenunua mboga, wengine wanahifadhi vitu delicate kwenye friji zao, watu wa saluni, mama lishe n.k wote hawa wanategemea umeme ili wafanye kazi. Unapokata umeme unataka waishi vipi?

Kinachoboa zaidi ni kuwa huduma hii ni prepaid, unalipa kwanza ndipo upewe umeme. Inaudhi sana kuona umenunua huduma halafu haipatikani, bora hata ingekuwa postpaid unaamua kutumia kwanza ndipo ulipie, ili pesa nyingine ununue mafuta ya kuwashia jenereta.

Ni ajabu sana kuona mambo haya yanafanyika kwenye zama hizi. Kama tumeshindwa kutoa umeme wa uhakika, tutawezaje kufika nchi ya ahadi kama ambavyo Serikali imekuwa inajinasibu kila siku?

TANESCO fuatilieni changamoto hii na kuipatia majibu. Mnatutesa sana!
 
Ukitaka kuelewa Tanesco vizuri, angalia tabia za wapiga debe na dala dala. Halafu amua namna ya kuishi nao.
 
Tunaweza kufanya masiala kwenye kila kitu, Tanzania ni Nchi yenye maajabu mengi sana
 
Nashindwa kuelewa kama TANESCO ni shirika linalosimamia maslahi ya umma, nini maana ya kutoa ahadi feki kila siku?

Kwa masikitiko makubwa sana, shirika hili limegeuza kile kinachoitwa 'Mgawo wa umeme' kuwa 'Hitilafu za kiufundi'

Ni siku 3 sasa watu wa Makongo Juu tunapata usumbufu mkubwa kutokana na kukatika kwa umeme usiotangazwa wala kutolewa ufafanuzi. Mathalani, Jana umeme ulikatika mchana, na umerudi saa 1:58 usiku, ukadumu kwa saa 1 kisha ukakatwa tena hadi saa 9 usiku.

Jambo la kushangaza zaidi hata nyakati ambazo umeme unakuwepo, unakuwa na nguvu ndogo sana isiyoweza kuwasha hata feni na friji. TANESCO, hii maana yake nini?

Jana baadhi ya wakazi wa Makongo Juu, usiku wa manane baada ya kuchoshwa na kadhia hii, walijaribu kupigia customer care, wakaunganishwa na mafundi wa eneo hili. Mojawapo ya sababu zilizotolewa ni kuwa transformer 2 za eneo hili zimeungua, hazifanyi kazi hivyo nyaya zimeungwa ungwa tu ili tupate umeme, na zinapozidiwa baadhi ya vifaa vyake huungua, ndiyo sababu kila siku umeme unakuwa unakatika.

Najaribu kuwaza, kama hii ndiyo sababu, kwanini tatizo halirekebishwi? Kuna joto kali, watu wamenunua mboga, wengine wanahifadhi vitu delicate kwenye friji zao, watu wa saluni, mama lishe n.k wote hawa wanategemea umeme ili wafanye kazi. Unapokata umeme unataka waishi vipi?

Kinachoboa zaidi ni kuwa huduma hii ni prepaid, unalipa kwanza ndipo upewe umeme. Inaudhi sana kuona umenunua huduma halafu haipatikani, bora hata ingekuwa postpaid unaamua kutumia kwanza ndipo ulipie, ili pesa nyingine ununue mafuta ya kuwashia jenereta.

Ni ajabu sana kuona mambo haya yanafanyika kwenye zama hizi. Kama tumeshindwa kutoa umeme wa uhakika, tutawezaje kufika nchi ya ahadi kama ambavyo Serikali imekuwa inajinasibu kila siku?

TANESCO fuatilieni changamoto hii na kuipatia majibu. Mnatutesa sana!

Uzi kama huu wale makada waaminifu kama kina johnthebaptist ni mwendo wa kupita kimya kimya ..
 
Usiombe transformer liungue halafu kuwe uswahilini hakuna kigogo hata mmoja. Mnaweza kukaa bila umeme wiki. Poleni sana lishawahi nikuta hilo.
 
Back
Top Bottom