Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,117
3,895
Licha ya gaharama za uzalishaji wa umeme kutarajiwa kushuka baada ya kukamilika kwa Bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere (JNHPP) Juni 2024, imebainika kuwa uzalishaji huo hautapunguza bei ya umeme kwa wateja.

Bwawa hilo linatarajia megawati 2,115 za umeme zitakazoingizwa katika Gridi ya Taifa.

Hayo yameelezwa leo Julai 27 na Mkurugenzi wa Tanesco, Maharage Chande katika kikao kazi kati ya Tanesco na msajili wa hazina na wahariri wa vyombo vya habari lengo kuelezea mafanikio na kazi za shirika hilo.

Amesema kwa mwaka 2020/2021 gharama ya uzalishaji wa umeme ulikuwa Sh1.5 trilioni ikilinganishwa na ongezeko la Sh 1.6 trilioni kwa mwaka 2021/2022.

"Mradi wa Mwalimu Nyerere ukikamilika gharama za umeme zitashuka lakini hatutashusha bei kwasababu tutashindwa kwenda," amesema.

Chande alitoa mchanganuo wa matumizi ya umeme kwamba mpaka sasa shirika hilo linawateja milioni 4.4, ambao miongoni mwao wateja wa viwandani ni 4,000 na majumbani zaidi ya milioni tatu.

Kiwango hicho kinawafanya wananchi kutumia asilimia 50 ya megawati 1400 zinazozalishwa na Tanesco kila siku na viwanda nako ni asilimia 50.

Kuhusu upotevu wa umeme, Makamu Mkurugenzi wa uzalishaji umeme Tanesco, Pakaya Mtamakaya amesema mwaka 2020/2021 upotevu ulikuwa wa asilimia tisa lakini kufikia 2021/2022 upotevu ukipungua kufikia asilimia 8.

Amesema sababu ya upotevu wa umeme ni umeme wenye kilovoti ndogo kusafirishwa umbali mrefu na sasa wanaendelea na mkakati wa kupunguza upotecy wa umeme.

Kuhusu bwawa la Nyerere

Ifikapo Juni, 2024 mradi huo utaanza kuzalisha.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma: Habari njema: Bei ya umeme kushuka kutoka Sh.600/= hadi Sh. 35/= kwa unit moja bwawa la Nyerere likikamilika
 
Tulishasema humu jamvini kwamba, viongozi wa Tanzania huwa wanatumia lugha laini wanapotaka ridhaa fulani kutoka kwa wananchi, ila jambo likikamilika wanabadilika.

Kwa kifupi viongozi wetu huwa hawataki kuwambia ukweli wananchi katika hatua za awali, na wananchi huwa tunapenda sana kuamini maneno ya wanasiasa. Binafsi huwa siamini maneno ya wanasiasa wa bongo mpaka nione vitendo.

Siyo kwamba bei ya umeme haitashuka tu, bali bei ya umeme itapanda.

Uzoefu unaonesha kuwa, miradi yote inayojengwa kwa fedha za mikopo, ikikamilika lazima wapandishe bei.

Siyo kwenye umeme, hata SGR ikikamilika lazima bei ya nauli ipande hata kwenye treni ya zamani.Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Licha ya gaharama za uzalishaji wa umeme kutarajiwa kushuka baada ya kukamilika kwa Bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere (JNHPP) Juni 2024, imebainika kuwa uzalishaji huo hautapunguza bei ya umeme kwa wateja.

Pia soma: Habari njema: Bei ya umeme kushuka kutoka Sh.600/= hadi Sh. 35/= kwa unit moja bwawa la Nyerere likikamilika
Au ni masheti ya mikono ya IMF. Ghana wana masharti ya mikono toka IMF kwamba waongeze bei ya umeme. Kwa kuwa hayo masharti nafuu ya mkopo hatuyajui ndo maana inakuwa ngumu sana kujua kwa nini tanesco wanasema hivyo. Mpaka sasa sababu zao ni nyepesi sana.
 
Hebu mwenye atukumbushe vile Prof Muhongo alivyoupamba huu mradi kabla ya kuanza kwake...

Maana wakati huo tuliambiwa kuwa umeme utakuwa wa ziada kiasi cha kuuzia nchi nyingine...

😁😁
 
Licha ya gaharama za uzalishaji wa umeme kutarajiwa kushuka baada ya kukamilika kwa Bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere (JNHPP) Juni 2024, imebainika kuwa uzalishaji huo hautapunguza bei ya umeme kwa wateja.

Bwawa hilo linatarajia megawati 2,115 za umeme zitakazoingizwa katika Gridi ya Taifa.

Hayo yameelezwa leo Julai 27 na Mkurugenzi wa Tanesco, Maharage Chande katika kikao kazi kati ya Tanesco na msajili wa hazina na wahariri wa vyombo vya habari lengo kuelezea mafanikio na kazi za shirika hilo.

Amesema kwa mwaka 2020/2021 gharama ya uzalishaji wa umeme ulikuwa Sh1.5 trilioni ikilinganishwa na ongezeko la Sh 1.6 trilioni kwa mwaka 2021/2022.

"Mradi wa Mwalimu Nyerere ukikamilika gharama za umeme zitashuka lakini hatutashusha bei kwasababu tutashindwa kwenda," amesema.

Chande alitoa mchanganuo wa matumizi ya umeme kwamba mpaka sasa shirika hilo linawateja milioni 4.4, ambao miongoni mwao wateja wa viwandani ni 4,000 na majumbani zaidi ya milioni tatu.

Kiwango hicho kinawafanya wananchi kutumia asilimia 50 ya megawati 1400 zinazozalishwa na Tanesco kila siku na viwanda nako ni asilimia 50.

Kuhusu upotevu wa umeme, Makamu Mkurugenzi wa uzalishaji umeme Tanesco, Pakaya Mtamakaya amesema mwaka 2020/2021 upotevu ulikuwa wa asilimia tisa lakini kufikia 2021/2022 upotevu ukipungua kufikia asilimia 8.

Amesema sababu ya upotevu wa umeme ni umeme wenye kilovoti ndogo kusafirishwa umbali mrefu na sasa wanaendelea na mkakati wa kupunguza upotecy wa umeme.

Kuhusu bwawa la Nyerere

Ifikapo Juni, 2024 mradi huo utaanza kuzalisha.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma: Habari njema: Bei ya umeme kushuka kutoka Sh.600/= hadi Sh. 35/= kwa unit moja bwawa la Nyerere likikamilika
Hapa yaleyale ya gesi ya Songosongo yanaendelea. Mtz hatoenjoy lolote kwenye huu mradi. Wahuni watajipigia,na tusipate chochote kama raia.

Tukitukana tunaambiwa tunakosea😭😭
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom