Tamko la Wapiganaji CCM Feb 10, 2010

Tamko limekuja wakati muafaka?

  • Ndiyo

    Votes: 8 57.1%
  • Hapana

    Votes: 5 35.7%
  • Sijui

    Votes: 1 7.1%

  • Total voters
    14
  • Poll closed .
Mawazo mazuri,lakini harakati za kumpatia Mtanzania ukombozi wa pili haziwezi kuzaa matunda tukiekeza kuishi dunia ya KUFIKIRIKA.Nasema hivyo kwa vile kinachoendelea muda huu Bungeni ni uthibitisho tosha kuwa waraka huu ni wa KUFIKIRIKA maana ingekuwa kutoka kwa the so-called wapambanaji basi tungewaskia wakipinga changa la macho tunalomwagiwa live and direct from Dodoma.
 
aLIYEANDIKA AMETUNGA MANENO YA UONGO TUU,HAKUNA CHA UKWELI WOWOTE HAPO
 
Nafikiri watu wengi tunaendeleza u-Thomaso (Thomas wa biblia) huku ndani tuna hamu ya kuona ili tuamini!!!
 
Nothing good will come out of CCM. Kuwashabikia wajanja kama hawa wazee spin ni kazi bure. Wanaoeka hizi pressure pressure humo ndani ya CCM ni kwamba wapo mbali na mgawanyo wa keki, na ndio kinachowasukuma hawa waganga njaa.
 
maneno matamu sana yametumika na kweli kidogo nimejisikia nafuu kuona kuna watu ndani ya ccm wanafikiria hivi.kwa vile mda ni mchache sana kufikia uchaguzi ni vizuri wangetaja mpaka tarehe ngapi wanataka hao watu waliowataja wawe wameshachukuliwa hatua na kama hawajachukuliwa hatua ifikapo tarehe hio wao wapiganaji watafanya maamuzi gani?

mbinu za vita nyingi kweli na ni vizuri njia yako ya vita hiwe siri.mpaka sasa ni mwanzo mzuri tu waliofikia lakini bila kuweka tarehe ya wao kuchukua maamuzi mimi naona nachukulia kama uoga wakuwa responsible na kauli zao na ndio nia kubwa ya kuficha majina yao.

kama hatua haitochukuliwa hawa wapiganaji watarudi kujichanganya na hao mafisadi hili waendelee kuwa kwenye nafasi zao walizokuwa nazo sasa.

vita vya siasa ni tofauti na vita vya jeshi,kama wao wamejiandaa kisawa sawa na wana jiamini sioni kwanini wameshindwa kuhitisha waaandishi wa habari kwa pamoja na kutoa hili tamko.

kama wao wanaogopa kujitokeza mbele ya jamii ,wanategemea vipi sisi tuwe na moyo kwao kwamba wako tayari kuokoa taifa letu?
 
Nadhani kuna watu wanamiss pointi kubwa sana ya ujumbe huu; ndani ya CCM kuna wapiganaji wa kweli na wapiganaji uchwara; wapiganaji wa kweli hawajali wabunge wa CCM wanafanya nini Bungeni au wanachama wengine wanafanya nini; wao wanapigana.

Ninavyoelewa ni kuwa mstari umechorwa ardhini sasa kati ya wale wanaCCM walioweka Chama kwanza kwamujibu wa ibara ya 14:1 na wana CCM ambao wameamua kujitenga 'nao'. Ukiniuliza mimi I'll stand with these people than their opponents. CCM has been put on notice.

Nimemuuliza mmoja wao leo anasema mambo ya Ngoswe mwachie Ngoswe, wanajua wanachofanya na tamko hili ni kuwapa notice JK na uongozi wa juu wa CCM. Ati wamefunika kombwe mwana haramu apite.. lakini "haendi kokote"!
 
The same 'ol BS! Hakuna lolote hapo wala nini. Miaka kumi toka sasa mambo yatakuwa kama yalivyo sasa. Mafisadis don't die, they multiply.
 
.....what if nimeandika mimi NL na kuusambaza kny net tu? nani ataujali? Je, katika hayo yaliyoandikwa ni jipyi jipya kwako? kwani huwa hatupigi kelele hapa kuwa watu walihusika na ufisadi ulioainishwa kny doc wawajibishwe ikiwa ni pamoja na kuondolewa kny chama?

Kwa maoni yangu, uliokotoka huo msimamo ni muhimu kufahamika na pili, tujue nani alikusudiwa kuupata (public, m/kiti wa CCM, media)....vinginevyo ni kutwanga maji kny kinu tu......mnatoa mapendekezo halafu hamsemi nani ahakikishe yanafanyiwa kazi? yaani wahusika wayapate through rumours, sioni kama ni effective means of communication!

- Ni maoni yako tu, sio yangu na sio lazima yawe ya wengine, cha muhumu ni yana masilahi gani kwa taifa, aliyeandika sio tija kwangu cha muhimu ni message naa yes yaliyoandikwa mengi ni mapya kwangu na hasa mpangilio wake.

- Kufanyiwa kazi ni uamuzi wa kila mtu humu na uwezo wake si unajua kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake, humu ndani kuna watu wengi na wenye nafasi mbali mbali sasa do not underestimate uwezo wa members humu kufikisha huu ujumbe unapotakiwa, aliyeandika sio muhimu kama vile ambavyo sio muhimu kujua wewe ni nani, muhimu ni ujumbe wako na masilahi yake kwa taifa!

Respect.

FMEs!
 
Kama wangekuwa wapiganaji wa kweli wangepeleka hiyo hoja kwenye vikao vya CCM.ila hiyo karatasi na nembo ya CCM hata mimi naweza viandaa na nikajiita Bondia na si Mpiganaji tu.
 
Wapiganaji gani hao wasiokuwa na majina? Au ndo kuganga njaa kwenyewe huko?

Cheki wapiganaji hata kunukuu Mwongozo Wa CCM 1981 wanashindwa kutofautisha neno HUKO na UKO, huu ni ubabaishaji, nakubaliana nawe naona walikuwa wanaandaa hii doc wakiwa na wasiwasi na nafsi zao : Quote ''

Uko nyuma tulishinda katika mapambano yetu kutokana na umoja wetu wa kitaifa,
usahihi wa siasa yetu na uongozi bora wa Chama. Leo na katika siku za usoni tutahitaji
umoja imara zaidi, siasa sahihi na uongozi bora wa chama.. vibepari na vibwanyenye
vya humu nchini vimeonyesha dhahiri uhasama wao dhidi ya maslahi ya wakulima na
wafanyakazi, umoja wa sasa lazima usimame juu ya misingi iliyo wazi na sahihi,
misingi ya ujamaa; kwa hiyo ni umoja wa wakulima na wafanyakazi na wale wote wanaounga
mkono kwa vitendao ujenzi wa ujamaa nchini. – Mwongozo wa CCM, 1981''

''viongozi wa Chama katika ngazingazi mbalimbali na jumuiya mbalimbali na kundi la wanachama wa​
kawaida.....''

Pia Johnson Mwanyika ana cheo gani ndani ya CCM kiasi cha kushikiwa bango, au anatumiwa kama media stunt (kikaragosi) cha kuwazuga Watanzania, maana Johnson Mwanyika amekwisha staafu kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali!
 
Kama wangekuwa wapiganaji wa kweli wangepeleka hiyo hoja kwenye vikao vya CCM.ila hiyo karatasi na nembo ya CCM hata mimi naweza viandaa na nikajiita Bondia na si Mpiganaji tu.

- Ingebadilisha, kupunguza au kuongeza nini tofauti na CCM kuupata kwa njia hii? Halafu hiyo principle inatuweka wapi JF? Wapiganaji kweli au wababishaji?

Respect.

FMEs!
 
moto umewashwa.. tofauti imewekwa wapo wapiganaji na wapo wapiganaji wa kweli; wapiganaji wameonekana wakiunga mkono wizi na uporaji wa raslimali zetu.. wapiganaji wa kweli.. wamekana kuwa sehemu ya maamuzi yaliyofikiwa jana usiku Dodoma. Anayefikiri kuwa suala la Richmond limefikia mwisho anaota njozi.. subirini mtaamini kuna tofauti kati ya maembe na machungwa japo yote ni matunda.
 
- Ni maoni yako tu, sio yangu na sio lazima yawe ya wengine, cha muhumu ni yana masilahi gani kwa taifa, aliyeandika sio tija kwangu

Correct!

..cha muhimu ni message
....Correct lakini, hiyo message imefikaje kwa mlengwa? message ngapi hawa watu wamepelekewa /wamepeta lakini hakuna kinachotokea?

naa yes yaliyoandikwa mengi ni mapya kwangu na hasa mpangilio wake.
.....naweza kukubalina na upya wa mpangilio, sio contents mzee? ebu niambie kati ya hao walioorodheshwa hapo, ni nani ni mgeni kwako na umestuka kuona katajwa kny tamko?

- Kufanyiwa kazi ni uamuzi wa kila mtu humu na uwezo wake si unajua kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake, humu ndani kuna watu wengi na wenye nafasi mbali mbali sasa do not underestimate uwezo wa members humu kufikisha huu ujumbe unapotakiwa, aliyeandika sio muhimu kama vile ambavyo sio muhimu kujua wewe ni nani, muhimu ni ujumbe wako na masilahi yake kwa taifa!
Mzee humu ndani hili tamko ni sensitive kuliko information zooote zilizowahi pitia hapa mkuu? what makes this one iwe special sana kwa ''anyone mwenye uwezo'' hapa ndani kulifanyia kazi tamko hili? tulishaona mambo mengi sana humo ndani ambayo yanaunyeti mkubwa sana kwa maslahi ya Taifa and yet tukabakia kugongana miguu na vichwa na no action yeyote iliyochukuliwa na viongozi wetu.....!

Angalia issue ya Chenge vs Radar vs BAE......unasikia kinachotokea upande mwingine wa dunia on the same issue, sisi tunafanya nini na kina Chenge?Je, hizo information hazikupita hapa tena zikiwa zimeiva mkuu?

Respect.

FMEs
Cheers!
NL
 
Kabisa!wanaficha majina yao na sura zao wanadai wapambanaji upuuzi mtupu!
Hao no baadhi ya wabunge ambao katika kipindi chote cha ubunge walikuwa wakizurura na biashara ya vikoba wakasahau kusimamia shughuli za maendeleo katika majimbo yao.baada ya baadhi ya wanachama kuona udhaifu huo wameamua kutangaza kugombea nafasi hizo nao wamejumuishwa na kuitwa vikaragosi vya mafisadi.ama mbongo mwendo mdundo
 
Correct!

....Correct lakini, hiyo message imefikaje kwa mlengwa? message ngapi hawa watu wamepelekewa /wamepeta lakini hakuna kinachotokea?

.....naweza kukubalina na upya wa mpangilio, sio contents mzee? ebu niambie kati ya hao walioorodheshwa hapo, ni nani ni mgeni kwako na umestuka kuona katajwa kny tamko?

Mzee humu ndani hili tamko ni sensitive kuliko information zooote zilizowahi pitia hapa mkuu? what makes this one iwe special sana kwa ''anyone mwenye uwezo'' hapa ndani kulifanyia kazi tamko hili? tulishaona mambo mengi sana humo ndani ambayo yanaunyeti mkubwa sana kwa maslahi ya Taifa and yet tukabakia kugongana miguu na vichwa na no action yeyote iliyochukuliwa na viongozi wetu.....!

Angalia issue ya Chenge vs Radar vs BAE......unasikia kinachotokea upande mwingine wa dunia on the same issue, sisi tunafanya nini na kina Chenge?Je, hizo information hazikupita hapa tena zikiwa zimeiva mkuu?

Cheers!
NL

- Siku zote tatizo lako ni moja for some reasons known to yourself, huwa unaamini kwamba unawakilisha mawazo ya watu wote, I don't know why?

- Sasa unasema nini kwamba wakijua majina ya walioandika ndio watachukua hatua? Unasema wakijua majina yetu hapa JF, basi ndio watatusikiliza zaidi kuliko sasa hawayajui?

Respect.

FMEs!
 
- Siku zote tatizo lako ni moja for some reasons know to yourself, huwa unaamini kwamba unawakilisha mawazo ya watu wote, I don't know why?
.....sijaelewa hii imekujaje hapa mkuu! siku zote......huwa....???
- Sasa unasema nini kwamba wakijua majina ya walioandika ndio watachukua hatua? Unasema wakijua majina yetu hapa JF, basi ndio watatusikiliza zaidi kuliko sasa hawayajui?
...hayo unayoandika ni yako hoja yangu ni kwamba, yaliyopo kwenye tamko si mapya hapa JF. Wewe unasema ni mapya...sielewi huo upya unakujaje? nimekubaliana na wewe kwamba huo mpangilio wa hoja zao unaweza kuwa ni unique lakini content yake tushaizoea sana hapa!

Jipya kwangu ingekuwa hili tamko liko addressed kwa public moja kwa moja thorugh radio, magazeti, TVs na liwe signed na hata mtu mmoja like kiongozi wa hao wapiganaji! Hapo kungekuwa na uzito zaidi, na watu wengi sana wangeweza kuliona, kuliko sasa ni mimi na wengine wenye access na hizi net na wajanja wameweza kuliona.....! hayo ndio maoni yangu mzee!

Respect.

FMEs!
Cheers!
NL
 
.....sijaelewa hii imekujaje hapa mkuu! siku zote......huwa....???

...hayo unayoandika ni yako hoja yangu ni kwamba, yaliyopo kwenye tamko si mapya hapa JF. Wewe unasema ni mapya...sielewi huo upya unakujaje? nimekubaliana na wewe kwamba huo mpangilio wa hoja zao unaweza kuwa ni unique lakini content yake tushaizoea sana hapa!

Jipya kwangu ingekuwa hili tamko liko addressed kwa public moja kwa moja thorugh radio, magazeti, TVs na liwe signed na hata mtu mmoja like kiongozi wa hao wapiganaji! Hapo kungekuwa na uzito zaidi, na watu wengi sana wangeweza kuliona, kuliko sasa ni mimi na wengine wenye access na hizi net na wajanja wameweza kuliona.....! hayo ndio maoni yangu mzee!

Cheers!
NL

- Hayo ndio maoni yako kwamba hakuna jipya, maoni yangu ni kwamba mengi yaliyomo humu ni mapya, then tatizo liko wapi?

Resepct.

FMEs!
 
- Ni maoni yako tu, sio yangu na sio lazima yawe ya wengine, cha muhumu ni yana masilahi gani kwa taifa, aliyeandika sio tija kwangu cha muhimu ni message naa yes yaliyoandikwa mengi ni mapya kwangu na hasa mpangilio wake.

- Kufanyiwa kazi ni uamuzi wa kila mtu humu na uwezo wake si unajua kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake, humu ndani kuna watu wengi na wenye nafasi mbali mbali sasa do not underestimate uwezo wa members humu kufikisha huu ujumbe unapotakiwa, aliyeandika sio muhimu kama vile ambavyo sio muhimu kujua wewe ni nani, muhimu ni ujumbe wako na masilahi yake kwa taifa!

Respect.

FMEs!

Kwenye red hapo humu JF tunapeana thanks si kwa vile namjua ni nani ila nagonga thanks kutokana na hoja yake kwa hiyo hakuna ulazima wa kuwajua ni akina nani muhimu ni content ya hoja zao.Period.
 
Back
Top Bottom