Tamko la Wapiganaji CCM Feb 10, 2010

Tamko limekuja wakati muafaka?

  • Ndiyo

    Votes: 8 57.1%
  • Hapana

    Votes: 5 35.7%
  • Sijui

    Votes: 1 7.1%

  • Total voters
    14
  • Poll closed .
Kuficha majina yao inawezekana ni mbinu yao ya kupambana, tusubiri muda si mrefu tutawafahamu kwa majina.
 
hii yaweza kuwa propaganda kutoka upinzania (thinking out of box)


Upinzani upi huo unaweza kufikiria na kutoa kitu kama hiki...I mean wale wote waliopo upinzani wanaoweza kuandika dossier kama hii wana uhakika na majimbo yao. Hakuna motive iliyo na mashiko kuwashuku upinzani.




 
nimeshindwa kusioma maana imejaa porojo na uchochezi kila siku ni kulalamika lini tutatenda? Che Guevara na wanamapinduzi wengine hawakuwa watu wa porojo bali ni utendaji
 
china wananyonga kama mtu ulikuwa fisadi.....hapa tanzania kesi mpaka mahakama inachoka kusikiliza kesi za mafisadi.....sasa tuwe na sheria inayoeleweka kasi yoyote ya ufisadi iwe na limit kwa kusikilizwa na judgement itikoke mapema...hakuna jipya chini ya jua.
 
Wewe ndio umeruhusu itoke? Maana naona imetolewa na Enigma.

Hii inaitwa DIVORCE PAPER

Kwa style ya uandishi na hata nukuu hii kitu ni ya kutoka kwa wenyewe kabisa. Sasa kama ni mtu mmoja au kakundi miongoni mwao ni lingine. Hii ikiwekwa vizuri ni Ilani tosha ya uchaguzi.

Sasa wameweza kuwataja watuhumiwa bila kujitaja wao? Huu ni upungufu mkubwa sana kuacha statement iliyosheheni uzalendo kama hii mpaka damu inachemka bila ya kuweka majina.

Hapo ndipo inapoonyesha ukosefu wa kujiamini wa wanasiasa wa Tanzania. Toka uhesabiwe kwa mema au mabaya na sio kujificha ficha!

Hii kitu ukisoma ni uandishi wa mwanakijiji lakini ameandika hisia za kina Sitta/Malecela kuelekea kikao cha Kamati Kuu na NEC ya CCM kinachotarajiwa kukaa hivi karibuni.

Kwa bahati mbaya CCM ya kufanya maamuzi haya ilikuwa ya hayati Nyerere. Hivyo hoja hizi zitaaishia hewani kwa kuwa zilikuja pia kupitia CCJ!

Jitihada zote hizi zitakuwa na maana kama zitaipasua CCM lakini kama zitaendelea kuwachanganya wananchi kuhusu ni yupi hasa masiha wa kuleta mabadiliko Tanzania basi zitakuwa zinarudisha nyuma harakati zote za wanahabari na wanasiasa wakweli.

PM
 
Jamani msipende kuangalia vitu in isolation.. jaribuni kuangalia kila kitu kwa ukaribu wake na umoja wake... why now?
 
Inawezekana kuficha sura na majina siyo kwasababu ya kuona haya. Ni kwasababu ya mbinu za mapambano ndani ya medani ya vita.
Yote haya yanadai tena kwa sauti kali kwamba hakuna tena muda wa kupoteza katika kufany mabadiliko. Mwenye macho haambiwi ona.
Tunakoelekea uongozi utataka mtu uonyeshe nini umekifanya. Siku hizi uongozi ni tiketi ya kuhudhuria makongamano kwenye hoteli za nyota tano ndani na nje ya nchi, tukiwa tu watanashati na kuzunguka dunia nzima bila kuwa na agenda ya kueleweka zaidi ya kuomba omba kama Matonya.
 
Tanzaia kila siku tunavumbua movie ambazo haziendi theather, unaangalia kwa kusikiliza na kusoma.
 
Lisemwalo lipo kama halipo..............

Kabisaaaa. Unakumbuka kuna watu humu jamvini waliwahi kusema CCJ haipo, ni uzushi. Leo tunaiona hadharani.

Siku hizi mambo yamebadilika, 'redio mbao' zina data za uhakika na za haraka kuliko vyombo rasmi vya habari. Si unakumbuka Tiger Woods?

HAPA KUNA KITU.
 
Hii kitu ukisoma ni uandishi wa mwanakijiji lakini ameandika hisia za kina Sitta/Malecela kuelekea kikao cha Kamati Kuu na NEC ya CCM kinachotarajiwa kukaa hivi karibuni.
PM


Hata mimi mwenyewe nimeipenda kwa sababu hiyo; imebeba mawazo yangu mengi. Sasa hivi ukiangalia kuna watu wengi wanaandika kwa staili yangu kiasi kwamba siwezi tena kubeba ujiko wa uandishi wa aina yangu. But.. no.. siyo ya kwangu.. niko busy kwa mambo makubwa zaidi kuliko migongano ndani ya CCM. Nilishaandika hisia zangu kuhusu upiganaji CCM, and I'm still standing on them.
 
Hata mimi mwenyewe nimeipenda kwa sababu hiyo; imebeba mawazo yangu mengi. Sasa hivi ukiangalia kuna watu wengi wanaandika kwa staili yangu kiasi kwamba siwezi tena kubeba ujiko wa uandishi wa aina yangu. But.. no.. siyo ya kwangu.. niko busy kwa mambo makubwa zaidi kuliko migongano ndani ya CCM. Nilishaandika hisia zangu kuhusu upiganaji CCM, and I'm still standing on them.

DU.....kweli wewe ni wa majuu......
 
Bila ya RA kweli orodha hiyo imekamilika? Hao ndio CCM ya sasa. Pengine tufanye kinyume chake. Ambao hawakutajwa wajiondoe CCM. Waende CCJ kama inavyosemwa
 
Samahani wakuu... yaani nimeanza kusoma tu! nikakutana na "uko nyuma'... badala ya "huko nyuma"

ilitusumbua hii lack ya umakini kwenye AGOA kama mnakumbuka; anyway good move but dangerous;

Don get me wrong, i support the move but WHO ARE THESE PEOPLE? KAMA WAMEWEZA KUTAJA MAJINA YA WATUHUMIWA KWANINI YAO YAWE HAKUNA?

Could this be a conspiracy move to victimise wapigananaji waambiwe wao ndio wameandika?

With email ya jumla, inawezekana pia kwamba mtu mmoja anweza kuchukua liberty ya kuwa mwakilishi?

Once again, its a daring move... but it needed to come more strategically than that... i see huge potential ya victimization for a few

good for the day
 
muhimu ni kusubiri,ila subira inatakiwa iwe na limits zake,so wasitumie muda mwingi kutusubirisha jamvini,tafadhali....
 
hii yaweza kuwa propaganda kutoka upinzania (thinking out of box)
mimi naamini wewe ndio upo ndani ya Box, kwasababu hata mwenyekiti wa chama hicho/CCM alikiri wazi kuwa kunampasuko wa dhahiri shahiri ambao umepelekea wanachama wake hata kuogopana na kuchukiana kiasi cha kutoaminiana na kuachiana glass za maji kisa watawekeana sumu...maneno ya JK Kikwete MWENYEKITI WA CCM na Rais wa JMT.
vita inafukuta ndani ya chama hicho kikongwe, mtafaruku upo, Makamba hawezi kuimba wimbo mmoja na Mwakyembe, Serukamba Peter haimbi shairi moja na Kimaro, Lowassa agongeani glass na Sitta.
kweli ni vigumu kudhani kwamba hawa ni wanachama wa chama kimoja cha siasa.
Huo waraka mbona ni marejeo tu ya harakati zakuwataka kizazi cha mafisadi kiondoke ndani ya mfumo wa utawala .
hakuna lingine, awe kaandika Kingunge ama Tambwe hiza, maudhui ni kua , mafisadi ni wanyama na wanyonyaji na ni wakoloni weusi.
 
Back
Top Bottom