Hatuwezi kamwe kukubali kwa namnayoyote ile.
yoyote ile kuendelea kukaa na wahusika wa kashfa hizo kwa kisingizio au sababu
!
tutajitokeza mstari wa mbele, maana nnchi hii imekosa mtu wakujitoa muhanga kama Mrema alipojaribu miaka ile, tunahitaji watu wa aina ile, lakini tuwe tayari kwa mapambano.Mimi nafikiri wamechelewa kuwasha moto.
Washa moto ikibidi ongeza nguvu kupitia chama chochote. Mapambano ni kushinda au kushindwa hila kwa mapambano haya nina uhakika Ushindi ni lazima.
Nakumbuka Mbowe mwaka 2005 alisema ni kupiga kiberiti tu.
Tanzania ya sasa inasubiri nani aanzishe. Ngoma ikisha pigwa wachezaji ni wengi tu.
wamejawana uwoga na ufitini hawana lolote ni wivu tu unawasumbua na roho ya kwanini?mngekuwa wapiganaji mngekuwa mnapokea posho mara mbili kama sio upunguani ni nini?
baada ya kumkamata tayari ukombozi wa watanzania utakua umepatikana.....?Wapiganaji wanaficha majina yao?
Basi na sisi huku kwetu Kyela tuongeze madai yetu. Wale waliofanya yafuatayo wasimamishwe:
- Walioiba pesa za mafuriko na wakajengea mahekalu Kunduchi
- Walioba michango ya shule na wakanunua majengo ya NBC Tukuyu,
- Waliolipwa mamilioni kwamba wanaenda kutibiwa Ujerumani kumbe walijifungia hapo Kunduchi.
- Wale wanaoteka wapiga kura wao na kuwafungia majumbani kwao.
- Wale wanaochukua posho mbili kinyume na sheria.
Ningeona wa maana kama wangeombe serikali iwachukulie hatua watu wanaotuhumiwa kwa madhambi mbalimbali. Lakini kusema chama kiwafukuze watu uanachama wakati hawajashitakiwa na chombo chochote nafiki ni mawazo yaliyojaa chuki zaidi kuliko uongozi bora.
Wakitaka tuwaelewe wajitoe CCM na kupoteza mafao yao, hapo ndio tutajua kweli wana nia njema. Mbona Mrema alijitoa na kupoteza kila kitu na wananchi tulimwunga mkono.
Mzee hii ni tungo tata, hasa hapo kwenye red. La muhimu iwe imetoka kwako ama umeruhusu itoke au hukuruhusu itoke, bado tamko kama tamko, limebeba bango ambalo mwanaccm yeyote makini yafaa apime na achukue maamuzi sahihi ya nini kinachofaa kwa sasa!Hapana.. kwa upande wangu.. Enigma hawezi kutoa chochote hapa bila ya ridhaa yangu, at least not kwa kutumia handle hiyo ya Enigma. Sijui nani aliruhusu itumwe huko ilikotoka.
Huu ni unafiki tu ndugu zangu wana JF. Hawa jamaa kama ni wapiganaji wangetaja majina yao halafu nasi tutambue ni akina nani. Kufanya hivyo, kungesaidia kupunguza maswali kwa mfano "je, kama huo waraka umeandikwa na mtu mmoja tu na akaamua kutumia neno kundi?" Je, kama siyo wanachama? Huu ni woga tu ndugu zangu. Upiganaji hauishii na kutaja maneno kama mlivyo/ulivyofanya kwa kuweka waraka hapa jamvini! Tuwajue sasa ili hata kuna wengine tungependa kuungana nanyi tuelewe. Vinginevyo, nyie siyo wapiganaji maana mnaogopa kujitokeza hadharani kwa manufaa ya wengi kuwapa nguvu juu ya hilo. Natoa mfano, Dk. Slaa alijitokeza japo hakuwa na si wa CCM watu wakamuona wakati anatangaza orodha ya mafisadi kipindi kile. Tabia yetu watanzania tulio wengi tu wazembe wa kusoma. Je, wanaCCM wasioingia humu jamvini kwa mfano watapateje taarifa hizi? Nashauri tunapoamua kujitokeza kwa ajili ya kutetea au kuanzisha vuguvugu lenye lengo la kuleta maboresho kwenye jamii kisiasa, kiuchumi na kijamii tusiwe vinyonga.mmmh .......hawa wapiganaji hawana jina? au ndio usawa ule ule wa siasa za `kuogopana` na `kuoneana haya`?