Tamko la waislam wa Tanga

nadhani iwapo wakatristo nao watadai fidia kutokana shule na mahospitali yao yote yaliyotaifishwa na nyerere serikali hii itafilisika kwa sababu wakati wa uhuru shule na mahospitali karibu yote makubwa yalikuwa ya wakristo. Hata kikwete mwenyewe alisomea kwenye shule za kikristo zilizotaifishwa na nyerere.

Ndugu zangu waislamu wanakosea sana kukubali kudanganywa kuwa eti serikali inafanya kazi kufurahisha wakaristo na kusahau jinsi ambavyo taasisi za kikristo zinavyoisaidia serikali katika huduma mbalimbali za kijamii. Inawezekana mikoa ya tanga na dar es salaama hawapati huduma hizo, lakini kwenye mikoa mingi kama ile ya kati, kaskazini, kusini na kanda ya ziwa kuna huduma nyingi sana zinazotolewa na taasisi za dini ambazo zilitakiwa ziwe zinatolewa na serikali; kwa mfano mahospitali ya rufaa ya kcmc na bugando, na mahospitali mengineyo mengi sana.
pia hawa hawa wanaopiga vuvuz ndio wanaoongoza kutibiwa ktk hosptali hizo.
 
Bravo ma-shekh!!
Ongezeni kipengele kingine kwamba:- Michango na sadaka zote zinazotolewa makanisani zigawanywe nusu nusu moja ibaki kanisani nusu nyingine wapewe waislam kwani ndiyo walochangia wakristu kupata hiyo sadaka!!!
 
hakudanganya ila alisema serikali imeongeza ruzuku hiyo ili huduma za afya zifikie watu wengi zaidi.
Uzuri ni kwamba hakulazimishwa kuongea hilo ila alisema kwa uwezo wake.
Hivyo basi nawaomba wenzangu mkikutana naye misikitini muulizeni kulikoni mbona nyie hawapigii pande???? Pia mkullo si uwa mnakutana naye, waulizeni hela wanatoa za nini?? Si ni wenzenu.
Na pia kuna mawaziri na manaibu waislam waulizeni kwa nini huwa hawapingi hayo malipo kwenye mikutano ya baraza la mawaziri??? Mwisho waambieni waumini wenu wote wasiende kutibiwa kwenye hospitali za kanisa ili ijulikane kuwa pesa zinawasaidia wakristo tu.

i love your comment pal!!!!
 
1. Kuna daraja huko Kigoma lilijengwa na Wamisionari wa Kanisa Katoliki (huu ni mfano mmoja tu).
2. Nilienda Kiloleni (nadhani iko Mombo) miaka ya 1980s barabara iliyokuwa inatumika na usafiri vilikuwa mali ya Kanisa Katoliki.
3. Nilienda Kisiwa cha Kome miaka ya 1990s boti iliyokuwa inatumika kusafirisha watu kwenda na kutoka kisiwani Kome ilikuwa mali ya Kanisa Katoliki.
4. Nina mifano pia kutoka nchi nyingine kama Malawi, Zambia na Msumbiji.
5. Soko tayari kuwatetea mafisadi wanaotuibia na kutufanya tushi kwenye umaskini wa kutupwa wawe Wakristo au wasio Wakristo.
Mkuu mimi sina tatizo na hapo kwenye Red, najua kama Kanisa Katoliki inafanya kazi zake kama Institute swali langu mimi taingia mwanzo ni hawa wanaojitapa kama wasomi wa Tanzania wamelisaidiaje taifa kutoka kwenye dimbwi la umasikini? zaidi ya kutuletea umasikini
 
mwisho wa uelewa wao utauona just wait. kwa sababu wewe ni kama mbuzi, mbuzi ukimzungumzisha atakusikia lakini hatokuelewa lakini ukimpa bakola ya mbavu atakuelewa. so wait at the end utawaelewa nini wanachozungumza
Aaah! kwa hiyo una mpango wa kutupa bakola ya mbavu, eh?
 
Nasubiria tamko la wapiga debe wa stendi kuhusu mchakato wa kuhuisha katiba ya Tz, kwani inaelekea kupata mpya labda mtu afe- uhenda hili la ruzuku lingeshughulikiwa ipasavyo.
Nchi hivi sasa imejaa matamko, sijui ni nani anaweka kumbukumbu ili baadaye kufuatilia utekelezaji.
Anyway, ndo tulipofika
 
Hivi wakikosa jambo la kufanya kwa nini wasiendelee na michezo yao ya bao kwenye vijiwe vya kahawa na kashata!
 
Shule ndio tatizo,huo mgawo kama upo kwa nini wao wasiuombe?duh kazi kwelikweli
 
Hawana jipya tumeshawazoea.Muhimu kwao ni kuwagawa watanzania kwa misingi ya dini zao.Na kwa jinsi wasivyoipenda CHADEMA muislamu wa karatu au wa wilaya ya mbulu wanamuona kama si mwenzao.
 
Nadhani iwapo wakatristo nao watadai fidia kutokana shule na mahospitali yao yote yaliyotaifishwa na Nyerere serikali hii itafilisika kwa sababu wakati wa uhuru shule na mahospitali karibu yote makubwa yalikuwa ya wakristo. Hata Kikwete mwenyewe alisomea kwenye shule za kikristo zilizotaifishwa na Nyerere.

Ndugu zangu waislamu wanakosea sana kukubali kudanganywa kuwa eti serikali inafanya kazi kufurahisha wakaristo na kusahau jinsi ambavyo taasisi za kikristo zinavyoisaidia serikali katika huduma mbalimbali za kijamii. Inawezekana mikoa ya Tanga na Dar es Salaama hawapati huduma hizo, lakini kwenye mikoa mingi kama ile ya Kati, kaskazini, kusini na kanda ya ziwa kuna huduma nyingi sana zinazotolewa na taasisi za dini ambazo zilitakiwa ziwe zinatolewa na serikali; kwa mfano mahospitali ya rufaa ya KCMC na Bugando, na mahospitali mengineyo mengi sana.

Hata Dar es Salaam wanapata huduma hizo.

1. Kanisa Katoliki pale 'opposite na Mlimani City' jirani na Kanisa la Kakobe wana shule ya chekechea (English Medium) na hospitali. Ukienda pale utakuta watu mchanganyiko.

2. Kanisa Katoliki pale Temeke (karibu na kituo cha Polisi Chang'ombe) wana kituo pia cha watoto wadogo.

3. Kanisa Katoliki Mbagala Mission wana hospitali ya Mission huwa imejaa watu wa kila aina - wenye vilemba, vibandiko nk na sidhani kama ni Wakristo, ambao huwa wanajifanya kuvaa hijabu ili waonekane ni Waislamu wakati ni Wakristo.

4. Hii ni mifano michache tu na wengine wanaweza kuwa na mifano mingine pia kutoka Dar es Salaam. Hata makanisa mengine yanatoa huduma kama hizo Dar es Salaam.
 
Mkuu mimi sina tatizo na hapo kwenye Red, najua kama Kanisa Katoliki inafanya kazi zake kama Institute swali langu mimi taingia mwanzo ni hawa wanaojitapa kama wasomi wa Tanzania wamelisaidiaje taifa kutoka kwenye dimbwi la umasikini? zaidi ya kutuletea umasikini

Nadhani jibu unalo mwenyewe. Cha muhimu ni:

1. Kwanza orodhesha mazuri unayoyajua
2. Halafu orodhesha mabaya unayoyajua
3. Kisha ujiulize hayo mazuri yanatoka wapi na hayo mabaya yanatoka wapi?
4. Mwisho utakuta - kuna baadhi ya mazuri na wewe umechangia na kwa baadhi ya mabaya yanayotokea umechangia pia!
5. Hivyo, 'don't look for the root cause of our problems from external forces; start with internal forces including yourself'.
 
inasikitisha tz bado kuna watu tena wengi tu, wanafikiria kwa kutumia nyayo za miguu na sio ubongo..pamoja na yote ila BADO TUTAFIKA TU
 
Dah nimesoma coments zote moja baada ya moja, jaman hv nani katufikisha hapa?kudharauliana,kukejeliana,matusi ya kidini n.k tumesahau waislam na wakristo tumeoleana,tumeishi pamoja kwa upendo kwa miaka mingi tu.
Mimi ni mwislam tena kwetu ni Tanga-muheza ingawa cpo huko kwa sasa.
Kusema wazi hao waliotoa hilo tamko nadhani hawakuona athari zake, unajua ina hitaji reasoning kuandaa tamko lolote hata kama ni in family situation.
Sharti la kutaifisha mali zote za wakrisho i.e mashule,mahospital n.k hili halitawezekana, na kupiga hesabu ruzuku walizopata wakristo then jumla yake waislam pia wapewe nalo ni impocbo pia,
Hv mmetafakari kwa kina kama hospital na taasisi zote za wakristo zikikataa kutoa huduma kwa waislam, je hakuna athari yoyote kwa hilo,

Jaman ndugu zangu watanga hata kama kuna dhuluma mnayodai ipo cdhan kama masharti mliyoyatoa ndio suluhisho, wakristo wanapewa ruzuku kutokana na huduma wanazotoa na huwa hazibagui dini na kwa ushahidi wa hilo mm mwenyewe nimetibiwa holispital mbali mbali za kanisa tena bila ubaguzi, kwa hili acheni niwe mkweli.
Suluhisho ya matatizo ya waislam si kuendekeza visasi na kulalamika bali ni kutafuta elimu kwa bidii zaidi ili kusaidia ustawi wa jamii. Tujenge mashule,mahospital n.k ili ndugu zetu wasome coz elimu ni muhimu sana kwa maisha ya sasa!Then Bakwata kama taasisi ya ustawi wa waislam ina wajibu gani kwa maendeleo ya waislam? je shule ngapi za Bakwata zimejengwa tangu mwaka 90 tu mpaka sasa?wakristo hupeleka proposal ulaya na hupata misaada je Bakwata inafanya hivyo kwa nchi za kiarabu?mana ninavyojua waraabu ni matajiri mpaka pesa zao wanaenda kuwekeza timu za soka ulaya mf. bilionea wa Man city. Je Bakwata wana mpango gani endelevu kuwasaidia waislam kielimu i mean kujenga vyuo n.k? Hatuwez kulalamika ikiwa hatuonyeshi juhudi za dhati za kuandaa mazingira ya elimu kwa watoto wetu.
Wakati leo hii wakristo wanajenga shule,vyuo n.k Bakwata kupitia mufti wanapiga kelele kuilaumu Chadema eti inavuruga amani.

Chadema ni chama cha siasa kinachopigania haki ya kila mtanzania mnyonge,
Japo waislam kwa ujumla hawaipendi Chadema kutokana na sumu ya udini anayoihubiri Kikwete lakini bado vijana wasomi nikiwemo mm hatujakubali kudanganyika na propaganda na tar 16 wazalendo tunaandamana kupinga muswada wa katiba mbovu! je ndugu zangu waislam katiba bora tunayoipigania ni kwa ajili ya wakristo tu.

Angalizo, wakristo ndugu zangu hapa JF acheni jazba nk maneno ya kejeli mfano kahawa na kashata sijui ubwabwa hayafai, tujaribu kumuelimisha mtoa mada na waislam kwa ujumla ukweli na hali halisi,naamini si makosa yao bali elimu imewapita pembeni hasa ukizingatia waislam wasomi wapo asilimia ndogo tuki compare na wakristo hivyo, sote ndugu moja kiasi kwamba tupo watu kama mm hatuwez kukubali mifarakano ya kidini mana itakua ni kilio na huzuni kwasababu nina ndugu wa damu kabisa wengi wakristo na ndugu wa damu kabisa waislam na tunaishi kwa upendo tu.
Tanzania ni yetu sote bila kujali dini.
 
  • Thanks
Reactions: F2S
Back
Top Bottom