Jamani sisi wakristo inabidi tujilaumu wenyewe na kutubu kwa mabaya tuliyoyayafanya ktk nchi yetu,ebu tuangalie ile mikataba ya buzwagi,melemeta,angalia Epa,dowans,angalia mauaji ya mwembe chai,mauaji ya zanzibari na ya karume lengo letu lilikuwa tuitawale nchi lakini tumeipelekea nchi kutambaa sasa,nchi inayumba,hata hii elimu tunayojigamba nayo haina maana kabisa,vizazi vyetu tumeviandalia mazingira magumu sana hapo baadae,
Nadhani umefika wakati sasa tuihurumie hii nchi masikini,tumeila vya kutosha hebu sasa tufanye kazi kwa maendeleo ya taifa letu kwa vizazi vya sasa na baadae,