TAMISEMI: Serikali inatoa elimu bila ada sio elimu bure

habari wadau..!
Ukisoma hiyo thread hapo chini,utatambua kuwa mawazo mazuri huwa hayapati uchangiaji mwingi.

Niliandika kuhusu swala la elimu bure jinsi linavyotakiwa kupatiwa ufafanuzi ili wananchi waelewe vizuri na si kuliweka kisiasa

Nashukuru muheshimiwa Silinde sijuhi alipita humu juzi kalitolea ufafanuzi na kuweka uelekeo mpya katika elimu yetu.

Swali 18 May 2018👇👇👇
 
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, David Silinde amesema serikali inatoa elimu bila ada sio elimu bure hivyo wazazi washiriki katika kutoa michango mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya shule...
Ila kwenye majukwaa ya siasa wananchi tulidanganywa ni Bure. Ila Mimi siku zote nikapinga nikasema tena ni ghali sana si Bure kwa sababu zufuatazo:
1. Nauli analipa Mzazi ila wakati wa Bure tulipanda train au bus kwa warrant
2. Tunajinunulia chakula wakati zamani chakula cha Bure kiko shuleni
3. Tunanunua vitabu wakati zamani vitabu ulikuwepo shuleni
4. Tunanunua madaftari na pencil na pen wakati zamani tulivukuta shuleni
5. Tunanunua magodoro wakati zamani tuliyakuta shuleni
6. Ongeza wewe maana sasa kichwa kimeniuma


Eti ni Bure tunajitapa. Watanzania tatizo huwa tunapokea Paroko za kisiasa tunaacha kutumia akili. Yaani sijui aliyetuloga. Utasikia Yaani elimu ni Bure. Ninaangalia huku natikisa kichwa.
 
Habari wadau..!
May 18 2021 niliandika uzi kuhusu swala la elimu bure lisifanywe kisiasa ila wawaeleze hali halisi wazazi na wasiwazuie kuchangia nashukuru TAMISEMI wamejibu (coincidence) hii ni hatua nzuri sana inatoa matumaini makubwa kwa uongozi wa rais Samia Hassan.


 
Ili kuepuka kupata kiongozi aina ya Magufuli ni vizuri tukipata katiba mpya.
Tusijisahau na Mama Samia.
 
Nchi mbov kabisa sanaa tupu sasa kwanini wanangangania madaraka, na wanaoweza kutoa elimu bure bure kabisa wapo
 
Kwenye Ilani ya Chama mbona mmendika mtatoa Elimu bure na mkajinadi hivyo majukwaani?.

Ndio kusema mliwahadaa watu?
 
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, David Silinde amesema serikali inatoa elimu bila ada sio elimu bure hivyo wazazi washiriki katika kutoa michango mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya shule.

Aidha Waziri wa Elimu, Joyce Ndalichako amesema waraka wa serikali namba 3 wa 2016 ulieleza ushirikishwaji wa wazazi katika maendeleo ya shule lakini shule hairuhusiwi kufukuza watoto kwa sababu ya michango ya maendeleo ya shule.

Majibu hayo yalikuja baada ya Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Aida Khenani ambaye alisema kwa sasa michango inaendelea ila kwa kibali maalumu cha kudai michango hiyo.


Ongeza volume aisee
 
Teknolojia hiyo
20210607_134442.jpg
20210607_134438.jpg
20210607_134432.jpg
20210607_134435.jpg
 
Ukweli ni mchungu sana,
Kuna watakaopata ya kusema hapa,
Lakini huo ndio ukweli,
Na ukweli daima hukuweka huru,
Hongera sana mama
 
Back
Top Bottom