TAMISEMI: Serikali inatoa elimu bila ada sio elimu bure

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,613
2,000
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, David Silinde amesema serikali inatoa elimu bila ada sio elimu bure hivyo wazazi washiriki katika kutoa michango mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya shule.

Aidha Waziri wa Elimu, Joyce Ndalichako amesema waraka wa serikali namba 3 wa 2016 ulieleza ushirikishwaji wa wazazi katika maendeleo ya shule lakini shule hairuhusiwi kufukuza watoto kwa sababu ya michango ya maendeleo ya shule.

Majibu hayo yalikuja baada ya Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Aida Khenani ambaye alisema kwa sasa michango inaendelea ila kwa kibali maalumu cha kudai michango hiyo.

 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
47,053
2,000
Ndiyo nini sasa? Kumbe tatizo ni jina ada na siyo michango? Basi na ada iitwe mchango.
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
23,632
2,000
Msibadilishe kauli - sisi tunajua msimamo wa Serikali ilikuwa Elimu BURE hadi kidato cha nne, masuala ya kubadilisha sentensi na kuwa eti Elimu bila Ada sisi halituhusu na hatulitambui.

Mbona hamkuyasema haya wakati marehemu akiwa hai - msituchanganye.
 

data

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
23,262
2,000
Kwani wanaogopa nini kukiri kuwa sera hii imefeli.

Hivi huenda bado Magufuli anaogopwa eehh.

Aisee... Ana Mzimu mkali sanaa.
 

Natena wiza

JF-Expert Member
Mar 13, 2021
312
500
Tunajua hamuoni uwezekano wa kuendelea na ile system kasababu hela hamna kwasasa. Twambieni tu, sisi tupo tayari kuchangia kila kitu kama ulivyokuwa zamani.
 

Nyambi Sr

JF-Expert Member
Apr 17, 2021
418
1,000
msibadilishe kauli - sisi tunajua msimamo wa Serikali ilikuwa Elimu BURE hadi kidato cha nne... masuala ya kubadilisha sentensi na kuwa eti Elimu bila Ada sisi halituhusu na hatulitambui.

Mbona hamkuyasema haya wakati marehemu akiwa hai - msituchanganye !!
He he eeeee sisiemu kwa kupinduka tik Tak wapo vizuri wangekuwa wanatumia rafu hizo kuleta maendeleo tungekuwa mbali sanA
 

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
3,307
2,000
Mapato kwa mwezi kutoka trion mbili hadi trion 1.2 na bado huko yatashika hadi b 800 si anataka watu walipe kodi kwa kubebelezwa
𝚃𝚞𝚜𝚒𝚖𝚜𝚒𝚗𝚐𝚒𝚣𝚒𝚎 𝚑𝚊𝚝𝚞𝚓𝚊𝚠𝚊𝚑 𝚔𝚞𝚔𝚞𝚜𝚊𝚗𝚢𝚊 𝚝𝚛𝚒𝚘𝚗 2 𝚔𝚠𝚊 𝚖𝚠𝚎𝚣𝚒 𝚣𝚊𝚒𝚍𝚒 𝚝𝚞𝚕𝚒𝚔𝚞𝚜𝚊𝚗𝚢𝚊 𝚝𝚛𝚒𝚘𝚗 1.6
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
42,435
2,000
Habari hii ni kwa mujibu wa JamiiForums ambapo Silinde amenukuliwa Bungeni akiseme, "serikali inatoa elimu bila ada, sio elimu bure na kwamba wazazi watapaswa kutoa michango".
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom