Selous,
Asante. Nakushukuru kwa changamoto na hasa kwa kuanzisha mchango kwa lengo hilo. Kesho kuna kikao muhimu. Nitawasilisha wazo hili ambalo sasa limekuwa kilio cha wengi, ikiwa ni pamoja na Chadema kuwa na akaunti ya YOUTUBE. Nitawajulisha wapenzi wetu maamuzi ya kikao hicho ambayo iwa[po yatakubalika yatapaswa kupitishwa na Vikao vya maamuzi ambavyo navyo vinatarajiwa kukaa siku chache zijazo. Nakushukuru tena, na ninatoa mwito kwa wale wote ambao wangelipenda TV na Radio ya Chadema waendelee kutoa mawazo yao. Ukombozi uko kwenye kona na utalertwa na wenye moyo. Kuchangia jambo jema halihitaji utajiri wa mali bali zaidi wa moyo na uchungu kwa Taifa letu linaloangamizwa kwa spidi na kasi ya ajabu na mafisadi. Natanguliza shukrani za dhati kwa wanahadema na wapenzi wetu kwa ushauri wa mara kwa mara. Tunazingatia yote