Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,853
- 1,310
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Magharibi, Mhe. Tauhida Gallos Nyimbo na Mbunge wa Viti Maalum Vijana Tanzania, Mhe. Amina Ali Mzee wameendelea na Kampeni Mkoa wa Arusha huku wakiwaombea Kura kwa Wananchi Wenyeviti wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji wanaotokana na CCM ili CCM ishinde kwa kishindo nchi nzima.
Tauhida Gallos na Amina Mzee walioungana na viongozi mbalimbali wa CCM Mkoa wa Arusha na Jumuiya zake kumpokea Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Ndugu Rajabu Abdulrahman Rajabu (MCC) alipofika kuzindua kampeni kwaajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Unaotarajiwa Kufanyika tarehe 27 Novemba, 2024.
Akiwa Arusha, Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Vijana Tanzania, Mhe. Amina Ali Mzee akiwa ameambatana na Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Arusha na viongozi wengine wamepita mtaa kwa mtaa hasa kwenye masoko na kuwaombea kura wagombea wa CCM Wilaya ya Arusha Mjini.
Aidha, Mbunge Tauhida Gallos na Mbunge Amina Ali Mzee wakiwa Mkoani Arusha wamefika Wilaya ya Monduli katika Kata ya Islaley ambapo wameungana na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mhe. Fredrick Edward Lowassa kuendelea kuomba kura za wagombea wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Vilevile, Mbunge Amina Ali Mzee na Mbunge Tauhida Gallos Nyimbo wameeleza kwa kirefu sababu za msingi kwanini Watanzania wanapaswa kuendelea kuipa dhamana CCM ya kuongoza Serikali, wameeleza miradi mbalimbali inayotekelezwa nchini ikiwemo Sekta ya Utalii, Ujenzi wa Arusha Airport, Ujenzi wa Uwanja wa Michezo Arusha utakaotumika kwenye AFCON 2027
PIA SOMA
- LIVE - LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Attachments
-
WhatsApp Image 2024-11-26 at 05.45.30.jpeg715.9 KB · Views: 3
-
WhatsApp Image 2024-11-26 at 05.45.29.jpeg799.5 KB · Views: 3
-
WhatsApp Image 2024-11-26 at 05.34.14.jpeg795.6 KB · Views: 3
-
WhatsApp Image 2024-11-26 at 05.30.34.jpeg753.2 KB · Views: 3
-
WhatsApp Image 2024-11-26 at 05.30.33.jpeg686.8 KB · Views: 3
-
WhatsApp Image 2024-11-26 at 05.45.08.jpeg801 KB · Views: 4
-
WhatsApp Image 2024-11-25 at 18.49.16.jpeg79.1 KB · Views: 3
-
WhatsApp Image 2024-11-26 at 05.37.24.jpeg656.3 KB · Views: 3